Kutoka gazeti la raia mwema 3 March 2019 dini ilivyotumika kuwaunganisha watanganyika dhidi ya ukoloni sehemu ya kwanza: Mwanzo wa harakati 1950

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074

Raia Mwema Jumatano 3 March, 2019

Mwaka wa 1950 uongozi wa TAA ulikuwa chini ya Dr. Vedasto Kyaruzi kama Rais na Abdulwahid Sykes akiwa Katibu na ikaundwa TAA Political Subcommittee (Kamati ya Siasa ya TAA) iliyokuwa na pamoja na Rais na Katibu, wajumbe hawa wafuatao: Sheikh Hassan bin Ameir aliyekuwa Mufti wa Tanganyika, Sheikh Said Chaurembo, Hamza Mwapachu, Steven Mhando na John Rupia.

Katika kipindi hiki cha mwaka wa 1950 Abdul Sykes alikuwa katika majadiliano na Chief David Kidaha Makwaia akimtaka aingie TAA wamchague kuwa rais kisha waunde TANU yeye akiwa rais wadai uhuru wa Tanganyika.

Kwa kuwa hapa tunazungumza nafasi ya dini katika historia ya uhuru wa Tanganyika napenda kueleza kuwa Chief David Kidaha Makwaia hakuwa Muislam ingawa alikuwa mtoto wa Chief Makwaia Mohamed Mwandu.

Wakati huu Abdul Sykes alikuwa mmoja wa viongozi wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) lakini hili halikuingia katika fikra zake katika kumtaka Chief Kidaha Makwaia kuongoza harakati za kudai uhuru wa Tanganyika na uhuru ukipatikana awe Waziri Mkuu wa Kwanza wa Tanganyika.

Juhudi hizi hazikufanikiwa.

Mwaka wa 1951 Waingereza walimpa uhamisho Dr. Kyaruzi na kumpeleka Jela ya Kingolwira, Morogoro kisha wakamuhamishia Nzega.

Hamza Mwapachu yeye akahamishiwa Nansio, Ukerewe na yote hii nia ya Waingereza ilikuwa kuivunja nguvu TAA Makao Makuu, New Street kudhoofisha juhudi za kuunda chama cha siasa.

Mwaka wa 1952 Mwalimu Julius Nyerere alipelekwa kwa Abdul Sykes na Joseph Kasella Bantu.
Wakati huu Abdul Sykes alikuwa Kaimu Rais wa TAA na Katibu.



Picha hiyo hapo chini ni Chief David Kidaha Makwaia wa Siha na picha ya Abdul Sykes akiwa kwenye mavazi ya Prison Superintendent.



 
Historia zote hizi, hazina maana kwa mkitadha wa Tanzania ya leo..!

Ninachoona ni kuonesha kazi ya uislam dhidi ya Ukristo enzi za kudai uhuru..!

Ila tambua watu kama akina nyerere na wasomi wengine wamesoma shule za missionary.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bigmind,
Hapana hii ni historia ambayo kwa takriban nusu karne haikuwa inafahamika.
Kutokana na kutofahamika huko nimeona kuna mambo madogo sana lakini
yanaleta migongano isiyokuwa ya lazima na ndipo nikaona niandike makala
kuwaeleza wananchi wenzangu historia ya nchi yetu.

Usitishike kwa kuona mchango wa Waislam katika kupigania uhuru wa nchi
yetu hivyo ndivyo ilivyokuwa wala isikutie unyonge hayo yote ni changamoto
za ukoloni.

Wajerumani waliwanyonga majemedari Waislam zaidi ya 60 kwa kuwa ndiyo
walionyanyau silaha dhidi yao.

Hii ni historia isikutie hofu kuwa kwa nini iwe hivyo.
 
Asallam Aleikum
Pongezi nyingi kwako kwa kumbukumbu zuri za nchi yetu...Hakika ww ni hazina kwa historian ya Taifa

Mzee wangu wewe ni mkongwe,naomba kujua mchango wako kipindi kile cha harakati za Uhuru..je ulishiriki?

Kwa namna gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Historia haitabadilika,hata isipopendeza machoni au madikioni kwa mtu yeyote,lakini ni muhimu kufahamu ukweli wa kilichotokea mpaka leo tukawa taifa huru.
Kuumizwa na historia ni dalili ya mtindio wa ubongo(brain drain),kwanini ukimbie kivuli chako mwenyewe wakati hakina madhara?.
 
Mohamed Said ni Nabii na mtume wa kufanya Tanzania iwe rasmi Nchi ya kiislam, harakati zake kazianza mdogo mdogo. Mwanzo wa ngoma ni lele. Habari nndio hiyo
 
Heller,
Mimi nimezaliwa 1952.

Wakati TANU inaundwa nilikuwa na miaka miwili tu kwa hiyo sikushiriki katika
kupigania uhuru wa Tanganyika.
 
Mohamed Said ni Nabii na mtume wa kufanya Tanzania iwe rasmi Nchi ya kiislam, harakati zake kazianza mdogo mdogo. Mwanzo wa ngoma ni lele. Habari nndio hiyo
Bujibuji,
Unajitia hofu isiyokuwa na sababu.

Hii historia ni historia ya nchi yetu lakini kwa bahati mbaya haikuandikwa
kwa hiyo haikuwa inajulikana.

Mimi nimeiandika ili tuwe na historia ya uhuru kama mataifa mengine ya
Afrika.

Kuwa Waislam wanaonekana sana katika historia hii hatuna njia ya kufuta.

Tukifuta tutakuwa tunafuta historia yetu na tukitaka tuibadili tutakuwa sisi
tunajidanganya wenyewe.
 
Ndivyo itakiwavyo, hasa pale unapokijua kitu na wenzako hawakijui.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…