Kutoa moshi

kinehe

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2016
Posts
205
Reaction score
198
Habar wadau naomba kujua kwa nn gari inatoa moshi mkali yaan ukifika machoni macho yanawasha mwanzo tatzo hl halikuwepo.
 
Haichomi mafuta vizuri na linaongeza matumizi ya mafuta waone wataalamu wataondoa ni tatizo pia husababisha gari kukosa nguvu
 
hapo huenda spark plugs hazichomi vizuri mafuta
 
Habar wadau naomba kujua kwa nn gari inatoa moshi mkali yaan ukifika machoni macho yanawasha mwanzo tatzo hl halikuwepo.
Moshi unaotoka ni wa rangi gani

Tuanzie hapo ili upewe majibu sahihi kwasababu kila rangi ya moshi kwenye gari unatafsiri tofauti
 
Moshi unaotoka ni wa rangi gani

Tuanzie hapo ili upewe majibu sahihi kwasababu kila rangi ya moshi kwenye gari unatafsiri tofauti
Mweusi. Ila co mwing ni wakawaida2
 
Mweusi maana yake ni kwamba uchomwaji wa mafuta haupo sahihi kutokana na kiwango cha hiyo kutokua katika uwiano mzuri hivyo ni vyema kuangalia mfumo wa upepo unaoingiza hewa kwenye combustion chamber

Pia kuna sababu nyingine wadau wanaweza kuongezea
 
Hiyo maana yake ni kwamba ule mchanganyiko wa hewa na mafuta hauna uwiano sahihi,kama hewa ni nyingi kuliko mafuta hii inaitwa "lean mixture" hii huwa inatoa moshi mweupe, na kama mafuta ni mengi kuliko hewa hii inaitwa "rich mixture" hii huwa inatoa moshi mweusi au moshi wenye kama ubluu flani hivi lakini sio bluu kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…