Wataalamu,nilikuwa nauliza inawezekana
kutengeneza mfumo kwa kutumia WordPress kwa ajili ya kuplace order!
Unahizi functionalities!
• Wafanyakazi wa ofisi wanaweza kuweka maombi(order placing) ya vitu vinavyotakiwa kununuliwa mtandaoni.
• Mtu wa manunuzi (procurement) anaweza kuona maombi hayo, kuyakubali, na kushughulikia ununuzi.
Inawezekana kwasababu unaweza kufanya chochote na WordPress ila shida ni kwamba kama mfumo utakua ni mkubwa zaidi hasara zitakuwepo ila ni nzuri kwenye kuanzia kama unataka uwe sokoni haraka huku ukiwa unaendelea kutengeneza mfumo kamili, baadhi ya changamoto ambazo unaweza kukumbana nazo ni hizi hapa...
Swala la usalama litakua ni dogo sana kwenye mfumo wako kwa maana WordPress ni mojawapo ya majukwaa maarufu, na hii inawafanya wadukuzi kulenga tovuti zake, kwahiyo bila usimamizi mzuri wa usalama, data ya orders inaweza kuvuja au tovuti inaweza kudukuliwa. Plugins zisizoaminika pia zinaweza kuwa na udhaifu wa kiusalama (unaweza ukaingia ukakuta website iko down pasipo na sababu ya msingi)
Pia ingawa WordPress inaruhusu customization, ila ni kama haitoi uhuru sawa na utengenezaji wa mfumo kwa namna ile wewe unataka kwa maana ya custom-built system kwahiyo kama unataka mfumo wa kipekee, itakuwa ngumu na inaweza kuwa ghali kuutekeleza kupitia WordPress kwasababu utahitaji utafute plugins zenye mfanano na ule upekee unaouhitaji na mostly hautaweza kuzipata ila utaambulia zile zenye kufanya kazi ya kile unachokitaka.
Lakini pia WordPress haitoi scalability nzuri kwa mifumo mikubwa yenye idadi kubwa ya maombi (orders) au watumiaji, kwahiyo katika huo mfumo tajwa hapo juu nadhani unaweza kupitia hii changamoto kwa maana Kadri maombi yatakavyoongezeka, utendaji wa mfumo unaweza kudorora, hasa bila miundombinu ya nguvu kama servers za juu (ambazo hizi nazo ni gharama).
Ila pia plugins nyingi za premium zina gharama za mara kwa mara (mwezi au mwaka) kwahiyo hii nayo itapelekea mfumo wako uendeshwe kwa gharama kubwa zaidi kuliko ilivyotarajiwa mwanzoni hasa pale utakapohitaji kufanya updates ya features kadha wa kadha.
Pia changamoto ya kasi ya huo mfumo wako itajitokeza hasa pale utakapotumia plugins nyingi na hii inaweza kusababisha uzoefu mbaya wa mtumiaji (user experience), hasa kwa watu wanaotumia mtandao wa kasi ya chini.
Lastly, ni kwamba WordPress ni jukwaa la jumla (general-purpose) na si maalum kwa mifumo ya kibiashara kama kama huo unaoutaka wewe, kwahiyo utakua mnyonge sokoni kwa maana inahitaji marekebisho zaidi ili iweze kushindana na mifumo ya kitaalamu iliyoundwa mahsusi kwa order placing, kama ERP systems na kadhalika.
So kama unataka uwe kwenye biashara haraka Anza na WordPress ila kama unataka utengeneze mfumo wa kudumu sikushauri mkuu.