THE GREAT CAMP
JF-Expert Member
- Jun 29, 2012
- 765
- 194
Shahawa ni yale maji mazito meupe yamtokayo mwanaume wakati anafanya tendo la ndoa. Mbegu za kiume huwezi kuziona kwa macho mpaka utumie darubini maalumu. Shawaha (semen) hutengenezwa tofauti kabisa na mbegu. Mbegu za kiume (sperm) hutengenezwa kwenye (seminiferous tubules). Shahawa hutengenezwa kwenye( seminal vesicle). Hivyo basi inabidi Sperm zisafiri kwenye mirija maalumu (Epidydimis) hadi ziende kuchanganyikana na Shahawa ndipo ziogelee humo. Unapo kojoa (ejaculation) ndipo shawaha zilizo changanyikana na mbegu hutoka na kumuiingia mwanamke. Sasa kama mirija ya epidydimis imeziba, baba mbegu haziwezi kwenda kwenye shahawa, hivyo utakua unatoa maji tu meupe yasiyo kuwa na mbegu za kumpa mimba mwanamke.
NB: Kabla ya kumtuhumu mwanamke kuwa hazai nenda kafanye uchunguzi wa Maumbile yako ya uzazi ili ujue kama hauna matatizo. Maana Unaweza UKAWA UNATOA SHAHAWA ZISIZO KUWA NA MBEGU.
Huu ni mfano mmoja tu ipo mifano mingi:
SOURCE: Mimi mwenyewe, anaye bisha abishe lakini huo ndio ukweli, tusaidiane kufahamu mambo kabla ya kudharilika.