Ndallo
JF-Expert Member
- Oct 1, 2010
- 7,619
- 4,299
Hapa Arusha leo ni kelele mji mzima kupitia vipaza sauti kwenye magari mawili yanayotangaza zoezi la ukusanyaji wa kutoza ushuru wa magari yanayopaki Arusha mjini pamoja na viunga vyote vya jijini hapa!
Kulikoni? nikwamba kampuni ambayo ilikua inaendelea na ukusanyaji ushuru ya Barrick Printers Parking Sistem wanatakiwa kuondoka kwenye maeneo ya ukusanyaji ushuru na kuwapisha wakusanyaji wapya wanaojiita Kilimanjaro Parking Sistem, ukipita kwenye viunga vyote vya mjini utaona wakusanya ushuru wa aina mbili kwenye hizi Uniform zao, wale ambao wanaendelea na zoezi hili wao wamevaa Jacket za rangi ya Chungwa (Barrick Printers Parking Sistem), na hawa ambao wanadai sasa ndio wanayohaki ya kutoza ushuru, wao wamevaa Jacket za rangi ya Light Blue (Kilimanjaro Parking Sistem).
Hali hii imeshawachanganya hata waendeshao magari kua kwasasa wamlipe nani? nimeuliza kutoka kwa mkusanya ushuru mmoja kulikoni? akaniambia kua kuna kesi iko mahakamani na mahakama imeshatoa amri kua hawa Barrick Printers Parking Sistem waendelee na zoezi hili la utoza ushuru, na hawa wa kampuni ya Kilimanjaro Parking Sistem nao wanadai wanahaki ya kukusanya ushuru na kibali wapepata kutoka halmashauri yaani Manispaa. Sasa basi kutokana na kelele hizi za maspika barabarani na kua kero, madereva nao wamedai zoezi hili likiendelea na wao pia watagoma kulipa ushuru kutokana na hawajui ni nani mwenye dhamana hii ya kukusanya ushuru. Haya ndio mambo Mseto kutoka jijini Arusha.