Kutapeliwa kiwanja

A.Ngindo

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
276
Reaction score
101
Habarini wana JamiiForums,

Miezi mi tatu iliyopita nilinunua kiwanja maeneo ya Bunju kutoka kwa mzee mmoja aliyekua anakata viwanja kutoka kwenye shamba lake kubwa na kuviuza vipande vipande kwa watu,sasa tatizo lililo nikuta mwezi ulipita nilienda ofisi za watu ardhi (survayers)ili wanipe mchakato wa nini kinatakiwa ii niweze kurasimisha kiwanja changu yani kupata hati nikaambatana nao hadi kwenye eneo langu ili kuchukua coordinates ndipo hapo kugundua kua yule mzee aliniuzia kiwanja kwenye shamba ambalo lilikua na hati yayani haikua squatter bali eneo ambalo lilikwisha pimwa na lilikua na hati ya wizara.

Sasa hawa ma savayer walicho niambia ni ili niweze kufanikisha zoezi la kupima kiwanja changu inatakiwa ni mtafute yule mzee aniandikie barua ya kusurrender ile hati yake ya mwanzo pamoja na copy zetu za makaratasi ya mauziano zikiambatana na copy ya hati ya huyo mzee.

Sasa nimejaribu kumtafuta muuzaji zaidi ya mara tano kumuelezea kua nahitaji hizo document lakini naona hanipi majibu ya kuelewka kila nikimtafuta ananiambia mara wiki ijayo mara mwezi mpaka hivi sasa amekua hapokei simu zangu kabisa naombeni msaada wa nini naweza kufanya ili kupata hizo document na hatimaye niweze kupima kiwanja changu maana naona nimetapeliwa
 
Hao wanaosababisha migogoro ya ardhi serikali inawatafuta sana ili ishughulikenao. Nenda ktk ofisi za serikali za mitaa au ofisi za kijiji theni omba barua ya kwenda kumfungulia mashitaka ya kukutapeli na kusababisha migogoro ya ardhi kwa makusudi, ukishapewa RB mtafute muonyeshe kisha mwambie kesi yake ni kesi kati yake na jamuhuri akimalizana nao ndio kesi yako itazungumzwa. Atalegea mwenyewe aidha arudishe pesa au akupe ushirikiano.
 
Kama nimekuelewa nikwamba umetapeliwa huna chako we mtafute huyo mzee akurudishie hela yako,next time kabla hujanunua onana na watu wa ardhi kwanza
 
Wewe unataka mahala ya kujenga na kuishi ama unatafuta HATI. Kwa Daaaslam hiyo hali ipo sana, kikubwa waulize Hati inayomiliki eneo ina jina gani? Je, ndilo jina la aliyekuuzia?? Kama ndiyo agiza Suppu ya Kuku na chappati ujipoze. Kama siye hapo ndipo pana shaka.
 
Mkuu sio kama ninakusema vibaya ila mmezidi sana, yaani huwa mnaona mkitoa hizo laki mbili au tano kumpatia wakili huwa mnaona kuwa mtafilisisika na ukute upo hapo Dar miaka na miaka na una elimu ya chuo kikuu.

Humu JF ulipokuja kuomba ushauri huu kuna nyuzi nyingi sana za tahadhali za kuchukua unaponunua viwanja lakini nadhani na wewe ulikua kwenye ule mkumbo wa 'mwenye hela hashauriwi'.

Acheni uzembe na matumizi ya hela zenu pale mnapojua kuwa likiharibika litakuumiza, ona sasa laki tano ambayo ungempa wakili inakuingiza kwenye maumivu ya mamilioni na hapo ukute ndio mmeingia ile mikataba ya kwa mwenyekiti wa mtaaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ mbona patamu hapooo.

NINI UFANYE?
Nenda polisi ukapeleke malalamiko ya wizi wa kuaminiwa yaani umetapeliwa unataka kurudishiwa hela zako. Na siku nyingine ukitaka kununua hayo maeneo ya namna hiyo hakikisha unawapata mashahidi wa pande zote zinazopakana na hilo eneo unalotaka kununua itakusaidia kuepusha migogoro ya kimipaka na kiumiliki, pia fanya uchunguzi kujua umiliki halali wa eneo husika
 
Usikute ni wewe tumwenye mchecheto wenzako wote wametulia...wamejiwekea kimsingi chao wanajivuta waje kupandisha kozi bila wasiwasi. sawa ilikua plot yake kwa ujumla si ndo maana kaona avikate vidogo vidogo ili awauzie pengine kwa less than 6m to 10m..angalia jina la hati liwe lake tu hapo wizarani..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…