Kuteguka kwa bega na kukaza kwa misuli

Kuteguka kwa bega na kukaza kwa misuli

Mwamba028

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2013
Posts
4,595
Reaction score
3,670
Habari zenu waungwana

Mwenzenu nimekuwa na hili tatizo la kuteguka bega, ni ngumu kidogo kuielezea hii hali ila nitajitahidi kadri ya uwezo

Iko hivi, tatizo hili mara ya kwanza kunitokea nilikua form 3 mwaka 2005 nilikua nafanya mazoez ya kurusha mikono km mtu anaempiga mtu vibao ghafla mkono pale sehemu ya bega ikateguka na bega likahama sehem yake na kurudi kwa nyuma ikiambatana na maumivu makali,kwa sababu niliogopa basi nikashika mkono huo ulioteguka na kuurudisha kwa nguvu na ukarudi kisha nkaskia maumivu makali

Sasa hii hali imekua ikiendelea kunitokea japo sio mara kwa mara ila kwa mwaka inaeza kunitokea mara 2 mpk 3,kuna mara ishakua ikinitokea usiku nikiwa nimelalia ule mkono nkistuka ghafla mkono unateguka na mara nying hutokea pale napokua nafanya baadh ya mazoez,nataman niendelee kuelezea ila naona km nitawachosha na makala

Nahitaji kuliondoa hili tatizo mana inaponitokeaga napataga maumivu makali kupita kiasi na baada ya hapo siku nzima huo mkono unakuwa na maumivu ya mbali
 
hv ina mana hamna ambae ashawahi kuwa na tatizo km hili humu ndani ?!
 
Back
Top Bottom