Kutochaguliwa waamuzi wetu kwenye mashindano ya CHAN ni uwezo mdogo ama unbeaten za mchongo?

Cashman

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2018
Posts
3,017
Reaction score
5,294
Nimepitia orodha ya waamuzi walioteuliwa kutumika kwenye mashindano hayo yanayoanza Januari,lakini sijaona mtanzania hata mmoja.

Jambo hili,halipendezi na sijui waamuzi wanalichukuliaje!

Je ninyi waamuzi hamuoni ni kwa sababu ya tamaa za wengi wenu kuibeba timu fulani ili ivunje record?Hamuoni aibu hii?

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Bahasha za mkwepa kodi zimewaponza
 
Jamii forum imevamiwa na matakataka sana siku hizi zamani ulikuwa huwezi kuukuta UHARO kama huu humu jamvini

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Jana goli la pili la Simba lilifungwa Kwa beki wa prisons kurudisha pasi fupi Kwa beki vipi mkuu mbona haujaliongelea halikuwa la tigopesa kweli? Maana kila Young Africans ikishinda huwa unafungua Uzi kusema wananunua mechi..hata goli la Boko la kichwa lile siyo la mchongo kweli? Tunaomba comment yako mkuu maana wewe huwa ni mtu wa kulaumu tu naona Leo umeamka na waamuzi
 
We jamaa haujawah kuishiwa malalamiko wakati kina Komba wanaenda Afcon mbona hatukuona Uzi wako hapa kuwapongeza?? Chuki zitakuua mzee acha wivu
 
Achana na wivu wa ,unbeaten,ila pia ni kweli Watz janja janja miingi miingi,japo pia yote haya yanaweza kuwa sio sababu,ila vigezo vingine.
 
Hao mliowapa ahadi ya milioni 30?Mliowapa kazi ya kuumiza wachezaji wa Simba?
Hii yote ni hofu ya kutojiamini ndio maana mnatumia mbinu chafu kudhoofisha wapinzani.
Naamini mnajua kilichomnyoa kanga manyoya.

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Mashabiki wa simba hawana tofauti na mwanamke mwenye mimba kila kukicha malalamiko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…