Kutembea na aliekuwa shemeji yake

stephot

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2012
Posts
17,216
Reaction score
26,225
Walikuwa marafiki sana,jamaa akamtambulisha rafiki yake kwa mpenzi wake wa kike kuwa huyu ndo shem wako,jamaa akaja kuhamishwa kikazi na mwanamke kamuacha palepale na mwasiliano akakata,mshikaji akatia miguu kwa shemeji yake shemji kakubali,penzi likanoga sana mpaka wakazaa mtoto,baada ya miaka 6 jamaa karudi anataka tena penzi akatolewa nje,mshikaji wake hakumwambia kuwa yeye ndio anakula goma ila jamaa kapata tetesi kuwa mshikaji wake ndio anakula goma,jamaa kakasirika kinoma hataki tena kuongea na mshikaji wake,wadau hapo kuna kosa au mwenye makosa nani na je mshkaji aachie ngazi kama kosa ni la kwake kwa kutembea na aliyekuwa shemeji yake?
 

Hapo kwenye bold hapoo, miaka 6 bila mawasiliano alitegemea mchumba amsubiri tu!! Wasiumize vichwa sababu yake.
 
alikata mawasiliano sasa antaka nini? huyu rafikiye sio ndugu yake. yeye ndio anatamaa miaka sita na technolojia ya miaka hii hakuweza kuwasiliana hata kumjulia khali.

Ndio sio vizuri kula vya rafikio, ila yeye lazima aliongea maneno ya kumfanya rafikie amuone binti yupo free.

akalale mbele atafute binti mwingine, asiharibu maisha ya walio wote sasa.

ndio nionavyo mie
 
Sioni tatizo zaidi ya wivu!

Bazazi!
 

umeuliza swali au umenena
 
Mwanamke anawakosanisha wanaume wazima na akili zenu?What a shame!
 
Mwanamke siku zote nikifaa....uongo Eiyer??
 
Last edited by a moderator:
Mkosa aliyekata mawasiliano. Nyumba inayohamwa huhamiwa na mara nyingi yule anaeijuwa ilivyo ndani atakuwa muhamiaji mkubwa!
 
Nae amtambulishe sasa kwamba huyu ndo shemeji yako.
 
Take it from me kaka, dunia isingekuwa na wanawake, amani ingeongezeka kwa 80%, na lifespan ingekuwa ile ya kina yakobo, miaka 400! Tatizo ecosystem isinge-balance.
Mwanamke anawakosanisha wanaume wazima na akili zenu?What a shame!
 
Duuh sasa yeye alifikiri muda wote atamsubiri yeye isitoshe huyo rafiki yake hana makosa hakuwa mke bali ni GF ambaye walishatengana. Hana lolote huyo anataka kuwaletea kiwingu tu inabidi wampotezee
 
Sioni tatizo zaidi ya wivu!

Bazazi!

Bazazi umenena kaka! Yeye aliona cha nini kumbe rafikiye alikuwa anapiga mahesabu atakipata lini...hhahahaha. Hao wawili hawana makosa,maadam hakuwah kumuoa then ruksa. Inamuuma tu kuona mwanamke kanawiri tofaut na alivyokuwa nae.
 
Mambo haya kusema kweli yanatokea sana..........'shemeji kula kaka/rafiki kasafiri.....'
 
yaani akate mawasiliamo...
Halafu arudi baada ya miaka sita, atake penzi?

Mwambie huyo 'jamaa' akapime akili....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…