Civilian Coin
JF-Expert Member
- Dec 2, 2012
- 2,305
- 4,380
Binafsi kama mwalimu mwenye taaluma ya ualimu, matokeo ya Mtihani wa kidato cha nne 2012 ambayo yametoka juzi yanakatisha tama kabisa kutokana na idadi ya walio feli kuwa kubwa kuliko kawaida. Mwezi jana tu matokeo ya kidato cha pili nayo watoto walivurunda sana hasa mkoa wa Dar es salaam ukiongoza kwa kuvurunda. Kwa matokeo mabovu kama haya ya kidato cha nne ni janga la Kitaifa na ingekuwa ni busara zaida kama serikali ingepandisha bendera nusu mlingoti kuashiria msiba wa kitaifa katika elimu maana vijana wengi watakosa lakufanya na malengo yao hayatatimia maana wamefeli si kwa makusudi bali kutokana na mfumo mbovu wa elimu wa nchi yetu.
Kutokana na kuwa na mfumo wa elimu mbovu ndio maana pale mwanzo nilisema tunataka Rais ajaye awe amesoma shule za kata kwani atakuwa anajua machungu ya shule hizo maana watoto wa vigogo na wabunge wanasoma international school na private school. Sioni haja ya Mawaziri kuendelea na nyazifa zao,nashauri Waziri Kawambwa na watendaji wake wajiudhuru nafasi zao na Wizara nzima ifumuliwe na kuundwa upya na ikiwezekana kuwepo na wizara mbili ya wizara ya Shule za msingi,sekondari na wizara ya elimu ya juu ili kuleta ubora wa elimu lasivyo mambo yatakuwa yaleyale.
Tukiendekeza siasa litakuwa Taifa la kujiudhuru bila mafanikio. Tusiweke maslahi ya kisiasa mbele tuangalie maslahi ya Taifa kwanza. Mitaala iboreshwe na sera ya elimu ifanyiwe ukarabati.Binafsi nimekaribia kukamilisha kuandika MSWADA WA SERA YA ELIMU TANZANIA ambao mwishoni mwa mwezi wa tatu taukabidhi kwa Rais wa nchi Mh. Jakaya Mrisho Kikwete ili kujenga uimara wa elimu yetu maana Rais ndiye atakaye kuja na majibu kutokana na mswada wangu. Katika mswada huo nimeonesha namna inavyotakiwa kupata wanafunzi kutoka Shule za misingi mpaka vyuo, namna ya uandaaji wa mitihani inayoendana na mazingira na wakati husika, namna ya walimu kuendana na mazingira husika na wakati husika katika mfumo wa elimu duniani.
Tanzania mpaka sasa Tunatumia mfumo wa Elimu ya Uingereza ambayo inawafanya watoto wakariri zaidi badala ya kuelewa, wakati mfumo wa Elimu wa Marekani ni wakumfanya mwanafunzi aelewe zaidi na si kukariri, hivyo katika Mswada pia nimezungumzia ulinganifu wa elimu ya Tanzania na Marekani na Uingereza na wapi tunatakiwa kuiga kwa muda huu ili kunusuru mfumo mbovu wa kufelisha watoto wetu.
DEOGRATIUS KISANDUMwenyekiti wa JUKWAA LA WALIMU NA WANAFUNZI-TANZANIA(Teachers and Students Forum-Tanzania).