Neema ya BWANA
Member
- Jun 25, 2023
- 45
- 32
Ulimwengu wa sasa umejaa wanadamu wenye mitaji ya fedha lakini waliokosa mawazo ya UBUNIFU; kwani zinaibuka kampuni, biashara, kazi na huduma nyingine kila siku lakini ni zilezile za kuigana, kukaririshana, kufundishana, ku-'copy' na ku-'paste' kutoka kwenye mitandao, na kadhalika.
Hii ndiyo changamoto inayopelekea ulimwengu kukosa kina Samia Suluhu wapya, kina William Gates wapya, kina Elon Musk wapya, na kadhalika, badala yake yanaibuka makundi mapya ya U-Sodoma na U-Gomora kila kukicha, na ulimwengu unasimama kuwapigia makofi kwa kigezo cha HAKI kumbe ni unafki na roho chafu ya uasi iliojaa ulimwenguni.
Usodoma na Ugomora ni kila aina ya dhambi ya zinaa na ukahaba aitendayo mwanadamu juu ya mwili wake. (1 Wakorintho 6:18)
(Ufunuo wa Yohana 17); Usodoma na Ugomora ndiyo ajenda kuu ya kuzimu katika nyakati hizi za mwisho, hivyo Ukweli ni kwamba USODOMA NA UGOMORA (USHOGA) ni uwanja mpana ambao unahusisha;
Mwanamume anayeshiriki mapenzi ya jinsia moja na mwanamume mwenzie,
Mwanamume na mwanamke aidha walio ndani ya ndoa au nje ya ndoa; wanaoshiriki mapenzi kinyume na maumbile,
Mwanamke anayeshiriki mapenzi ya jinsia moja,
Mwanamke na Mwanamume wanaofanya ngono kabla na nje ya ndoa,
Mwanamume na mwanamke wanaobadili jinsia zao.
Vitendo hivi vyote kwanza ni dhambi na laana MBELE ZA MUNGU lakini pili vinaharibu afya za uzazi, afya za maumbile, afya za roho, afya za mwili na afya za akili; hivyo wanaowapigia makofi watu wa makundi haya wanayo maswali matatu ya kutujibu;
Kwanini wanahalalisha haramu inayoharibu afya za watoto na vijana ulimwenguni kote, kama madawa ya kulevya yanavyofanya?
Wanafahamu Haki ni nini? Sawa ngoja niwaandikie; Haki ni kitu ambacho mtu ni lazima akipate chini ya sheria mara tu baada ya mtu huyo kuzaliwa, na Haki namba moja ya mwanadamu hapa duniani ni Haki ya Kuishi.
Swali ni; je! Kwa nini ulimwengu unapitisha sheria za kuhalalisha vitendo ambavyo kwanza vinaathiri afya lakini pia vinapelekea kumnyang'anya mshiriki wa vitendo hivi Haki yake ya kuishi baada ya afya yake kuathirika?
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Mhe. Dokta Phillip Mpango amewahi kusema kuwa, mapenzi na ndoa za jinsia moja hata wanyama hawana. Kauli hii ni ukweli 100% kwa sababu hata mimi tangu nizaliwe mpaka sasa nina umri wa miaka 28; sijawahi kuona wala kusikia jogoo amemfanyia uasi jogoo mwenzie.
Tafsiri yake ni kuwa; wanaofanya, wanaoshangilia, wanaovihalalisha na wanaovipigia makofi vitendo hivi labda watuthibitishie pia kuwa uwezo wao wa kufikiri, kutenda na kufanya maamuzi uko chini zaidi ya jogoo jambo ambalo si kweli kwani MUNGU Ametuumba wanadamu tukiwa na ufahamu tofauti na wanyama, hivyo kamwe hatutaweza kuwaelewa wala kuwaunga mkono watu hawa.
SULUHISHO
Haki pekee wanayoweza kuipata watu hawa walioathiriwa na vitendo vya Usodoma na Ugomora ni kutouawa, kutohukumiwa, kutotengwa, kutofungwa jela kwa sababu huko ndiko kunaweza kukawa kubaya zaidi kwao watakapokutana na vidume au vijikedume waliofungwa kwa makosa mengine, lakini pia wala wasiaibishwe hadharani; bali watengewe maeneo maalum ya kuwasaidia Ki-Roho na Ki-mwili kama ambavyo watu wa madawa ya kulevya wamejengewa 'sober houses' ili kuwasaidia kwa UPENDO kuacha vitendo hivi, kwani wao ni waathirika hawafahamu chochote.
