Kutoa na kupokea, ni moja ya sheria ya ulimwengu

Kutoa na kupokea, ni moja ya sheria ya ulimwengu

Magical power

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2022
Posts
2,158
Reaction score
5,626
Kutoa na kupokea
1736965420140.jpg
👇👇
👉sheria ya ulimwengu.
Hii ni moja ya sheria ya ulimwengu /universal laws.

Muda wote ulimwengu unatoa
Ulimwengu unatoa uhai ,
Ulimwengu unatoa Baraka
Ulimwengu unatoa maumivu kwa watu na vitu.

Ulimwengu unatoa fursa mbalimbali kwa watu .
Ulimwengu unatoa maarifa nk nk

Lakini pia usisahau kuwa ulimwengu unapokea ,ulimwengu unapokupa basi na wew toa ,kwa maana unapotoa wenyewe unapokea ,

Ulimwengu unapokea Magonjwa yako,
Ulimwengu unapokea matatizo yako ,
Ulimwengu unapokea vitu vyote .

Sheria hii ni vyema kuibalance ili kuruhusu nguvu ya Ulimwengu kufanya kazi katika mtiririko sahihi.

Unapoona umepokea ,toa pia ili kuruhusu mtiririko wa kutoa na kupokea kwenda sawa.

Kuna watu wanasoma tu makala mbalimbali bila kutoa hayo maarifa pengine👉ulimwengu utakunyima pia.

Unapopewa toa pia.

Simaanishi kutoa pesa au vitu ,kitu chochote unachopokea ,hakikisha unatoa pia ili kuruhusu mzunguko kuendelea.
 
Keys of the Universe.

111=3
222=6
333=9

Hivyo 369 ni funguo la ulimwengu.

Ukitaka kuufunguq ulimwengu na kuingia ndani yake na kutawala .

Hakikisha unakuwa/unamiliki funguo Hilo .
Funguo Hilo lii nda
1736966191888.jpg
ni mwako.
 
Kila kitu ni ndani mwako .

Anzia kufanya maamuzi ndani mwako.

Anzia kujiponya ndani mwako.
.
Anzia kukua ndani mwako/Rohoni mwako.

Anzia Kila kitu ndani mwako.
Iwe ni uponyaji kwa mmeo,mkeo,mtoto,biashara ,mahusiano ,Magonjwa nk .
Yote hayo chemchemi yake ipo ndani mwako.

Anzia kuviita au kuviongelesha ndani kwanza ,UTAONA vinakutii na Kuja katika umbile.

1736966276194.jpg
 
Vitu vinavyonyon
1736966354050.jpg
ya nguvu zako ndani mwako

1.kuwaza vitu nje yako.
Mfano unawaza Namna ya kupata ada ya mtoto.
Unawaza biashara yako kisa imedororq ,
Unawaza Mme wako au mke wako kisa amekuwa hayupo sawa na wew
Wazo lolote unalowaza nje yako ni sehemu ambayo inaiba nguvu zako za ndani ,ndio maana ukija katika ulimwengu huu wa nje unakuta huna uwezo wa kuzitumia nguvu zako za ndani.

2.matendo yote hasi kama vile dhuluma ,ukaidi,masengenyo,aibu,wizi,maneno yoyote machafu ,kujiona /ubinafsi,tabia zote mbaya huwa zinanyonya nguvu zako zilizoko ndani,undani wako huwa unaibwa na zile kelele unazozifanya.

3.vyakula sumu.
Kuna baadhi ya vyakula ambavyo vina kemikali na sumu ,hivyo pale unapovitumia huweza kuathiri Malango yako ambayo ndio kiunganishi Cha undani wako.

4.kumilikiwa na viumbe wenye nguvu hasi.
Hapa ulimwenguni Kuna viumbe wenye nguvu AMBAO wanaweza kumteka mtu na kumtumikisha watakavyo,
Wew utadhania una Hasira kumbe umekuwa controlled kutokea mahala,
Wew UTAONA una roho mbaya kumbe ni mateka kutokea sehemu faulani,
Wew UTAONA ni mzinzi wa kutupa ,kumbe ni nguvu zimechannel kutokea dension Fulani.

5.Karma mbalimbali zinazokuandama.
Kumbuka apandacho mtu NDICHO atakachovuna ,na mavuno hayo ni kifungo kwako katika nguvu zako za ndani.

Ni vyema sasa ,kuanzia kuchannel kutokea ndani mwako,Kila jambo ulifanyalo Anzia ndani mwako,iwe mke/Mme unamuhitaji ,yupo hapo ndani yako,ingia umuone muongee nae ,mkubaliane huko ,ndipo mje huku muendelee na maisha katika mwili/miili.
Kila kitu anzia kutokea ndani ,na mafanikio yako hayapingiki kwa maana ni kutokea kwenye chemchemi ya asili iliyofanya vyote u ivionavyo na usivyoviona katika macho haya ya nyama
 
Sheria ya kwanza ya Ulimwengu.

Sheria ya Umoja wa kimungu.

Sheria hii inasema ,Kila kitu kimeunganishwa .

Hapo ulipo umeunganishwa na Kila kitu,umeunganishwa na marafiki zako,umeunganishwa na Maadui zako,umeunganishwa na Ancestors wako,umeunganishwa na Ulimwengu wote.

Sema kinachokufanya ujione upo separete ni hako kamwili ,ila siku ukipoteza mwili huo ndipo utakapojua kuwa sisi sote tumeunganishwa.

Hapo ulipo hata husogei popote,hata hiyo kazi unayoililia na kuhombania haipo.
Hata hujawahi kwenda popote ,kinachokufanya ujione ulivyo ni sababu ya hayo maumbile au illusion/Udanganyifu.

Kila kitu katika ulimwengu ni nishati.
Sisi sote ni kiumbe kimoja ,hatuna tofauti kabisa kwa maana sisi ni Energy.

Sheria ya pili ni Sheria ya vibration/mitetemo.

Sheria hii inasema kwamba ,Kila kitu katika ulimwengu huu kinaundwa na nishati ambayo inatetema kwa mzunguko maalumu.

Iwe kitu kinachoonekana au kidichoinekana vyote vimeundwa kwa nishati ya mtetemo.

Hivyo ili kukivutia kitu inahitajika kuinua mitetemo yako ili kuvuta kitu unachokihitaji .
Iwe unahitaji mpenzi,pesa ,utajiri ,umaarufu nk ,ni jambo la kuinua mitetemo yako tu.

Mitetemo yako inapokuwa juu ,kuwa makini kuvuta vitu usivyovihitaji ,usiwaze juu ya wachawi ,usiwaze juu ya umaskini,usiwaze juu ya jambo lolote baya kwa maana utakivuta kitu hicho kwako bila kujua.
1736966421101.jpg
 
UNIVERSE.

Universe ni vyote ,wew hapo ni universe .

Wewe unajiona ni mwanamke,mwaume,mdudu,mnyama,nk lakini Mimi nakuona kwanzq huna jinsia Bali ni the One.

Kwa hiyo naongea na vyote ,naongea na wew,naongea na yule,naongea na vitu ,naongea na mawe ,kwa maana vinanisikia NAMI navisikia.hii ni kwa sababu sisi tunasikilizana ,hatuna tofauti.

Tofauti yake ni kwamba wewe hujajua kama up
1736966570224.jpg
o Ivo.
 
Sheria 12 za Ulimwengu.

Sheria hizo ni.

1.Sheria ya Umoja wa kimungu.

2.Sheria ya mtetemo

3.Sheria ya mawasiliano.

4.Sheria ya kuvutia.

5.Sheria ya Sababu na athari.

6.Sheri ya kitendo kilichovuviwa.

7.Sheria ya ubadikishaji wa nishati daima.

8.Sheria ya Fidia .

9.Sheria ya Uhusiano.

10.Sheria ya polarity.

11.Sheria ya mdund
1736966611165.jpg
o.

12.Sheria ya jinsia.
 
naona mko wengi wenye mada hizi ila hamtulii sehem moja sasa hebu turudi kwenye funguo mana yangu sjui nutaipataje.
 
Full moon;Namna ya kupokea .

👉fanya sana meditation ,ukiwa kwenye tahajudi au la omba ukitakacho kwa dhati kitakuja haraka sana.

👉Sambazq upendo kwa wengine ,nawe Ulimwengu utakupatiq ulichotoa mara dufu.

👉Andaa maji kwa ndoo na weka chumvi ya mawe ,Anika kwa mwezi unakomulikq ndani ya saa au masaa 2 baada ya hapo nendq kaoge na Omba ukitakacho na universe itakutendea hitaji lako.

👉chukua chupa yenye kuonesha kwa nje na ndani,weka maji na chumvi ya mawe ,halafu Andika mahitaji yako kwenye karatasi nyeupe ,weka karatasi ndani ya maji ya chupa na funga kizibo ,kaiweke chupa hiyo kwenye Nuru ya mwezi(mchana unaitoa ,usiku unaiweka nje ) baada ya siku 3 ,nenda kamwage maji kwenye mti wowote unaozaaga matunda, na karatasi kama haijayeyukq ,ikaushe na ichome moto,universe utakupa hitaji lako unalot
1736966761835.jpg
aka .
 
Meditation.

