Kutoa huongeza moyo wa shukrani

Kutoa huongeza moyo wa shukrani

fakhbros

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2013
Posts
384
Reaction score
658
likuwa jioni ya majira ya baridi kali katikati ya jiji la Arusha, ombaomba na mtoto wake mwenye umri wa miaka mitano walikuwa na njaa kali ilio ambatana na hali ya dhoruba,

Walikuwa wakitembea tembetembea katika mitaa ya Sanawali.

Hawakuwa na chakula tangu asubuhi njaa ilio watesa nakuwatia udhaifu wa mwili na ngozi zao zikiwa zimepoteza nuru, Nyuso zilizojaa majonzi ziliashiria ukweli kuwa walikuwa ni watu wenye dhiki"

Ndipo walipo fanya maamuzi yakugonga mlango wa nyumba moja ilio jengwa kifahari katika mtaa ule huku wakiwa na tumaini tele japo hawakumjua yoyote katika nyumba ile.

Ndipo geti lilipofunguliwa na binti mdogo alikuja mbele yao huku akiwauliza nyinyi ni akina nani na mmetokea wapi?

Yule ombaomba akamwambia yule binti sisi tumekuja hapa tunalo tatizo la chakula vinywa vyetu havijaweka chochote mdomoni leo yapata siku ya tano ikiwa mtakuwa na ziada ya chakula basi twaomba mtupatie ili tukidhi njaa yetu"

Yule binti alikimbia mbio nakwenda kumueleza jambo hilo mama yake alie kuwepo ndani'

Baada ya kufika yule mama alikasilika sana kutokana na ujasiri wa yule ombaomba akiwa mwenye ghadhabu alimsukuma yule ombaomba huku akimkalipia kwa maneno yalio jaa kejeli'

Yule ombaomba na mwanae walijikunyata kwa huzuni huku wasijue kipi cha kufanya ndipo yule mzee maskini alipo muuliza yule mama"

Samahani sana mama kwa yote yaliotokea lakini tunakuomba utupatie japo zawadi ndogo kutoka kwako'

Yule mama alikataa.

“Mama , hatujala chochote tangu asubuhi. Tafadhali tupe chakula?”

Uso wa yule mama ulizidi kukunja ndita

Yule maskini akasema tena
"Hata mabaki yanaweza kutufaa?"

yule mama alikataa tena.

yule ombaomba akamwambia tena je hata "Nguo za zamani?"

Mwenye nyumba alikataa tena.

yule ombaomba alipo ona yule mama hawezi kumsaidia kitu
akasema tena'

“Mama unaweza kutupa mchanga kutoka kwenye bustani yako?”

yule mama alionekana kushangazwa na ombi hilo,

Akatikisa kichwa kwa ishara ya kukubali kuwapatia ule mchanga akaenda na kumletea mchanga.

Wale ombaomba wakambariki na kuanza kuondoka zao'

Yule mama, akiwa bado amechanganyikiwa,
Huku wale ombaomba wakiwa wanatoweka nje ya geti'

Ndipo alipo amua kumfata yule ombaomba kwa kasi pale nje'

Samahani Mzee wangu naomba kujua kwa nini baada ya kuwanyimeni kila kitu mmeomba mchanga je utakufaaeni katika lipi?"

Yule mzee ombaomba kwa upole kabisa akamjibu yule mama tumekuomba udongo ili ikufundishe kutoa kitu katika Maisha yako"

Kisha wale watu wakatoweka"

Village life.jpeg
 
Back
Top Bottom