Baada ya kusoma maoni mbalimbali kuhusu swali na Elektron, naomba kuweka swali jingine la challenge kama hilo. Sote tunajua kuwa kutembea kwa viumbe wengi ardhini kunategemea kuwapo kwa msuguano (friction) kati ya kiumbe hicho na ardhi.
Je kuna sababu kwa nini lazima kutembea kufanyike kwenye uso (surface) wenye friction tu? Kwa nini viumbe visitembee kwenye uso wenye utelezi bila matatizo? Je kuna kiumbe chochote kinachoweza kutembea kwenye utelezi bila tatizo lolote? Ni kiumbe gani hicho na kinatembeaje?
Unazungumzia Amoeba hapo ,huyo ndo pekee anaeweza kutembea katika anga hizo wengine ni fungus ambao wao sio kutembea tu wao wanajenga kabisa na kuishi hapo na kuzidisha utelezi .ila sijakufahamu unazungumzia utelezi gani maana hata nimewahi kusikia kuwa jamaa alipanda mlima akateleza mwengine alipanda mkarafuu akateleza mwengine alivuka mto akateleza na kuburuzwa na maji..........kiswahili kikubwa !
Labda ktk kuchangia kidogo nilichonacho, wakti tunafuta ujinga huko skuli tuliambiwa kwamba msuguano baina ya mtembeaji na ardhi sio chanzo cha; mwendo,kubadili uelekeo, au kusimama kutoka ktk hali ya mwendo, bali husaidia tu hayo mambo anuai. Kanuni ya 3 ya Newton ikizingatiwa, nguvu ya msuguano si kisababishi bali nguvu itokanayo na nguvu anzishi/kisababishi.
Hivyo basi si sahihi kusema kuwa bila msuguano hakuna mwendo, kubadili uelekeo au kusimama. Ili mambo haya yatokee inabidi nguvu sababishi na ambukizi ziwe ktk uwiano.
Kukosekana kwa msuguano kutaweza kusababisha mwendo au kusimama kutoka ktk hali ya mwendo kuwa ngumu kutokana na kukosekana kwa msuguano na kusababisha utelezi. Hali hii itasababisha mwendo, kubadili uelekeo au kusimama kutoka ktk hali ya mwendo kuwa shaghalabaghala na hivyo mambo mengi ktk shughuli za kila siku za mwanadamu kuwa shakani.
Was'alam