Kutana na Watu Hawa Hapa JF.

magnifico

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2013
Posts
11,075
Reaction score
24,634
Tangu nianze kutumia hii forum miaka kadhaa nyuma kuna vitu nimegundua humu JF. Vingine vinaelimisha, vingine vinaburudisha na vingine vinashangaza pia.

Sasa pamoja na kuwa hii ni forum ya ma-great thinkers kuna baadhi ya vijimambo havizuiliki toka kwa member wa humu humu.

1. Great Thinkers.

Nisingependa kuwataja kwa ID ila wapo wengi tu. Na ukitaka kuthibitisha jaribu kuufuma uzi wa uongo hata kwa mwaka mzima halafu njoo upost hapa uone.

Kuna nyuzi zinaandikwa kuhusu matukio fulani yaliyopata kutokea hadi unafurahi mwenyewe jinsi hoja zinavyoibuliwa. Hawa mara nyingi huwa wanabisha kwa hojabkuliko mihemko.

2. Wasoma Heading.
Hawa jamaa wapo sana na njia pekee ya kuwagundua ni pale anapochochora (kwenda nje ya mada) au unaposhauri kitu ambacho mleta mada ameshakiainisha kwenye post yake.

3. Wasioangalia Muda wa Post.
Unaweza ukakuta mdau kachangia mada kana kwamba hilo tukio limetokea leo kumbe ni mwaka 2008.

4. Wanaondika ki-Facebook.

Xaxa kama umedhamiria wadau waxichangie kwenye kitu ulichopoxt na badala yake wadili na uandixhi wako wewe andika hivi utaona.

5. Wanaolalamika kujaziwa server.

Inaweza kukushangaza kidogo lakini ni kweli kuna wadau wanalalamika kujaziwa server. Hatujahi kusikia ndugu Melo akilalamika kuhusu udogo wa server ila wapo wanaolalamika. Hapa tunahitaji ufafanuzi..

NB : Kama kuna mtu atahisi nimemjazia "SERVER" yake anisamehe.

Wengine watajeni nyie.....
 
Wapo waliommiss Jakaya pia, wao huponda issue yoyote inayohusu sirikali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…