Kutoa mimba kwa makusudi nini hasa?

Kutoa mimba kwa makusudi nini hasa?

kipili

Member
Joined
Oct 6, 2011
Posts
29
Reaction score
6
nimepata kusikia sana kitendo cha kutoa mimba tokea nasoma primary hadi chuo'pia nafahamu kuwa kitendo hicho ni kosa lajinai,kwanini , naje ? kutoa KWA MAKUSUDI mimba mara kwa mara kuna madhara gani? kwa mwanamke
 
Kwanini ni kosa la jinai?Kwasababu ni kukatisha maisha ya kiumbe ambacho hakiwezi kujitetea.
 
Kuhusu kosa la jinai sina uhakika maana wengine wanatoa mimba kwa kufuata ushauri wa daktari (medical grounds) kuwa mimba hiyo inaweza mletea matatizo katika ukuaji wake huko mbeleni etc. Kutoa mara kwa mara nayo ni mbaya navyoelewa mimi tena mbaya sana maana unauchakaza au unaulegeza mfuko wa uzazi kiasi kwamba huko baadae ukiwa una hamu ya mtoto inakuwa ngumu mimba kushika na kukaa katika mfuko wake kwa miezi tisa. ndo maana wengine (sio wote) huwa wanawekwa bed rest miguu imenyanyuliwa juu ili kuepusha mimba hiyo kutoka na wakati huo huo wanakuwa wameshafanyiwa minor operation ya kuweka kiraka chini ya mfuko angalau kiweze kubeba mtoto mpaka hapo atakapozaliwa.

Tusubiri wajuzi watueleweshe kiundani
 
Back
Top Bottom