Dotto C. Rangimoto
JF-Expert Member
- Nov 22, 2012
- 1,985
- 1,286
Watu wengi wameandika kuhusiana aidha, umuhimu/ulazima wa CHADEMA kuimarisha BRIGEDIA NYEKUNDU au hatari ya kufanya hivyo. Waliozunguzia hatari wengi wao walijitia upofu waso kuwa nao wakati wakiipitia katiba ya CHADEMA na kwa makusudi kuacha kuzingatia uwepo wa kikosi kiitwacho GREEN GUARD ndani ya CCM.

Mara kadhaa katika mikutano au maandamano ya CHADEMA kumeripotiwa kutokea matukio yenye kuhatarisha usalama wa wanaCHADEMA na viongozi wao, na mara zote polis wamekuwa wakisema wao hawahusiki kwa vurugu zote zinazotokea. Jeshi la polis ndio lenye wajibu wa kulinda usalama, lakini limeshindwa kuwalinda wananchi na mbaya zaidi wakati mwingine linahusihwa na matukio mabaya yanayotokea kwenye maandamano na mikutano ya CHADEMA.

Kutokana na ulazima na umuhimu wa usalama katika mikutano ya hadhara na maandamano ya CHADEMA, na tukizingatia kuwa jeshi la polis halina nia ya dhati ya kulinda mikutano na mihadhara ya CHADEMA, tukizingatia kuwa jeshi hilo linatuhumiwa katika kuripua bomu katika mkutano wa Arusha, na tukizingatia kuwa GREEN GUARD sasa yapewa mafunzo ya kijeshi kama vile inajiandaa kwenda vitani, hivyo basi, ni lazima na muhimu CHADEMA iimarishe BRIGEDIA NYEKUNDU na bregedia hiyo ipewe jukumu la kuwalinda viongozi wa CHADEMA kwani kuna dalili zenye uzito kuwa Dr.Slaa na Mbowe hawatakiwi japo kuinusa 2015.

Nasikitika kwa kuona kama vile mchakato wa katiba unaifanya CHADEMA kusaahu hili jambo muhimu na la lazima, tuimairishe ulinzi kwa viongozi wetu kwa kuimairisha BREGEDIA NYEKUNDU, kinyume chake sitashangaa 2015 tukawa na majina tu ya akina Dr.Slaa na Mbowe lakini wenyewe tukiwa tumeshawalaza kwa baba zao, inasemekana bomu la Arusha walilengwa viongozi, kama ndivyo na mambo kama yale yakiendelea, je, si kwamba ni rahisi zaidi kuwatabiria vifo viongozi hawa kabla ya 2015?

Serikali na CCM wanafanya kila hila kuhakikisha viongozi wa CHADEMA wanakutwa na hatia katika kesi za jinai na kufungwa hili kuwaharibia sifa kuelekea uchaguzi mkuu ujao, kwa bahati nzuri mahakama zetu bado hazijashikwa na mkono wa MAGAMBA, na kwakuwa kesi nyingi viongozi hawa hushinda na kuiachia aibu serikali na CCM yake, hivyo yawezekana wakawa na mipango ya kuwapoteza jumla hawa viongozi, bomu la Arusha laweza kuwa kielelezo hapa.

Kama serikali inadhamiria kuizuia CHADEMA kuimarisha BRIGEDIA NYEKUNDU, ni vema kwanza ikaanza kwa kulipangua jeshi la polis kwa kumuondoa kazini Wema na makamnda wote wa polis waliohusika katika kuvunja sheria za nchi hususani wakati wanakabiliana na maandamano na mikutano ya CHADEMA na iivunje kikundi cha kijeshi ndani ya CCM kinachojiita GREEN GUARD, serikali ikifanya haya ndipo itapata uhalali katika mizani ya haki na usawa katika kuitaka CHADEMA isianzishe au kuimarisha BRIGEDIA NYEKUNDU, kinyume chake ule msemo wa "mlipa mpiga zumari ndio huchagua wimbo" utaendelea kuthibiti.
View attachment 109165
Njano5.
M4C
0784845394.