Jambo zuri sasa wewe utatoa figo lako kwa msaada au kwa pesa? ungeliweka pia namba yako ya simu ili wenye shida ya hilo figo wakutafute.nimewahi kuandika humu sikupata attention. nimeona watu wanatafuta msaada wa figo kwa wagonjwa wao ambao baadaye wameripotiwa kufariki kwa kutozipata.
mimi niko tayari ku donate figo moja. kama kuna mwenye ndugu anaumwa kiasi cha kuhitaji figo, au mwenye kujua wenye shida hii wawasiliane nami kwa PM. nitasikia kwenu kitambo.
Umefanya jambo la maanaMkuu huwezi kujiuza wala kuuza sehemu ya mwili wako. nimejua kuwa kumbe mtu anaweza akaishi akiwa na figo moja wakati huo nimejua kuna wengine wanakufa kwa sababu figo zao zote zinafeli na wakikosa wa kuwasaidia. ndiyo maana miye nikajitolea kuokoa maisha ya mtu mmoja mwenye kuhitaji kweli.
nimesema mwenye shida kwanza ani PM kisha tutapeana namba za simu binafsi huko.