Kutoa kifurushi kutoka nje ya nchi

Kutoa kifurushi kutoka nje ya nchi

yahoo

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2011
Posts
3,526
Reaction score
1,409
Naombeni msaada hapa rafiki yangu kutoka ghana ananitumia laptop 2, moving camera na vitu vingine vichache vya dizaini hizo.

Nauliza ni kampuni gani reliable nimshauri aitumie kunitumia hivyo vitu na gharama za yeye kunitumia hivyo vitu kuja huku ni kiasi gani na taratibu zikoje mpaka huo mzigo kunifikia.
 
Rafiki toka Ghana? angalia usiingizwe mjini na scams za nigeria kama amekuambia ulipie hela jua utaingizwa mjini....
 
ONANA NA MKUU Rich Pol atakusaidia zaidi
Naombeni msaada hapa rafiki yangu kutoka ghana ananitumia laptop 2, moving camera na vitu vingine vichache vya dizaini hizo.

Nauliza ni kampuni gani reliable nimshauri aitumie kunitumia hivyo vitu na gharama za yeye kunitumia hivyo vitu kuja huku ni kiasi gani na taratibu zikoje mpaka huo mzigo kunifikia.
 
Last edited by a moderator:
Nahisi jamaa anaenda ingizwa mkenge sasa hivi haya all the best mkuu
 
rafiki kutoka ghana,dah nishapata wasi wasi na huyo rafiki japo simjui
 
Mweee!!! Nicheke mie
yahoo mzigo wako umefika?????

Ha ha nimegundua kuwa ni marapeli lakini sikutuma pesa,walitaka nitume pesa kwaajili ya kutumiwa laptop 2,video camera nk...
 
Last edited by a moderator:
Ha ha nimegundua kuwa ni marapeli lakini sikutuma pesa,walitaka nitume pesa kwaajili ya kutumiwa laptop 2,video camera nk...

Wangekutapeli ndio akili ingekukaa sawa, huyo rafiki shida zake na za ndugu zake kazimaliza hadi aku2mie wewe hvo vitu???

Alafu wao wanatuona sisi malimbuken wa laptop, ipad nk. Wakwende zao
 
Back
Top Bottom