SoC02 Kutengana kwa wazazi, malezi ya mzazi mmoja na afya ya akili

SoC02 Kutengana kwa wazazi, malezi ya mzazi mmoja na afya ya akili

Stories of Change - 2022 Competition

Gideon kimaryo

New Member
Joined
Sep 3, 2022
Posts
2
Reaction score
3
Katika jamii zetu za kitanzania kwa sasa utakuwa shahidi wewe mwenyewe kuona kwa jinsi gani ongezeko la watoto wanaolelewa na mzazi mmoja, sababu za zinawezakuwa ni KIFO cha mzazi mmoja au KUTENGENGA.
Masuala ya kifo tumuachie mungu ila kwenye hili swala moja la kutengana kwa wazazi ndo huwa chanzo kikubwa na hii inaweza kusababishwa na;

[emoji3503]UGUMU WA MAISHA.
[emoji3503]TAMAA ,USALITI ,NA KUSHINDWA KURIDHIKA NA HALI TULIZONAZO.
[emoji3503]KUTOKUJIELEWA AU KUSHINDWA KUTAMBUA NAFASI YAKO WEWE KAMA MZAZI.
[emoji3503]KUSHINDWA KUVUMILIA CHANGAMOTO ZA NDOA.
[emoji3503]NDOA ZA UMRI MDOGO ,KUINGIA KWENYE NDOA AU MAHUSIANO BILA KUJIPANGA.
[emoji3503]UZINZI NA ULEVI.

Mambo haya huweza kupelekea wanafamilia wawili kutengeneza aidha kwa uzuri au kwa ubaya na uadui mkubwa[emoji35], hivyo basi kuna uwezekano ikawa ni kesi mahakamani ili kujua hatima ya watoto au kutokana kutokujua sheria kesi huishia kwa mama mkwe bila hatima isioeleweka. Na mara nyingi zaidi wakina mama ndo huwa wanaachwa , hivyo jukumu la kubaki na mtoto hubaki kwake.

Sasa kuna makundi mawili apa, la kwanza ni lile la mama kubaki na mtoto alafu baba awe anamuhudumia mtoto au mwingine asilete kabisa na kupotelea mbali na pia kundi la pili ni wale ambao hata baba wa mtoto hajulikani au kutokana na baba kutokawa na uwezo ,mtoto au watoto kuhamishiwa kwa mama mzazi wa baba au wa mama, na kazi huwa ngumu zaidi kwa wale watoto wenye ULEMAVU/MATATIZO wakuzaliwa kama vile kichwa kujaa maji, ulemavu wa ngozi,bubu au kiziwi n.k.

Hivyo basi watoto kwenda kulelewa kwa bibi ,kama bibi bado ananguvu kwa kiasi chase huwa anaweza kujitahidi basi kama vile wewe alivyo kutunza basi na mjukuu wake basi atamsaidia hivyo hivyo lakini kama bibi kidogo atakuwa amechoka kutokana na umri kwenda sana basi malezi kidogo huwa utegemea na tabia za mjukuu mwenyewe kama mjukuu kulingana na malezi mabovu ya mama na baba waliokuwa hawaelekewi basi huwa na changamoto kubwa sana kwa bibi anaelea mtoto huyo.

Hatuwezi kuukwepa ukweli kwamba malezi ya mtoto yanahitajika kutoka kwa baba na mama, mzigo unaporushwa kwa bibi na babu huwa changamoto sana na mara nyingi hii ni kwa sisi vijana wadogo tulioyakimbilia majukumu lakini sasa yamekuwa mazito tunayaacha tena kwa watu wengine.

Kwa upande wa upande wa wakina mama ambao wanaishi na watoto/mtoto pekee yao, changamoto kubwa zaidi ndo huwa iko hapa kwa kuwa mama ndo azibe nafasi ya baba kutafutia watoto chakula ,kuwalea watoto kama mama na masuala ya kimaadili dhidi ya watoto wake kwaiyo, kubalansi mda wakutafuta ela na mda wamalezi huwa ni ngumu sana kuwa mlinzi wa afya ya mtoto ,kumfundisha,kukaa nae na kumlea kama watoto wanavyo elewa kawaida.

Na haishii apo wakati mwingine mwendelezo wake huwa ni kwa wakina mama kuona kama hamna faida au haja ya kuwa na baba katika familia na ndio maana KUSAGANA kumezidi kuonekana sana. na hapo ndipo tunaposema kutokana na malezi watu wamekuwa wakipata changamoto za afya ya akili ,kwa sababu wanawake wengine huona kama kila mwanaume ni shetani kutokana na alivyotelekezewa watoto na kiukweli watoto wanatelekezwa sana[emoji174].

Au baada ya kifo cha baba aliekuwa na mke zaidi ya mmoja ,hali ya watoto wanabaki kuanzia mke mkubwa mpaka mdogo huwa sio nzuri kama baba hakuwa na uchumi mzuri.

