KUTOA UCHAFU MWILINIi......................

BIG X

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2011
Posts
777
Reaction score
212
Wakubwa kuna hii huduma ya kutoa uchafu mwilini nadhani imeanzishwa na watu wa jamii ya kichina lakini sasa naona kuna wakenya na baadhi ya waTZ nao wanatoa hiyo huduma. Kuna vitu wanakufunga mwilini na miguu yako inakuwa kwenye beseni lenye maji, hivyo vitu vinakuwa vimeunganishwa na mashine, baada dakika chache baada ya hiyo mashine kuwashwa maji yanabadilika rangi na kuwa myeusi kabisa na mafutamafuta ambayo wanasema ni uchafu kutoka mwilini.

Naomba kujua ukweli wa hii tiba. na pia kama kuna madhara yoyote ambayo mtu anaweza kupata.
 
nishasiaga kuna iyo kitu arusha na nilijiuliuza maswali mengi sana yasiyo na majibu,ngoja tusubiri wataalam watujuze
 
make sure hauna Kansa kabla ya kutumia hiyo huduma
 
kutumia hiyo tiba ilihali una kansa ni kujimaliza, kuna daktari alinidokeza

Wenyewe wanasema haina tatizo lolote. Kama una cancer ina madhara gani!!!
 
hao watakuwa na lao jambo, wanatafuta kitu so wanaamua kufanya experiment, najua itakuwa na madhara makubwa tu japo cyajui.
 

inapatikana wapi mkuu. Bado nasubiri jibu wakuu.
 
Nimekutana na huduma hii mara ya kwanza Morogoro wakati wa maonyesho ya wakulima nane nane, kuna banda moja jamaa (wabongo tena) walikuwa wamekusanya watu kibao! Mara ya pili nikawakuta jamaa wengine Lindi (Kilwa Masoko) nao pia wabongo. Nikajaribu kuuliza wataalamu wa afya/madaktari wanijuze lakini ki ukweli wote niliowauliza walisema ni utapeli tu kwani haina maelezo ya kisayansi: mfano walihoji ni vigumu sana kuweza kuyatoa mafuta mwilini kupitia kwenye vinyweleo vya ngozi, na ndiyo maana wengi wenye mafuta mengi mwilini imekuwa kazi kweli kama hawafanyi mazoezi au kuwa makini kwenye diet. Pia kuna jamaa yangu mmoja aliniambia kwamba siku moja alikwenda kwenye hiyo tiba na baada ya maandalizi kabla hakaweka miguu kwenye beseni lenye maji, yule mhusika nadhani alipitiwa so akawasha hicho kimashine mara maji yakaanza kubadilika rangi kuwa meusi!! jamaa akamwambia mbona yamebadilika kabla hayaweka miguuu?? jamaa akaanza ooh mashine mbovu...jamaa yangu akaachana nao. Ushauri wangu: Tujenge tabia ya kuuza watu professional tunapokutana na mazinira kama haya kabla ya kufamia tu maana utapeli umezidi sana.
 
Wanachofanya hapo ni electroplating ebu pitieni electrolysis utapata mwanga hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…