- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Kumekuwepo na taarifa ikieleza kuwa Katibu mwenezi wa BAWACHA taifa aliyetekwa huko kibiti kkuwa sababu ya kuofanyiwa hivyo ni kutokana na kutembea na wanaume wa watu, Je ni kweli?
- Tunachokijua
- Aisha Machano ni katibu mwenezi wa Baraza la wanawake CHADEMA (BAWACHA) Taifa kwa mujibu wa kurasa za mitandao ya kijamii ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) tarehe 20-10-2024 walieleza kuwa Katibu Mwenezi Bawacha Taifa Mhe. Aisha Machano akiwa Kibiti kuendelea na majumu ya Chama ametekwa na kupigwa sana kisha kutupwa porini na kwamba Vijana wa bodaboda wamemuokota akiwa katika Hali mbaya na maumivu makali.
Katibu machano baada ya kutuhusiwa kutoka katika hospitali ya Mwananyamala amefanya mkutano na waandishi wa habari tarehe 20-10-2024 ambapo alielezea tukio la kutekwa kwake alisema alikamatwa na watu waliokuwa na gari alilolitambua kuwa ni la polisi.
Kumekuwepo na grafiki mitandaoni inayoeleza kuwa chanzo cha Katibu Aisha kutekwa ni kutembea na wanaume za watu huku ikionesha kuwa imetengenezwa na The Chanzo, grafiki hizo zipo hapa na hapa.
Ukweli upoje.
JamiiCheck imefanya ufuatiliaji wa kimtandao na kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (key words search) na kubaini kuwa madai hayo hayana ukweli na pia grafiki hiyo haijatolewa na The Chanzo.
Kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (key words) ‘ukweli wafichuka tabia za Aisha Manongi’ kama inavyoonekana katika grafiki hiyo inayosamambaa hakuna uthibitisho wa kuwepo kwa taarifa hiyo kutoka katika vyanzo vya kuaminika.
Baada ya kupitia katika kurasa za mitandao ya kijamii ya The Chanzo, tumebaini kuwa hakuna taarifa ya hivyo huku taarifa zao za mwisho walizochapisha mathalani katika mtandao wa X kuhusiana na suala la Aisha ilikuwa ni kuhusu matangazo ya moja kwa moja ya waandishi wa habari na katibu huyo kupitia katika chanel yao ya Youtube na nyingine grafiki ilikuwa ikisomeka kuwa ‘watekaji wa kiongozi wa wanawake CHADEMA walijitambulisha wao ni polisi’
JamiiCheck imefuatilia mahojiano aliyoyafanya katibu Aisha na waandishi wa habari ambaye alielezea kilichotokea baada ya kutekwa ikiwemo kupigwa. JamiiCheck pia imefuatilia taarifa ya Jeshi la polisi waliyoitoa kwa umma na kueleza kuwa wanaendelea na uchunguzi na watatoa majibu sahihi ya nini kilichotokea, sababu ya tukio hilo pamoja na wahusika.