nyakahanga
JF-Expert Member
- Mar 7, 2013
- 240
- 65
Akiongea na Radio5 katika kipindi cha GOOD MORNING TANZANIA asubuhi hii kaimu mkurugenzi wa bodi ya mikopo ya elimu ya juu bwana Asanje Bangu amejibu swali la mtangazaji aliyetaka kujua ni kwa nini wanafunzi wanaoenda kufanya mafunzo kwa vitendo hawajapata pesa zao kutoka bodi hiyo. Alijibu kama ifuatavyo;
"Hii imetokana na kuchelewa kwa fedha hizo kutoka hazina, lakini hata hivyo jitihada zinaendelea kufanyika kwa kasi kubwa ili kuhakikisha kuwa mafunzo kwa vitendo yanafanyika kwa wakati na pesa zitakapopatikana haraka iwezekanavyo zifikishwe kwa wanafunzi.
Na asubuhi hii nimetoka wizara ya fedha ambapo nimeahidiwa kuwa upo uwezekano wa kupata fedha kidogo ili ziweze kupunguza ukubwa wa tatizo hili, na pia ningeomba wanafunzi wote wanaoenda mafunzo kwa vitendo wawe wavumilivu, tunajitahidi kwa kiasi kikubwa fedha zipatikane na waweze kuzipata kwa wakati na haraka iwezekanavyo"
Alipoulizwa juu ya baadhi ya vyuo kupata pesa mapema huku vyuo vikubwa vyenye wanafunzi wengi kama UDSM, UDOM na SAUT (mwanza) kaimu mkurugenzi huyo alijibu kama ifuatavyo, "Ni kweli kabisa juu ya uwepo wa suala hili, lakini hii imetokana na ukweli kwamba vyuo vyote havianzi mafunzo hayo kwa muda mmoja. Hivyo vilivyopata mapema ni vile ambavyo mafunzo kwa vitendo vimeanza mapema. Hata hivyo tunajitahidi ili hivi vingine vinavyoanza sasa viweze kupata mapema na haraka iwezekanavyo"
Kaimu mkurugenzi huyo ameongea mengi zikiwemo changamoto za upatikanaji wa fedha, n.k.
Alipoulizwa ni lini hiyo pesa kidogo aliyoahidiwa na wizara ya fedha itapatikana, amejibu kuwa kuna uwezekano ikapatikana jumatatu ijayo.
Source: ni mimi mwenyewe niliyekuwa nasikiliza Radio5 asubuhi hii na nilirekodi mazungumzo yote. Ukiihitaji nipm