Kuteuliwa na mamlaka za nchi ni heshima kubwa, anayekataa basi kuna maovu anataka kuficha kwenye nafasi aliyo nayo

Robert S Gulenga

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2013
Posts
2,255
Reaction score
1,565
Kama umeteuliwa ni kwamba umekidhi vigezo kwa maana una sifa stahiki lakini pia umepewa heshima kubwa na Mamlaka iliyokuteua.

Jiulize kuna Watanzania wangapi wenye sifa zaidi yako lakini hawakupewa nafasi hiyo?

Vyombo vya habari vimetoa taarifa kuna Watu wamekataa Heshima waliyopewa na Mamlaka ya Uteuzi.
Itoshe kusema watu hawa kama ni kweli wapo hawana chembe ya uzalendo hata kidogo, umetumwa ukawatumikie Watanzania ukiwakilisha Mamlaka ya Uteuzi unakataa na bado unataka uendelee kwenye nafasi yako ya sasa?

Kuna mambo yanatakiwa kutiliwa shaka kwa watu hawa ikiwa ni pamoja na

1. Yawezekana nafasi walizopo sasa kuna maovu mengi wamefanya hivyo wanaogopa kuachia ghafla mengi yataibuka.

2. Yawezekana kile wanacholipwa ni kikubwa sanaa kuliko wanavyostahili, Wote tunajua Waajiri wao ni Wanachama. Je Wanacholipwa kama Mshara na Stahiki nyingine zinalingana na Waajiri wao?

3. Waajiri wa hawa watu (Wanachama) Je, ni kweli wanawapima utendaji wao kwa Maana ya Investment zinazofanyika chini ya Chama Chenu? Tutakuwa na Michango isiyokoomaa au tutafute uwezekezaji wenye tija na tupunguze michango?

Mwenyezi Mungu ibariki Tanzania

Mwenyezi Mungu mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

20230131_111444.jpg
 
Kuteuliwa bila hata kujulishwa, uteuzi unausikia kwenye vyombo vya habari kama inavyofanya Ikulu ya Tanzania, ni dharau kubwa.

Yani unaonekana wewe ni kinyama tu, huna mipango zaidi ya utakayopangiwa na serikali.

Yani mtu anakuteua unasikia redioni. Kama unatoka nje ya nchi kwa miaka kadhaa siku hiyo hiyo je?

Yani mtu anakuteua hata mipango yako haijui. Huyo ni mjinga, na wewe kama una mipango tofauti, ukikubali eti uwe mzalendo tu, utakuwa mjinga pia.

Si kila mtu anataka kufanya kazi serikalini.

Kama mimi sikubaliani na serikali hii na sera zake, kwa nini nilazimike kukubali uteuzi wake?

Acheni hiyo groupthink ya kusema ukiikataa kazi ya serikali ndiyo umekosa uzalendo.

Nyerere alikataa serikali ya ukoloni na kazi yake, kwa sababu ya uzalendo kwa nchi yake.

Watanzania wengi hawana uwezo wa kutofautisha serikali na nchi.

Wanafikiri serikali ndiyo nchi.
 
Umefika wakati wa serikali ya CCM kufundishwa in hard way. Unateua kwa kukurupuka bila kumshauri mtu huo sio uteuzi bali ubabe. Kwani wanashindwa nini kumtaarifj mtu kuwa unahitajika kupewa nafasi fulani uko tayari?

Kuna siku haya ya kulazimishana unateuliwa kuwa mnyongaji pale Isanga na ukikataa eti watasema sio mzalendo
 
Kuteuliwa bila hata kujulishwa, uteuzi unausikia kwenye vyombo vya habari kama inavyofanya Ikulu ya Tanzania, ni dharau kubwa.

Yani unaonekana wewe ni kinyama tu, huna mipango zaidi ya utakayopangiwa na serikali.

Yani mtu anakuteua unasikia redioni. Kama unatoka nje ya nchi kwa miaka kadhaa siku hiyo hiyo je?

Yani mtu anakuteua hata mipango yako haijui. Huyo ni mjinga, na wewe kama una mipango tofauti, ukikubali eti uwe mzalendo tu, utakuwa mjinga pia.

Si kila mtu anataka kufanya kazi serikalini.

Kama mimi sikubaliani na serikali hii na sera zake, kwa nini nilazimike kukubali uteuzi wake?

Acheni hiyo groupthink ya kusema ukiikataa kazi ya serikali ndiyo umekosa uzalendo.

Nyerere alikataa serikali ya ukoloni na kazi yake, kwa sababu ya uzalendo kwa nchi yake.

Watanzania wengi hawana uwezo wa kutofautisha serikali na nchi.

Wanafikiri serikali ndiyo nchi.
Mtumishi wa umma/Mwalimu

Unapata wapi jeuri ya kukataa uteuzi wa Mwajiri mkuu wa watumishi?

Wangekuwa Sekta binafsi ahueni
 
Kazi ya U-DC ni ya kitumwa sana, haina work plan wala budget! Wewe ni kusubiri amri toka juu na kuzurula kama muhudumu wa ofisi!

