Wanabodi,
Lugha ni nyenzo kuu ya mawasiliano, na ukitaka umkamate mtu vizuri mwezeshe aifahamu lugha yako ili aione ndo lugha ya kistaarabu kuliko lugha yake, na ili kuimarisha mawasiliano na mtu unayetaka awe anakufanyia mambo unayotaka wewe ama yenye manufaa kwako, basi msingi mkuu huwa lugha ya kuwasiliana.
Siku hizi, utashangaa mtu ameenda kijijini kwao lakini anashindwa kuwasiliana na ndugu na jamaa zake wa huko kwao kwa kutokujua lugha ya kwao; anabaki akiongea Kiswahili tu. Huu si utumwa wa lugha? Tuenzi lugha zetu jamani.
Utakuta watu wamekutana wote ni Watanzania lakini lugha wanayotumia kujadiliana na tena mambo yanayohusu labda jamii yao, siyo Kiswahili. Je, huu si utumwa wa lugha?
Watu mmekutana watatu na wote ni Watanzania, salaamu zinatolewa kwa lugha nyingine na yumkini lugha yenyewe haiwezi kuongelewa kifasaha na wote hadi mwisho wa maongezi yenu. Tuache kuwa watumwa wa lugha!
Kwa nini na sisi tusiache kuzienzi lugha za wenzetu ili nao wajifunze lugha yetu nzuri ya Kiswahili?
Watu wakituhitaji na mambo yetu watalazimika kuijua lugha yetu na hawatatudanganya kwenye mambo yetu pia.
Lugha huenziwa kwa kuitumia. Tutumie lugha yetu maeneo mbali mbali.