Luqman mohamedy
JF-Expert Member
- Jul 24, 2016
- 899
- 1,231
TANZANIA TUNAYOITAKA NI ILE AMBAYO INATHAMINI WANAOTUMIA AKILI KULIKO WANAJITOA AKILI.
Tupo kama tulivyo kisiasa,kiuchumi na kijamii sababu ya kazi kubwa waliyofanya waliotutangulia ambao tunaendeleza waliyoanzisha.
Wimbi kubwa la viongozi wa juu kuthamini wasanii na wanaowasifia watu maarufu ‘chawa’ kwa kuwaita kwenye shughuli kubwa za kitaifa na kuwaacha walimu,madaktari na watumishi wengine wanaotoa jasho lao kulipambania hili taifa inaenda kuharibu kizazi kijacho.
Watoto wetu watakuwa wakijifunza kwamba watembea uchi,wanaonyesha uzinzi hadharani na wanaosifia watu mitandaoni ndio wenye thamani kwenye jamii matokeo yake na wao watatamani kupita njia hizo.
Kama taifa miaka 30 ijayo tutakuwa na kizazi cha aina gani?
Kizazi ambacho kila mtu anataka awe mwanamuziki na chawa?
Ni muda sasa kama taifa tukatae huu mfumo wa maisha unaokwenda kutuharibu kiuchumi,kijamii na kisiasa.
Tanzania ilijengwa na watu waliotumia akili na italindwa na watu wanaotumia akili,tusijitoe akili.

Upvote
0