Anyisile Obheli
JF-Expert Member
- Dec 13, 2009
- 3,400
- 320
Ndoa nyingi zina matatizo kwa kuwa wengi wetu wa wanandoa tumeingia na zile tabia zetu za ujana, pasi na kujua kuwa ndoa ni mlango mwingine ambao ili uweze kupita na kumudu sheria zake ni lazima ulazimike kukua kimawazo na kiakili
pia uweze kuvua baadhi ya mavazi ya umimi na kuyavaa mavazi ya sisi yaani wawili
kuna haja ya kubadirika tu uingiapo kwenye mlango huu wa nyumba inayoitwa ndoa na humo utakutana na mavazi mengine mazuri aina ya uvumilivu, utii, heshima, adabu, na kujifanya mjinga mwelevu.
Mavazi ya ujuaji mwingi kwenye ndoa hayatakiwi kabisa, na kama unaona kuwa bado unayahitaji na yanakufaa basi ni vema ukaendelea kwanza kuyavaa ili ukijaingia humo usilete usumbufu kwa mweza wako, kwani huchafua sana utu wa mtu, maana hakuna sifa mbaya ya kuitwa aliachika akaolewa tena, aliacha akaoa tena.
Kama unaona duka lako linahitaji wateja wengi, basi ni wakati mzuri wa kuwahudumia kwanza mpaka utosheke na ndipo uingie katika ndoa maana humo mteja ni mmoja tu, wala hahitaji kupanga foleni kutaka kuhudumiwa, nasema haya kwa waume na wake.