Fabian Evarist
New Member
- May 29, 2023
- 1
- 3
Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoendelea ambayo imekuwa na changamoto za migogoro ya ardhi kutokana mwingiliano na ongezeko la idadi ya watu hivyo ardhi kugeuka dhahabu. Pamoja na thamani na umuhimu wa ardhi, bado kuna haja ya kuweka mambo vizuri hususani katika kipindi cha sayansi na teknolojia katika karne yenye utandawazi ambao umeifunya dunia kuwa kama kijiji.
Maeneo mengi hasa ya makazi, viwanja na nyumba bado haviko katika mpangilio mzuri hususani katika utambuzi wake hapa namaanisha majina ya wamiliki, namba za viwanj na majengo nk. Vipo vyanzo vingi vya migogoro ya ardhi kama ununuzi usio sawa wa ardhi, viwanja au makazi; watu kutofahamu haki zao na wajibu wao juu ya masuala ya ardhi, kupanuka kwa mji, ukiukaji wa sheria za ardhi miongoni mwa watendaji na uhaba wa rasimali ardhi.
Sababu nyingine zinazopelekea migogoro ya ardhi nchini Tanazania ni masuala ya kisiasa, ubaguzi katika matumizi ya rasilimali ardhi, rushwa na mipango/ mifumo isiyo na tija katika usimamizi wa ardhi. Mambo haya yote yanapelekea migogoro mingi ya ardhi kutokea kutokana na kutofuata sheria wakati wa manunuzi ya viwanja, ardhi na nyumba. Manunuzi mengi ya ardhi, nyumba na viwanja hayazingatii sheria ndio maana ni rahisi kukuta kiwanja kimoja au nyumba moja inamilikiwa na watu wawili au zaidi.
Pamoja na serikali kuanzisha sheria ya Ardhi ya mwaka 1999 na hatua zingine kwa ajili ya kukabiliana na migogoro ya ardhi katika ngazi mbalimbali kuna haja ya kuanzisha mfumo ulio huru, unaofanya kazi kwa haraka na kwa haki kwa ajili ya kupunguza migogoro ya ardhi hasa kuanzia kwenye ununuzi na umiliki wa ardhi. Wengi mtakubaliana na mimi kuwa migogoro ya aina yoyote ile ni kitu kibaya sana hasa kutokana na madhara yake. Kwa mantiki hiyo basi kuna hoja ya kila mmoja wetu kuendelea kutafuta suluhu ya kudumu kwa kubuni njia/ mbinu mbalimbali ili zitusaidie kuepuka na kudhibiti utokeaji wa migogoro ya ardhi nchini.
Kutokana na changamoto hii, wajanja wengi wa mjini huitumia ili kujipatia viwanja, majengo na ardhi kwa njia zisizo halali na wakati mwingine watendaji wa serikali ambao sio waaminifu hushiriki katika vitendo hivi. Wengine huuza viwanja, nyumba au ardhi kwa mtu zaidi ya mmoja. Hii yote ni kwa sababu hakuna mpangilio mzuri wa ardhi katika utambuzi, uratibu na usimamizi wake.
Mwaka 2022, serikali ilianzisha na kuendesha zoezi la mfumo wa anuani za makazi kwa lengo la kuyatambua maeneo kwa kuzingatia mitaa, barabara, njia na majengo. Pamoja na utambulisho huo kimsingi umefungua njia yakujua namba ya nyumba, mmiliki, nk. Itakumbukwa kwamba zoezi la mfumo wa anuani za makazi ni sehemu ya utekelezaji wa sera ya Taifa ya posta ya mwaka 2003 (Sera hii imejikita katika kuchangia utekelezaji wa dira ya Taifa ya maendeleo ya mwaka 2025) ambayo inaelekeza kuwa na mfumo mpya wa anuani kwa kutumia mitaa, vijiji au barabara na namba za nyumba na posta kodi.
Kwa kuwa zoezi la anuani na makazi limefanyika kuna haja ya serikali kupitia wizara husika kuanzisha appliction maalumu ya simu ijulikanyo kama LAND APPLICATION ili taarifa mbalimbali zinazohusu ardhi, makazi na nyumba zipatikane kwa wananchi wengi kadiri inavyowezekana ili kuepusha migogoro ya ardhi nchini. Taarifa zote zinazohusu umiliki wa ardhi – nyumba na viwanja ziwe mpya, zilizobadilishwa au kusahihishwa zisambazwe kwa watumiaji ambao ni wananchi kupitia mfumo huu wa Application kadiri itakavyoonekana inafaa. Application hii ambayo ni mfumo ulio huru utafanya kazi kwa haraka sana kwa haki kwa mnunuzi wa ardhi, kiwanja au nyumba kupata taarifa sahihi kabla hajafanya maamuzi ya manunuzi. Appilication hii itasaidia serikali na wamiliki wa ardhi kubadilishana taarifa za ardhi, makazi, viwanja na mashabmba wanayomiliki ili kupunguza vitendo vya utapeli.
Maeneo yote yaliyopimwa na serikali yatasajiliwa pamoja na majina ya wamiliki, anuani ya mmiliki, namba ya kiwanja cha muuzaji au mmiliki kwa wakati huo, namba za simu picha ya mmiliki na majirani wote wanaopakana nao. Hii ni muhimu kwa nchi zilizoendelea ambapo kumekuwa na migogoro mingi ya ardhi ikihusu ardhi - mashamba, viwanja na majengo na watu wamekuwa wakiuana kutokana na baadhi ya watu na madalali kuuza kwa njia za udanganyifu au kuuza mara mbili eneo moja kwa wateja zaidi ya mmoja.
Application hii itamsaidia mnunuzi kabla ya kununua au kutumia eneo la ardhi au jengo alilonunua ataweza kufuatilia taarifa za eneo husika ili kupata taarifa halisi za muuzaji ikiwa zinaendelea na zile zilizopo katika Application hii ambayo itatumika kama database.
Hii inataka kufanana kidogo na Google Map isipokuwa yenyewe inakuwa na taarifa za namba ya kiwanja, mahali, anuani, mipaka yake, majirani wanaomzunguka na taarifa binafsi za mmiliki.Taarifa za ardhi, makazi na viwanja pamoja na mashamba zitakuwa zinazohusishwa mara kwa mara ikiwa umiliki utabadilika baada ya mtu kuuza au kununua.
Katika muktadha huu, maeneo yote ya makazi na yale yasiyo ya makazi ambayo hayakusajiliwa katika zoezi la anuani za makazi na sensa ya watu mwaka 2022 yataingizwa kwenye database hii na mtu yeyote ataweza kupakua application kwa ajili ya matumizi yake mwenyewe.

Upvote
6