Kutoa ushuzi au kujamba katika Lugha ya Kingereza

Kutoa ushuzi au kujamba katika Lugha ya Kingereza

Nyanda Banka

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2023
Posts
304
Reaction score
1,054
MSAMIATI UNAOTUMIKA KUMAANISHA ‘KUJAMBA’ AU ‘KUTOA USHUZI’ NI:

1. Fart: Hili ndio neno linalotumika sana. Huweza kutumika kwenye mazingira rasmi na yasiyo rasmi (Formal and Informal settings)
Mfano: Jesca farts a lot. (Jesca hutoa ushuzi sana / Jesca hujamba sana)

2. Flatulate: Hili ni neno rasmi (formal), ivyo hutumika sana kwenye mazingira rasmi.
Mfano: Jackline flatulated in the headmaster’s office. (Jackiline alitoa ushuzi ofisini kwa Mkuu wa Shule / Jackline alijamba kwenye ofisi ya Mkuu wa Shule)

3. Break wind: Hii ni tafsida, yaani lugha ya uficho, staha, au adabu kuelezea kujamba. Inatumika kupunguza ukali wa neno ‘jamba’ katika lugha ya Kiingereza.
Mfano: My daughter broke wind in the church last week. (Binti yangu aliachia ushuzi kanisani wiki iliyopita / Binti yangu alijamba kanisani wiki iliyopita)

4. Pass gas: Hii pia ni tafsida. Nadhani inajieleza wazi kuwa ni ‘kupitisha/toa hewa/gesi’.
Mfano: If you eat that food it will cause you to pass gas. (Kama utakula chakula hicho kitakufanya utoe ushuzi / Endapo utakula chakula hicho kitakusababisha ujambe).

Kwa ufupi huo ndio msamiati unaozungumzia suala zima la ‘kujamba’ au ‘kutoa ushuzi’. Cha muhimu kwako ni kuzingatia muktadha, na kuzingatia matumizi sahihi ya tense kwenye verb conjugation.

KAMA UMEPENDA POST HII, USISAHAU ‘KUSHARE’ KWA NDUGU, JAMAA, NA MARAFIKI (TUSAIDIANE KATIKA KUELIMISHANA).
 
Jamani wabongo mbona mko ignorant kiivyo? Jamaa kaleta madini mna mwandama hakika ujinga ni janga la kwanza kitaifa🤣
 
Jamani wabongo mbona mko ignorant kiivyo? Jamaa kaleta madini mna mwandama hakika ujinga ni janga la kwanza kitaifa🤣
Hii kama ni elimu kweli basi hata akienda kuwafundisha wafungwa huko Jela au Hospitali ya Milembe,lazima watamtimua tu.
 
Kichwa Suzuki injini ya isuzu
Unaweka dp mtu kavaa graduation gown , meaning una degree au specialized function, alafu akili kama yangu ya kunywa konyagi na siwezi andika upuuzi huu.

Nyie ndio mnasemaga duniani tusifatiliane. Ila huu upuuzi. Unafikiria nini mpaka uandike hivi. Eti share na ndugu jamaa na marafiki. Ndio nyie makundi ya ukoo, michango hamtoi kazi kutuma vituko.
 
Back
Top Bottom