Elections 2015 Kutoka Chuo cha Mipango, Dodoma: Mwigulu Nchemba atangaza nia kugombea Urais

yeye alikuwa ndani ya hiyo hiyo serikali iliyoshindwa yote hayo.hana jipya

hivi unadhani nani atakuwa na jipya? inawezekana kabisa ukawa unafanya kazi vizuri kwa bidii wala huli rushwa kwenye taasisi ambayo wenzio wengi ni wavivu na wala rushwa na ukawa unaumia ila huna jinsi ya kuleta mabadiliko zaidi ya kushikilia msimamo mwenyewe. Ukipata nafasi inayokuwezesha kuwa juu ya wale wavivu na wala rushwa unaweza kuleta mabadiliko. Mimi siamini kabisa kuwa mabadiliko Tz yatakuja kwa kubadilisha chama. Tabia za binadamu ni zile zile. Vyama vyote vina waungwana na washenzi ila vikipata waungwana wanaoweza kuwadhibiti washenzi mambo yanakwenda. Mchakato wa kuchuja wagombea ukiisha ndo ntajua nimpigie muungwana yupi maana aina ya chama au kuwa ndani au nje ya serikali hakumfanyi mtu kuwa na jipya au kuu kuu. Mie hata chama cha TADEA kikiwa na wagombea wazuri nadandia tu.
 
Ccm ni hatari hata akipewa nafasi ya kuongoza hawezi kufurukuta mbele ya mtandao wa watafuna nchi, ameingia kwenye rekodi but urais asahau sababu ili uwe rais wa nchi hii kupitia ccm lazima ubebwe na mafisadi kama alivyobebwa jk, na yanavyombeba el

Hilo tu ndio tatizo.
 

Akiba ya Dollah BOT wanaipata kutoka wapi !?
 
Mwigulu amefanya EL aonekane kama hakujipanga kabisa hakika asingefanya haraka maana naona kama Jana alikuwa anashangaa idadi wakati wenzake wanatoa darasa la kutosha poor EL
 
Kuna dawa serikali haina ila watu binafsi wanazo, Dr yupo sahihi wewe unaemtukana naona kikombe cha babu kinakusumbua
 
Anachekesha sana huyu. Mfumo mbovu lakini miaka yote hii amekaa kimya huku akifaidi nafasi ya juu ndani ya chama bila jitihada zozote zile za kubadili huo mfumo mbovu wa ndani ya chama. Amekuwemo ndani ya chama kwa miaka mingi sasa na na hadi kaingia Serikalini kama Naibu Waziri wa Fedha.

Miaka yote hii kimya hakutoa kauli ya kulaani mfumo mbovu hadi leo hii anapotaka kugombea urais ndio anauzungumzia mfumo mbovu ili kutuzuga Watanzania kama ilivyo kawaida ya MACCM. Mwigulu ulikuwa wapi 2005 kuzungumzia mfumo mbovu ndani ya MACCM na kuwashinikiza viongozi wa juu na wanachama kuuvunja mfumo huo na kuufanya uwe mzuri kama ambavyo wewe ungependekeza? Ulikuwa wapi 2010? Ulikuwa wapi 2012?

Hapana tumechoshwa na uongo wenu wa kukaa kimya huku nchini inaenda mrama miaka nenda miaka rudi kisha yale ambayo mnayajua kwamba ni mabaya kuja kuyazungumza pale mnapotaka kupata Urais ili mtuzuge Watanzania. Mkishaingia Ikulu speed ya kuendelea kuliangamiza Taifa inazidi kupamba moto.


 
sijaona kipya alichoongea cha kuvutia.
mipasho ilitawala pasipo utalaam wa hoja.
 
mliokaribu mmuulize utata wa jina lake, kuna taarifa humu jf kuwa yeye ni lameck madelu na hilo na mwigulu nchemba alianza kutumia baada ya kofoji vyeti vya darasa la saba.

kama alifoji vyeti vya darasa la 7 siyo yeye, ni wazazi wake labda kama alishazidi miaka 18. Yeye ni geniuos. Imagine ubongo wote ule ungeishia machungani.
 

Mfumo wa maccm wa kulindana ni vigumu sana kulikwamua hili taifa, tubadili chama waje wengine na system tofauti.
 
Duuu,haya bwana,ila mi nimeuona ni jembe sana,anafaa kuwa kiongozi wangu na namkaribisha kwa moyo wote aje kwetu Mvomero atangaze nia kwa mara nyingine,anajua sana
 
mwigulu nilikuwa sikukubali lakini hotuba yako imenigusa..umenikuna kaka...
 

Tuweke ushabiki pembeni, kati ya watangaza nia watatu kati ya jana na leo, Mwigulu Lameck Nchemba is the most bonafide genuine mgombea so far, ukimuangalia huku unamsikiliza, utaiona his genuinity kutoka moyoni mwake ku practice what he preach na kiukweli nadhani kwa kati ya hawa watangaza nia so far, naamini Mwigulu can make the best president this nation has ever had tangu mwalimu Nyerere!.

Jee wewe mwenzangu ulibahatika kumsikia, unamuonaje?!.

NB Ku make the best president ni jambo moja, mgombea anayependwa zaidi so far ni Edward Lowassa, na mgombea the most experieced so fat ni Stephen Wasira, nikichukulia mchakato wa 2005 wakati JK alipochaguliwa, kama reference, assuming hawa watatu ndio wameingia tatu bora, Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM wakipewa choice ya kuchagua between "the most loved", "the most experienced" and the "the best president", watachagua mtu anayependwa na watu, mtu atakayechagulika kwa urais na kuwatupa the rest, na hivi ndivyo JK alivyochaguliwa ile 2005 kwa sababu kwenye the finalist watatu, kulikuwa na "the most experienced" Dr. Salim, "The best Brain", Prof. Mwandosya, na "the good looking" Jakaya Kikwete, akapitishwa kwa hoja kuwa ndiye anayependwa na watu, as if mapenzi ya watu ndio uongozi wa nchi!.

JF has a role to play kuwaelimisha wananchi wetu waweze kufanya informed decisions kwenye choice of president, ili ifike mahali chaguo la mgombea wa CCM sio lazima ndio automatikally awe rais, wakituletea ule ujinga ujinga kama wa 2005, tunapiga tuu chini only if huko kungine kuna the better alternative!.

Ushauri wangu wa kwanza kwa wana JF, Mwingulu Nchemba is the man to keep watching seriously!.

NB. Kwa walionidhania mimi niko kambi fulani, uzi huu ni uthibitisho kuwa Pasco wa jf, hana chama, hana kambi, hana mtu, ila kuna watu anawakubali akiwemo yule 'jamaa yetu', hivyo sitarajii kuulizwa kama nimehama kambi kwa sababu sijawahi kuwepo kambi yoyote!.

Kiukweli mimi Pasco wa jf, nimeguswa na Mwigulu Nchemba!.

Pasco
 

Hapo kwe red, wewe kweli unaangalia mambo kwa jicho la pili mkuu. Kumbe na wewe umeng'amua janja yao eeh!
Kiukweli EL ni mtupu kichwani, najua washika remote wake wameweka pamba masikioni, lakini ukweli ni kwamba uki-rank kwa kigezo cha upstairs watia nia waliokwisha kuongea, mamvi anakuwa wa mwisho
 
kuna jamaa mmoja anataka kugombea ubunge kupitia ccm nae anatumia kauli hii "NITAWAVUSHA" nishamshtukia kumbe team mwigulu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…