Changamoto ya afya ya akili inaweza ikawa ya moja kwa moja(kuwa kichaa kabisa) au isio ya moja kwa moja. Kutokana ukosefu wa chakula(utapiamlo) na mahitaji ya nyumbani(mafuta ya kujipaka, sabuni na hata maji ya kuoga,kunyoa au kuchana nywele) au ya shuleni kama vile madaftari ,sare za shule maana yake ni kwamba uyu mtoto hata soma vizuri na hata kuelewa au kurudia yale anayofundishwa darasani na hivyo basi huweza kupelekea mtoto kujichukulia mwenyewe kutojithamini na saikolojia ya kuwa wachini,kujishindwa kujiamini katika masuala ya kitaaluma, kuwa na uwezo mdogo wa kujielezea na pia kuwa na matokeo mabaya, utoro kutokana na kusekana wa kumsimamia na wakati mwingine hushindwa kuendelea na masomo kabisa kutoka na changamoto hizo kwa kuwa wengine huwa na changamoto zaidi kama vile ubakaji na ulawiti.

Na kwa wale wanao bahatika kuendelea na masomo hii kazi huwa wanapewa walimu kudili na wanafunzi ,wengine ambao huwa wameshindika na mzazi au mlezi wao kama vile bibi au babu au baba au mama ,hapa shughuli huwa kubwa mno hua wanaipata walimu wetu hasa wa shule za msingi na sekondari za kata.

kisheria mume na mke kama mkilalimika kuachana kutoka na sababu zenu,tutawatambua kwa kuwepo kwa talaka(sheria ya Ndoa 1971,sura ya 29,toleo la 2002)ambazo zimepitishwa na bazara husika baada ya baraza la usuluwishi kushindwa,LAKINI ndo nyingi kwa [emoji1241] Tanzania huwa ni zile za kiolelaolela , msichana alikwenda kwa mume baada ya kupata MIMBA ndo ikaitwa ndoa bila utaratibu wa msikiti,kanisa au mahakama au bahada ya tu zoezi la kutoa mimba kushindikana. Hii yote utokana na ukosefu wa elimu ambao unachangia sana watu kutokujua haki zao.

"mzigo wa matatizo ya akili miongoni mwa vijana barubaru unasababisha mambo makubwa matatu ambayo ni msongo wa mawazo , kujiua ikiwa ni sababu inayoshika nafasi ya pili kwa vifo vya vijana kati ya umri wa mika 15-19 na tatizo linaloongoza ni matumizi mabaya ya pombe na mihadarati , na kufanya matatizo ya akili kuwa moja ya changamoto kubwa kwa nchi nyingi duniani na huchangia kuwaweka vijana kwenye hatari kama ya kufanya ngono isiyo salama, na hata uendeshaji mbovu wa magari unaosababisha vifo vya vijana wengi" WHO oktoba 2018.

Hivyo basi ilikuepukana matatizo haya ni jukumu la mamlaka za serikali zenye dhamana hiyo kuongeza bidii katika ufualiaji wa kesi zote zinazowafikia na kutoa elimu kwa jamii iliwaweze kujua sheria zao na utaratibu uwekwe wazi na HATUA KALI kuchukuliwa dhidi ya wanaokiuka.

Na kwa upande wa jamii ni jukumu letu kubadilika hasa sisi vijana wakiume kuachana na tabia za uzinzi ' eat and run' ambazo baadae upelekea kukimbia majukumu hayo kama vile KUTELEKEZA WATOTO na kama hauna uwezo wa kuhudumia mke zaidi ya mmoja acha haina haja yakuongeza mke kwa sababu ya tamaa zako
Na kwa upande wa vijana wakike hawa kwanza wapewe elimu ya jinsi iliwaweze kujitambua wao ni wakina nani na wana nafasi gani katika jamii kama mabinti wa kitanzania?,na pia mambo mengine kama kueleweshwa vizuri kuhusu mizunguko yao , KUONYANA wao kwa wao kwa sababu mda mwingine dada mtu yuko na mtoto kwao kwa mama yake idadi na bajeti inazidi kuongezeka na kuna uwezekamo mimba aliipatia akiwa shule na kosa hilo hilo! analirudia tena mdogo mtu wa kike na foleni inazidi kuongezeka nyumbani na mwishoe ndugu hawa huondoka na kuwacha wujuku ili kuendelea kupambana na maisha[emoji24][emoji24].

Inatia huzuni sana unakuta mama anaeishi na mtoto wake,wote wawili wanapata mimba na bado wenye mimba hawaelekewi yanajirudia yale yale tena na kuishi kutegemea misaada ya ndugu[emoji24][emoji24] ,wakina dada na kina mama na jamii nzima tujitambue inasikitisha sana na nini tunawafundisha watoto kwa kuwa ukuaji wao hutegemea sana au huiga yale yanafanyika ndani ya jamii.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom