Kutoa na kupokea rushwa Watanzania wanafundishwa katika sehemu hizi 3.

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
1. Shule za sekondari hasa kidato cha sita.
Shule nyingi kwenye practical za physics, chemistry na Biology walimu wa masomo husika wanawachangisha wanafunzi pesa ili wawape madini mapema kabla ya siku husika.
Kitendo hichi ni sawa na kumfundisha mwanafunzi au kumuandaa mwanafunzi awe mla/mtoa rushwa nzuri huko mbele aendako.

2. Vyuoni.
Kuanzia vyuo vya chini, kati mpaka vyuo vya juu wakufuzi na wasimamizi wamewageuza wanafunzi kama sehemu ya pili ya mapato.
Kipindi cha mitihani uhuni uhuni unafanyika mwingi sana ili tu wanafunzi wafaulu na walimu wapate pesa.
Kitendo hichi direct kinazalisha wahitimu (Watanzania wala rushwa) huko waendako.

3. Mchakato wa kupata kazi
Ni desturi ya miaka na miaka ili upate kazi sehemu fulani ni aidha wewe au mzazi wako ajuane na mfanyakazi au bosi wa ofisi husika. Hii iko private na government. Kama huna connection unaitafuta connection ya haraka kwa nguvu ya pesa.

Sio wote walioajiriwa wametoa rushwa au wamejuana na mabosi. Ila mifumo deeply iko hivyo.

Nimefanya mahojiano na wanajeshi kadhaa suala la kutoa takrima kwa wakufuzi ili wawatupie taulo au wawape utawala kwa lugha nyepesi wawape ahueni kwenye mikesha n.k lipo sana.

Cha ajabu mpaka daktari amewahi kunithibitishia kuwa wamewahi kuchanga pesa ili wapate utelezi.
Mpaka sasa sijawahi kuona jitihada za kweli za kusomesha rushwa na ufisadi Tanzania.

Afisa mmoja wa PCCB alinitonya kuwa alitoa pesa ili apate uhamisho kutoka Lindi kuja Dar es salaam
 
Mkuu pamoja na hayo, usisahau pia viongoz ndio vinara wa kulecture suala la rushwa kwa watz.
Unaweza kuta hata waziri wa sheria(mb) anagawa rushwa ili apate kura jimbin kwake.
 
1. Shule za sekondari hasa kidato cha sita.
Shule nyingi kwenye practical za physics, chemistry na Biology walimu wa masomo husika wanawachangisha wanafunzi pesa ili wawape madini mapema kabla ya siku husika.
Kitendo hichi ni sawa na kumfundisha mwanafunzi au kumuandaa mwanafunzi awe mla/mtoa rushwa nzuri huko mbele aendako.
2. Vyuoni.
Kuanzia vyuo vya chini, kati mpaka vyuo vya juu wakufuzi na wasimamizi wamewageuza wanafunzi kama sehemu ya pili ya mapato.
Kipindi cha mitihani uhuni uhuni unafanyika mwingi sana ili tu wanafunzi wafaulu na walimu wapate pesa.
Kitendo hichi direct kinazalisha wahitimu (Watanzania wala rushwa) huko waendako.
3. Mchakato wa kupata kazi
Ni desturi ya miaka na miaka ili upate kazi sehemu fulani ni aidha wewe au mzazi wako ajuane na mfanyakazi au bosi wa ofisi husika. Hii iko private na government. Kama huna connection unaitafuta connection ya haraka kwa nguvu ya pesa.
Sio wote walioajiriwa wametoa rushwa au wamejuana na mabosi. Ila mifumo deeply iko hivyo.
Nimefanya mahojiano na wanajeshi kadhaa suala la kutoa takrima kwa wakufuzi ili wawatupie taulo au wawape utawala kwa lugha nyepesi wawape ahueni kwenye mikesha n.k lipo sana.
Cha ajabu mpaka daktari amewahi kunithibitishia kuwa wamewahi kuchanga pesa ili wapate utelezi.
Mpaka sasa sijawahi kuona jitihada za kweli za kusomesha rushwa na ufisadi Tanzania.
Afisa mmoja wa PCCB alinitonya kuwa alitoa pesa ili apate uhamisho kutoka Lindi kuja Dar es salaam
Tunaomba utupatie pia njia mbadala za kuepukana na hizo rushwa.
 
Hapo njia ni mbili tu
1.kila Mtanzania afuate taratibu na sheria. Akatae kutoa au kupokea rushwa mahali popote
2. Serikali iweke usawa kwenye elimu, ajira na fursa zingine zote
 
Dah. Trump nae analalamika kuna rushwa sana Nchi za nje. ULAYA NA MAREKANI.

kwa tafiti zako huko wao wamarekani na watu wa ulaya wanaanza kufundishwa kidato cha ngapi?

Ni desturi ya miaka na miaka ili upate kazi sehemu fulani ni aidha wewe au mzazi wako ajuane na mfanyakazi
Tukizingatia neno Nepotism limeanzia na kutokea wapi, utaona tumejifunza kutoka kwa Wazungu rushwa.

Au sio batanzanie?

hayo niliyo yanukuu hayana ukweli wowote ule. Na kwa msingi huo hata hoja zako hazina mashiko.
 
Rushwa inaanzia ngazi ya primary school. Mtoto anaagizwa 200 ya mchango anaenda sema nyumbani 300 zinahitajika shule
 
Back
Top Bottom