Yaani umesoma mind yangu! Niliongea na mtu usiku, hili wazo likawa kichwani mwangu na nikaona uvivu kulitoa.
Kuna mtu aliweka stages za mapenzi humu. Nadhani unaanzia kwenye lust (mhemko wake ni balaa, hunywi maji, hulali, kila saa unamuwaza yeye. Akikugusa hata unywele unastuka kama shoti ya umeme imekupitia).
Stage inayofuata ni love. Mie huiita zone reality! You are not always in the mood for him or her. Unakuwa unafurahia space yako pia lakini huku unammiss na kumpenda pia. Mnaweza kutofautiana bila kupata kichaa cha kurushiana maneno na kulia.
Wenye bahati zao wanaishia stage two, lakini stage three ndo ile mambo yanapoa kabisaaa! Akikuona anaskia kichefuchefu kabisa! Kutegemeana na ustaarabu wenu binafsi, hapo ndio ndondi, kashfa na mengineyo yanaingia. Wastaarabu kidogo wanatafuta small houses, wanajificha ficha wanastuka haiwasaidii wanarudi kimya kimya.
Kufanya maamuzi ya kuingia ndani ukiwa kwenye stage 1 ni suicidal! Na mojawapo ni wazo la kum'badilisha mtu. Hakuna kumbadilisha mtu aisee, take it or leave it!