'Kutibu maji' ni Kiswahili sanifu?

'Kutibu maji' ni Kiswahili sanifu?

Bingwaman

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2010
Posts
549
Reaction score
288
Hivi maji yanatibiwa? Naomba wana-jamvi tuelimishane.
 
Shida ya wanaotafsiri kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza wanatafsiri maneno na si maana.

Treatment kwa kiingereza ni neno lenye upana, lina maana ya kutibu magonjwa, na katika mahusiano linahusu hali wema au ubaya wa matendo ya mtu kwa mwingine.

Lakini kwa maji, treatment ni matayarisho ya maji kwa matumizi ya watu. Na neno sahihi lingekuwa kusafisha, au kutayarisha maji.
 
Mtu wa Shamba nakubaliana na wewe kwa asilimia 100 mkuu. Tatizo hapa ni kwamba wengi wetu hatufahamu kuwa maneno mengi ya Kiingereza yana maana zaidi ya moja na mfano mzuri ni hili neno 'treat'. Moja ya maana kadhaa ya neno hili ni 'tibu' au 'kutibu' na hili ndilo linalotumika kama tafsiri bila kujali neno hilo limetumika katika muktadha (context) upi. Kwa hiyo 'water treatment' au 'to treat water' inakuwa ni 'kutibu maji'. Kwa mantiki hii, haitashangaza kama sentensi ya Kiingereza 'He treats his wife like a queen' itatafsiriwa kama 'Anamtibu mke wake kama malkia'. Lakini 'treat' hapa ina maana tofauti kabisa na 'tibu.'
 
Back
Top Bottom