Lakini kubwa zaidi; tuliopata NEEMA YA MUNGU ya kuvijua na kuvikataa vitendo hivi na vyote vibaya, tunatakiwa pia tusiwahukumu wanaoshabikia na kudai vitendo hivi vifanyike kwa kigezo cha Haki, bali tuwape msaada wa Ki-roho na Ki-mwili mpaka waache vitendo hivi, kwani hatufahamu na wao vimewaathiri kwa kiasi gani.
Usodoma na Ugomora umekuwa chukizo MBELE ZA MUNGU hata kupelekea kuchelewesha BARAKA zetu, lakini pia kuondoa uwajibikaji wa wanadamu hata kushindwa kutimiza MAKUSUDI YA MUNGU waliyoletwa kuyatekeleza hapa duniani, kwani wanaume wamekuwa wanawake, wanawake wamekuwa wanaume, hata kupelekea dunia kuwa kichwa chini miguu juu, baba ndevu mtoto ndevu na mama pia ndevu.
Ili kuteketeza Usodoma na Ugomora mpaka kubaki majivu kabisa yatupasa KWA NEEMA YA MUNGU kufanya yafuatayo:-
Picha ni kutoka Google.

- Kuwasaidia wale ambao tayari wameathiriwa na vitendo hivi; kwa kupambana vita hii kwa siri kubwa pasipo kuwaanika hadharani walioathiriwa wala kuanika hadharani njia, namna, jinsi, hatua, na mpango huu adhimu wa kupambana na vitendo hivi vichafu ili kurejesha NGUVUKAZI, UWAJIBIKAJI, UTU lakini pia MAHUSIANO MAZURI kati yetu na MUNGU Aliyetuumba.
- Kuanzisha somo maalum kwenye ngazi zote za Elimu, linalohusu kupambana na kupinga vitendo hivi vya Usodoma na Ugomora tangu ngazi ya awali yaani utoto wa mwanadamu mpaka ukubwani.
- Kutumia teknolojia kuunda programu maalum za kutusaidia vijana kuwajibika na mambo ya msingi hivyo kusaidia kupunguza wimbi la vijana kutojihusisha na vitendo vya Usodoma na Ugomora.
- Kupambania mpaka kuupata UHURU wa Mataifa ya Afrika na ulimwengu mzima ili lisitokee Taifa lolote duniani litakalolazimisha na kuhamasisha ufanyikaji wa vitendo hivi barani Afrika na duniani kote kwa tishio la kufungiwa misaada au kuwekewa vikwazo.
- Taasisi nyeti na muhimu zaidi duniani iitwayo NDOA NA FAMILIA iheshimiwe na watu wote, kuanzia wanandoa wenyewe kukwepa Usodoma na Ugomora ndani ya ndoa zao kwa kutofanya vitendo vya kinyume na maumbile lakini kila mmoja kuwa mwaminifu kwa mwenza wake ili kulinda HESHIMA YA NDOA, kwani NDOA NA FAMILIA ni taasisi ambayo kwa NEEMA YA MUNGU IKIIMARIKA VYEMA na kila mmoja kuanzia baba, mama na watoto kutimiza wajibu wake ipasavyo na kupelekea utawala ndani ya taasisi hii kuwa BORA; inayo UWEZO MKUBWA wa kutuletea wanadamu safi, wenye UPENDO, wenye maadili mema, wenye UHURU wa kutumikiana kwa UPENDO, wasio na hila wala mawaa, hivyo kupelekea dunia kubadilika kutoka kwenye uasi na upendo uliopoa na kuwa ulimwengu safi, mpya wenye UPENDO WA KWELI. (Waebrania 13:4)
- Chanzo cha uasherati, uzinzi, ukahaba na kila roho chafu ya Usodoma na Ugomora ni Ulevi wa pombe au unywaji pombe ambayo ndiyo kikombe cha mvinyo ya uasherati (Ufunuo wa Yohana 17:4-6) (Ufunuo wa Yohana 18:2-3); hivyo kupambana na Usodoma na Ugomora huku tukiacha unywaji wa pombe na ulevi uendelee kufanyika ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu. Tafsiri yake, tunatakiwa kupambana sana na Ulevi.
- Tuishi kwa NEEMA YA MUNGU na tusiishi kwa sheria (2 Wakorintho 12:9-10)
Picha ni kutoka Google.
Upvote
1