Kutoka bodi ya mikopo juu ya pesa za Field, wajibu malalamiko ya kuchelewa kwa Fedha hizo

nyakahanga

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2013
Posts
240
Reaction score
65
Akiongea na Radio5 katika kipindi cha GOOD MORNING TANZANIA asubuhi hii kaimu mkurugenzi wa bodi ya mikopo ya elimu ya juu bwana Asanje Bangu amejibu swali la mtangazaji aliyetaka kujua ni kwa nini wanafunzi wanaoenda kufanya mafunzo kwa vitendo hawajapata pesa zao kutoka bodi hiyo. Alijibu kama ifuatavyo;

"Hii imetokana na kuchelewa kwa fedha hizo kutoka hazina, lakini hata hivyo jitihada zinaendelea kufanyika kwa kasi kubwa ili kuhakikisha kuwa mafunzo kwa vitendo yanafanyika kwa wakati na pesa zitakapopatikana haraka iwezekanavyo zifikishwe kwa wanafunzi.

Na asubuhi hii nimetoka wizara ya fedha ambapo nimeahidiwa kuwa upo uwezekano wa kupata fedha kidogo ili ziweze kupunguza ukubwa wa tatizo hili, na pia ningeomba wanafunzi wote wanaoenda mafunzo kwa vitendo wawe wavumilivu, tunajitahidi kwa kiasi kikubwa fedha zipatikane na waweze kuzipata kwa wakati na haraka iwezekanavyo"

Alipoulizwa juu ya baadhi ya vyuo kupata pesa mapema huku vyuo vikubwa vyenye wanafunzi wengi kama UDSM, UDOM na SAUT (mwanza) kaimu mkurugenzi huyo alijibu kama ifuatavyo, "Ni kweli kabisa juu ya uwepo wa suala hili, lakini hii imetokana na ukweli kwamba vyuo vyote havianzi mafunzo hayo kwa muda mmoja. Hivyo vilivyopata mapema ni vile ambavyo mafunzo kwa vitendo vimeanza mapema. Hata hivyo tunajitahidi ili hivi vingine vinavyoanza sasa viweze kupata mapema na haraka iwezekanavyo"

Kaimu mkurugenzi huyo ameongea mengi zikiwemo changamoto za upatikanaji wa fedha, n.k.
Alipoulizwa ni lini hiyo pesa kidogo aliyoahidiwa na wizara ya fedha itapatikana, amejibu kuwa kuna uwezekano ikapatikana jumatatu ijayo.

Source: ni mimi mwenyewe niliyekuwa nasikiliza Radio5 asubuhi hii na nilirekodi mazungumzo yote. Ukiihitaji nipm
 
Huyo mkurugenzi ni kituko, tena si kidogo...
Amesema vyuo havianzi field kwa wakati m1, inakuaje sasa hapa UDSM;SOED, UDBS, SJMC, wamepewa chao afu CoET, CoNAS, CoICT, CoHU na CoSS hawajapata...?
 
Huyo mkurugenzi ni kituko, tena si kidogo...
Amesema vyuo havianzi field kwa wakati m1, inakuaje sasa hapa UDSM;SOED, UDBS, SJMC, wamepewa chao afu CoET, CoNAS, CoICT, CoHU na CoSS hawajapata...?

mkuu unaelewa lakin ulichokiandika....au nyi ndo wasomi wa big result.
 
Hakuna idara magumashi kama bod ya mikopo.pamoja na jengo la vioo zuri bt utendajikaz wao mashaka matupo
 
usiombee utumee pesa kimakosa online rgstrtion utazungushwa mpaka ukate tamaa.kiukwel kuna watu pale wapo kimakosa.
 
Kilichonishangaza ni uongo wa huyu kaimu mkurugenzi kuwa asubuhi hiyo alikuwa anatoka wizara ya fedha na akaahidiwa pesa kidogo zipunguze tatizo. Kweli saa moja ile ofisi za wizara zilikuwa zimefunguliwa? au ndo siasa za bongo
 
mkuu unaelewa lakin ulichokiandika....au nyi ndo wasomi wa big result.


You're loosing your marbles my brother, there's time to yell and time to stay silent, as far as a still tongue makes a wise head is concerned. Then see how you've kept you feet on your mouth...
::::gloomy::::
 
FaizaFoxy unaona huyu kaimu mkurugenzi anavyodanganya umma? Sisi mjukuu wetu wa UDSM kapata hela yake tayari yeye asema bado... Halafu ombi langu hujanijibu bibie.
 
Last edited by a moderator:
Enzi zetu sisi tulikuwa hatukubali UE's zianze kabla ya pesa za field kuingia. Maana tulijua kabisa kwamba tukianza UE hakuna ushirikiano tena.
Hawa/ninyi wanafunzi wa TCU na BRN hamna mikakati kabisa ya ushindi. Hivi mnadhani bila kutunisha misuli serikali ni baba yenu? Shame on you
 
FaizaFoxy unaona huyu kaimu mkurugenzi anavyodanganya umma? Sisi mjukuu wetu wa UDSM kapata hela yake tayari yeye asema bado... Halafu ombi langu hujanijibu bibie.

Ewe punguani, hajasema kama wote hawajapata. Nijuavyo UD ambao hawajapata ni wale wenye matatizo ya usajili na wale ambao field work zao zinachelewa kuanza.

Soma unavyojisuta hapa:

"Alipoulizwa juu ya baadhi ya vyuo kupata pesa mapema" huku vyuo vikubwa vyenye wanafunzi wengi kama UDSM, UDOM na SAUT (mwanza) kaimu mkurugenzi huyo alijibu kama ifuatavyo, "Ni kweli kabisa juu ya uwepo wa suala hili, lakini hii imetokana na ukweli kwamba vyuo vyote havianzi mafunzo hayo kwa muda mmoja. Hivyo vilivyopata mapema ni vile ambavyo mafunzo kwa vitendo vimeanza mapema. Hata hivyo tunajitahidi ili hivi vingine vinavyoanza sasa viweze kupata mapema na haraka iwezekanavyo"

Sasa hapo usichokielewa ni nini? punguani wahed, ni wazi kuwa wengine wameshapata na wengine bado. Na mjukuu wangu ni katika hao waliokwisha pata na yupo ARU hapo hapo UD.
 

Hapo nimekuelewa bibi mtu, niwie radhi kwa upunguani wangu. Sasa na lile ombi langu inakuwaje?
 

Sijakuelewa hapo, nafahamu ARU ni Chuo Kikuu cha Ardhi (zamani UCLASS) kinakwaje UD tena?
 
Sijakuelewa hapo, nafahamu ARU ni Chuo Kikuu cha Ardhi (zamani UCLASS) kinakwaje UD tena?

Siyo Chuo Kikuu cha Ardhi, ni Chuo Kikuu Ardhi (Ardhi University). Waijitoa kutoka College mojawapo ya UD, na sasa ni chuo kamili
 
Siyo Chuo Kikuu cha Ardhi, ni Chuo Kikuu Ardhi (Ardhi University). Waijitoa kutoka College mojawapo ya UD, na sasa ni chuo kamili

Ahsante kwa marekebisho, nilikuwa namshangaa huyu maamuma...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…