Andaa mazingira yaliyotulivu,iwe ndani ya chumba ,porini ,kwenye miti au popote pale.
Mazingira yako YAWEZA kuwa safi ,kama ni ndani waweza washa udi ,ili kuatract positive Energy na kuondoa negative Energy.(kumbuka sisi ni vyote)
Ni vyema pia ukavaa mavazi yaliyo mapana yasiyokubana ili uwe huru zaidi.

NB ni vyema sana kwa mazingira yaliyotulivu .

Mkao.
Chagua mkao unaopendelea Kukaa,waweza Kaa chini kwa kukunja miguu,kukaa kwenye kiti au kulala Chali kwenye mkeka ,kitanda nk .

Fumba macho yako ,taaratiibu ,huku ukiwa umejiachia mwili wako.

Vuta Pumzi ya kawaida na kuitoa .
Halafu Vuta Pumzi ndeefu(waweza Kaa nayo kwa sekunde chache) na kuitoa yoote ,ukiwq umeliacha tumbo bila kitu(tupu).

Vuta Pumzi ya Namna hiyo mara 7 kama nilivyoelekeza hapo juu na kipindi hicho ukiwa ufahamu wako umeangalia kwenye paji la uso na hakikisha hakuna mawazo yanayoingia ndani mwako Wala kutoka .

Endelea na kuangalia kwa ufahamu kwenye paji la uso .
Ukiona mawazo yanakuvamia Anza Pumzi Ile nilivyokuambia.

Baada ya muda mwili utaweza kushikwa na Ganzi,lakini weww endelea na kujitizama pajini kwako kwa ufahamu.
Kwa Leo tuishie apa 🙏🏽
1736966842899.jpg
 
MTU NA KUJITAMBUA.

Watu wengi siku za Leo,wamekuja na shauku ya kutaka kujitambua,je twajua au hatujui maana yake?.

Utambuzi wa mtu upo wa Namna nyingi sana.
Kuna kujitambua kifikra,Kuna kujitambua kiroho ,Kuna kujitambua kiakili,Kuna kujitambua kimwili nk nk.

Sasa ninachotaka kuongelea ni utambuzi wa kujijua wewe ni nani.

Utambuzi ni kujijua ndani mwako,kurudi ndani mwako ,kurudi kwenye asili,Sasa hapo ndipo ilipo kazi,wengi tunajua tunapo Rudi kuitambikia Mizimu ndiko kujitambua,wengine tunajua pale tunapoielezea historia ya Afrika saana ndiko kujitambua,Wengine wanajua pale tunapokataa Dini na madhehebu yake kisa yamekuja na wakoloni ni kujitambua nk ,Lahasha tunafeli ,kuabudu mizimu,Kumiliki majini na Negativity zingine zifananazo vyote hivyo ni mitetemo ya chini sana.

Asili ni Ile mwanzo ,Ile iliyokuwako ,iliyoumba Kila kitu,iliyokuumba na mwili wako,hiyo ndio LIGHT AND SOUND, ambayo Leo hii ipo ndani mwako,hiyo ndio asili ambayo ni mitetemo ya juu sana,ipo katika mwendo wa Ajabu mno,ndio maana haifi milele yote, hayupo mchawi ,Wala jini ,Wala mizimu Wala Mganga,,Wala chochote kiwezavyo kushindana nayo.

Asili Iko ndani mwako,jishushe na kimwili Kako hako nawe utaishuhudia,na itakutendea mambo makubwa na ya
1736966932778.jpg
Ajabu mno.
 
Tafsiri na maana ya Kifo.

Watu tumekuwa katika sitofahamu juu ya ni Nini haswa hii kifo.

Tumebaki na Uoga tu ,ya kukuigopa kifo na kubaki bila majibu juu ya watu wanapokufa huwa wanaenda wapi?

Nalijaribu kufundisha juu ya masomo ya dimensions lakini watu hawakuelewa,

Sasa tuanze na kifo Cha kiroho.

Tunasema wew upo katika mwili huu lakini pia upo katika ulimwengu wa kiroho,ndiko ulikoanzia ndipo ukaja katika mwili huu wa nyama.

Tunasema ya kwamba wew umelala chini ya kitako Cha UTI wa Mgongo ,umekufa hapo,huna ujanja wa kuamka,sense zako zipo mbaali sana hiyo tunasema umekufa ukiwa unatembea ,Rohoni/ndani mwako umekufa.hivyo siku ukipoteza mwili wako huu wa nyama halafu hujaamka kwenye kitako Cha UTI wa Mgongo ,hapo huna ujanja zaidi mpaka uje uzaliwe Tena katika maumbile mengine.

Kifo Cha kimwili.

