Kutoka damu puani kwa mama mjamzito tatizo ni Nini... Msaada

kijana255

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2017
Posts
277
Reaction score
261
Habari wakuu, Nina rafiki yangu ambaye ni mjamzito wa miezi Kama minne saivi leo anasema ametoka damu sana puani mfululizo na nyingine pia Kutoka kwa njia ya mdomoni kidogo Msaada kwa watalamu nn Inaweza kuwa tatizo?
 
Mama mjamzito mishipa yake ya damu hutanuka na pressure ya damu inayokwenda kwenye pua huongezeka. Ni rahisi mishipa hii kupasuka. Hii ndiyo sababu mama wajawazito hutokwa na damu puani mara kwa mara.

Ikikutokea kaa chini na uso uuweke uuweke mbele ya kifua. Uupandishe uso uwe juu ya usawa wa moyo.

Ziba pua kwa vidole gumba na cha shada kwa dakika 5 ukupumulia mdomo.

Weka barafu kwenye pua na uso ukiwa juu kwa dakika 10-15.
 
Nashukuru sana sky eclat, kwa iyo sio tatizo kubwa??
 
Ntamshauri Afanye haya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…