U-DC unawafaa machawa vinginevyo utaishia kudhalilishwa!
 
Mtumishi wa umma/Mwalimu
Unapata wapi jeuri ya kukataa uteuzi wa Mwajiri mkuu wa watumishi?

Wangekuwa Sekta binafsi ahueni
Tatizo watu wanaendekeza umasikini.

Kuna watu wana wito wa ualimu, hawana wito wa Ukuu wa Wilaya.

Ukiwateua kazi ambayo hawana wito nayo umewaharibia mipango yao.

Yani, kitu cha msingi ni maelewano.

Ukiteuliwa kazi bila hata kuulizwa, umedharauliwa.

Umeonekana kwamba wewe huna maoni katika uamuzi huo.

Wewe ni mtu wa kupangiwa tu.
 
Hiyo ni wewe wasema waache Kila mtu afanye anachotaka, freedom of association 🙃

Hayo majandokando Yao it's up to them kwani Kuna watu ambao ni wakubwa kuliko serikali iliyoamua jambo lake
 
Tutakutana nao Kisutu. State na coersive institutions zote zilizo at it's disposal haiwezi kuchezewa na wahuni.
 
Mshahara wa milioni 4 na kutokuwa na uhakika na cheo Vs Mshahara M 7.8 na uhakika wa cheo utaenda wapi?
Mheshimiwa rais anajua mapato Yao hata kabla hajawateua Ila aliwateua kwa manufaa mapana ya taifa.
Ngoja tuwafanyie audit kidogo tu tuone Nani mjanja.
 
Ingekuwa wamejiari au wapo sekta binafsi sio kesi! Tatizo huko wanakofanya kazi CWT inasemekana minoti ya walimu inatafunwa...wataanzia huko😀😀
 
CWT,NI TAASISI KUBWA TANZANIA AMBAYO NI YA PILI UKIACHIA CCM,UTEUZI ALIOFANYIWA NI DEMOTION,HATA WW USINGEKUBALI,

•DHAMBI ALIYOIFANYA NI KUTOWATETEA WALIMU WALIODHULUMIWA MADARAJA YAO BILA SABABU,WALIMU WALIOAJILIWA 2013,WALIPANDA DARAJA LAO LA KWANZA,2019 LEO WALIMU HAWA WAMELINGANA MSHAHARA NA WALIAJILIWA 2014 NA 2015,TENA WALIMU WAMKATAE TU NA HUKO ALIPO,TUMECHOSHWA NA UJINGA
 
Kama umeteuliwa ni kwamba umekidhi vigezo kwa maana una sifa stahiki lakini pia umepewa heshima kubwa na Mamlaka iliyokuteua.

Jiulize kuna Watanzania wangapi wenye sifa zaidi yako lakini hawakupewa nafasi hiyo?

Vyombo vya habari vimetoa taarifa kuna Watu wamekataa Heshima waliyopewa na Mamlaka ya Uteuzi.
Itoshe kusema watu hawa kama ni kweli wapo hawana chembe ya uzalendo hata kidogo, umetumwa ukawatumikie Watanzania ukiwakilisha Mamlaka ya Uteuzi unakataa na bado unataka uendelee kwenye nafasi yako ya sasa?

Kuna mambo yanatakiwa kutiliwa shaka kwa watu hawa ikiwa ni pamoja na

1. Yawezekana nafasi walizopo sasa kuna maovu mengi wamefanya hivyo wanaogopa kuachia ghafla mengi yataibuka.

2. Yawezekana kile wanacholipwa ni kikubwa sanaa kuliko wanavyostahili, Wote tunajua Waajiri wao ni Wanachama. Je Wanacholipwa kama Mshara na Stahiki nyingine zinalingana na Waajiri wao?

3. Waajiri wa hawa watu (Wanachama) Je, ni kweli wanawapima utendaji wao kwa Maana ya Investment zinazofanyika chini ya Chama Chenu? Tutakuwa na Michango isiyokoomaa au tutafute uwezekezaji wenye tija na tupunguze michango?

Mwenyezi Mungu ibariki Tanzania

Mwenyezi Mungu mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

View attachment 2501128
Hizi nafasi Lucas mwashambwa analia usiku na mchana azipate, halafu wengine wanazikataa. Aisee kweli dunia kigeugeu
 
Sikiliza wewe
Robert S Gulenga!

Uteuzi wa nafasi yoyote ile sio wa lazima!
Mteuliwa bado anakuwa na haki ya kushukuru na kukataa!

Watu pia wanaangalia Risk Management ya Future zao!

Maana uteuzi unakuwa siku zote unamtarajia mteuzi ameamkaje leo!

Sasa kama nina kaci yangu isiyo na Pressure za kisiasa,na kukaripiwa na watu hata wasiostahili.
Iweje nisichukuwe masmuzi sahihi kwa maslahi ya familia yangu na mimi binafsi?

Je!
Kwa nini mnanuna kwa watu tena wasiowahusu,ambapo wamekataa uteuzi?

Je Chawa wa Samia,mnaona kama mama yenu kafedheheshwa au??
 
Back
Top Bottom