Aina hii ya Kifo Kila mmoja anakijua ,tunaona watu,wanyama ,mimea nk jinsi wanavyokufa na kutoweka katika mwili wao
Kitendo hiki huitwa kifo Cha kimwili.
Na sababu zinazosababisha kifo Cha kimwili ni Magonjwa,ajali mbalimbali ,sumu,kujinyonga nk nk.

Lakini Ukweli ni KWAMBA kifo hakipo ,ila mazingira ya Hofu na kutokujitambua kunafanya tuwe na Hofu juu ya Kifo.

Pale unapoamka katika usingizi uliolala katika kitako Cha UTI wa Mgongo,tayari unaanza kuishi maana wewe ni nguvu ya uhai ,UTAANZA kuflow kutokea chini ya kitako Cha UTI wa Mgongo ,Hadi mbinguni ,unatoka mbinguni Hadi kuja kwenye maumbile ,Sasa siku ukifa kifo Cha kimwili na upo macho(hujalala) ,tayari unaijua njia ya kuutoroka mwili kwenda kwenye Uzima.

Hayo ni machache juu ya Kifo ,lakini endelea kunifatilia masomo yanayohusu dimensions za kiroho,utapata upeo m
1736966984847.jpg
kubwa sana juu ya Kifo.
 
Mambo ambayo huongeza mitetemo ndani mwako.

👉Utulivu(kufanya meditation).ni njia Bora sana ya kufungua Malango yako.

👉Kula vyakula rafiki,vyakula rahisi,vyakula ambavyo Sio sumu kwa mwili ,ambavyo havifungi Malango yako.
Mfano matunda ,mboga za majani ,mimea inayoinua mitetemo ya ndani.

👉Kufunga /Fasting ,ni njia endapo ikitumiwa vyema huweza kuinua uwezo ULIOPO ndani ndani mwako na hatimae kupangilia Malango yako.

👉Kupenda kutembelea maeneo ya asili ukiwa peke yako,kukaa peke yako porini kwa malengo ya kutafakari .

👉Kuwa na Upendo kwa Kila kitu,mpende Kila mtu,hata Adui yako ,hata mbakaji ,hata mla rushwa ,hata mwizi,hata mchawi kwa maana anatenda Hilo kwa kutumia ufahamu mdogo wa maumbile ,na wew huna hesabu na maumbile.

👉Matumizi ya Vito mbalimbali ,mawe madini nk ,kama bracelets ,Pete ,Shanga nk nk.

👉Matumizi ya baadhi ya mimea ambayo huweza kutumiwa kama dawa,na kuweza kufungua na kubalance baadhi ya Malango yako ya kiroho.
1736967027901.jpg
 
Mambo yanayoharibu utulivu wako au Energy yako.

👉kujichanganya na watu Negativity lukuki.

👉matumizi ya vyakula vyenye sumu.

👉mitazano hasi /mitazamo isiyofaa.

👉matumizi ya vilevi mbalimbali.

👉matumizi ya tendo la ndoa kupita KIASI/ni jambo jema kwa wanandoa ila likiwa too much ,litakunyonya Energy yako.

👉Kupenda makelele yasio na maana,music ,makelele ya kwenye sherehe nk.

👉Kusema Uongo/utafunga lango lako la 5 na hutapata nguvu za kunena utakacho.

👉Tabia zako Hadi

👆
1736967084005.jpg
👆👆

Jichunguze.
 
Kutoa na kupokea
View attachment 3202871 👇👇
👉sheria ya ulimwengu.
Hii ni moja ya sheria ya ulimwengu /universal laws.

Muda wote ulimwengu unatoa
Ulimwengu unatoa uhai ,
Ulimwengu unatoa Baraka
Ulimwengu unatoa maumivu kwa watu na vitu.

Ulimwengu unatoa fursa mbalimbali kwa watu .
Ulimwengu unatoa maarifa nk nk

Lakini pia usisahau kuwa ulimwengu unapokea ,ulimwengu unapokupa basi na wew toa ,kwa maana unapotoa wenyewe unapokea ,

Ulimwengu unapokea Magonjwa yako,
Ulimwengu unapokea matatizo yako ,
Ulimwengu unapokea vitu vyote .

Sheria hii ni vyema kuibalance ili kuruhusu nguvu ya Ulimwengu kufanya kazi katika mtiririko sahihi.

Unapoona umepokea ,toa pia ili kuruhusu mtiririko wa kutoa na kupokea kwenda sawa.

Kuna watu wanasoma tu makala mbalimbali bila kutoa hayo maarifa pengine👉ulimwengu utakunyima pia.

Unapopewa toa pia.

Simaanishi kutoa pesa au vitu ,kitu chochote unachopokea ,hakikisha unatoa pia ili kuruhusu mzunguko kuendelea.
Asante kutukimbusha mkuu barikiwa
 
Back
Top Bottom