Kuna kanisa moja nilihudhuria ibada yao wanakuambia kuna sadaka ya kujimaliza yaani utoe hela zote ulizonazo ili uweze kugusa moyo wa Mungu huku wewe ukirudi home kwa mguu/ kupata muujiza wa kufika nyumbani either kwa lift au kupata hela kwa njia ya ajabu;
Sasa juzi kuna sehemu mtume kasema kila mtu aikanyage hela kubwa kuliko zote alizonazo na kama huna hela ya kigeni ikanyage uiombee kwa kuiweka fedha chini ya miguu yako mwisho wa siku akasema kama una hela za kigeni njooni mbele mkanyage hapa mbele huku akitoa za kwake akawapa wachungaji wake wakanyage ilipofika mda wa mwisho akawaambia wachungaji wake rudisheni zile za kwangu halfu wengine wote wekeni madhabahuni; kiroho safi nilikuwa nimekanyaga teni yangu kwa imani ila mfukoni nilikuwa na zaidi ya laki saba nikarudisha ten yangu nikaenda toa buku kwa kuamua kufuata mkumbo ila sio kwa nia ya kubarikiwa;
Ila sasa niliona jamaa mmoja maarufu alitoka na mkewe wote na dola mia mia ; mwingine na watoto wake jinsi walivyokuwa mbele wanatamani kukimbia ndo macamera wameweka kwao makusudi inabidi watoe tu; ila sio kwa mapenzi yao; lengo la uzi huu sio kuwasema vibaya watumishi ila kwa suala la kutoa ili ubarikiwe ni soma ambalo halijawahi kuniingia akilini kabisa..
Niseme tu ukweli naonaga watu wakitoa sadaka zao za shukrani; miujiza; fungu la kumi ila sijawahi shiriki hizo sadaka sadaka ninayotoa kwa moyo mkunjufu ni moja na huwa sitoi zaidi ya buku labda kama sina change na yote hii naamini sina namna naweza mshawishi Mungu anipe baraka zake ila ni kwa neema tu.
Kuna watumishi wengi naamini Mungu anawatumia ila kwenye namna ya utafutaji wa pesa wanafeli; sijui kama wanapataga maoni ya waumini.
Masikini wengi wanateseka sana kwa kumaliziwa vipato vyao makanisani.