Kuna wakati, niliwahi kufanya kazi kwenye kampuni ya Barrick, nikiwa senior officer.
Tukataarifiwa kuwa plant imesimama, kuna kikao cha dharula. Kusimama plant kwa mgodi mkubwa siyo jambo dogo. Ndani ya saa moja, Head Office, Toronto ilikuwa tayari imejulishwa.
Kwenye kikao tukajulishwa kuwa sababu ya kusimama plant ni mgomo wa wafanyakazi wote Watanzania, kugoma kufanya kazi kwa madai kuwa kuna Kaburu katoa kauli ya ubaguzi.
Ilikuwa hivi:
Supervisor, ambaye ni mzungu aliona mfanyakazi Mtanzania amefanya kazi vibaya. Yule supervisor akasema, "that is why I do not trust you black people". Waliokuwa karibu na kuisikia kauli ile waliwajulisha Watanzania wengine, na wote wakaweka tools down. Plant ikasimama.
Taarifa ilipofika toronto, swali lilikuwa, "that has happenned, what do they want?" Meneja wa mgodi akawaambia, "they want him fired". Naye akawauliza, "then what is the problem? Do what they want, it is their country"
Hoja ni nini? Wafanyakazi wa kiTanzania kukosea, kusemwa, kuonywa na hata kukaripiwa na Watanzania wenzao haikuwa kitu cha ajabu, na hakuna wakati wafanyakazi walipogoma kwa sababu mfanyakazi mwenzao Mtanzania alikuwa amefokewa na Mtanzania mwenzao.
Kudhalilishwa na mgeni inaumiza sana, maana huleta tafsiri ya ninyi nyote mmedharauliwa. Kudharauliwa na mgeni kunaleta mshikamano na umoja, kama haukuwepo.
Marehemu Magufuli alikuwa anafokea sana. Wengi walivumilia maana ni kudhalilishwa na mwenzenu. Ingekuwaje kama kudhalilishwa kule kungekuwa kunafanywa na asiye Mtanzania au asiye Mtanganyika, kwa lugha ya Mtikila?
Ubaguzi wa kikanda au kikabila, ni mbaya sawa kama ubaguzi wa kidini au kieneo. Lakini unakuwa mbaya zaidi kama unafanywa na mgeni dhidi ya mwenyeji. Wazanzibari kuteuliwa kufanya kazi kwenye nafasi zisizo za muungano sawa, lakini mtanganyika kuteuliwa Zanzibar, hapana. Mzanzibari kupata ardhi bara sawa, Mtanganyika hata kumiliki square foot moja Zanzibar, hapana. Mzanzibari kuteua majaji Tanganyika sawa, lakini Mtanganyika kuteua hata sheha Zanzibar hapana. List ni ndefu, siwezi kumaliza.
IPO HIVI
Mtawala akitoka kwenye jamii ndogo tena ya ugenini, atakuwa muoga dhidi jamii kubwa ya wenyeji. Lakini anaweza kupata nguvu kubwa ya ajabu ya kutenda chochote anachotaka dhidi ya jamii kubwa, kama akiweza kuwagawa au akawakuta wamegawanyika maana atawapeleka kwenye mapambano wakapambane wenyewe kwa wenyewe, yeye akiwa raha mstarehe.
Yaliyotokea wakati wa Magufuli yalikwishatokea, tunatakiwa tutazame mbele kama Watanzania na kama Watanganyika, ili nguvu yetu ya pamoja iogopwe na ijitetee katika kuyalinda maslahi yetu.
Mambo sijui ya Sukuma gang, mara Kanda Pendwa au Chagadema na wachaga, hayataiacha Tanganyika salama wala Tanzania salama. Tukiyaendeleza haya niliyoyasema, anaweza kuja mtawala hata kutoka Comoro akatutawala kwa namna yoyote aipendayo, bila hofu kwa sababu atatumia mgawanyiko wetu.
Ni mchanganyiko wa hoja wenye dhamira moja. Wenye akili watanielewa maana lugha iliyotumika ni rahisi na mazingira yaliyotumika ni tunayoyaishi.