Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
KUTOKA GAZETI LA JAMVI LA HABARI: KITABU NILICHOSOMA
RAJABU KIRAMA JEMEDARI WA VITA KUWA JEMEDARI WA UISLAMU: MOHAMED SAID
Na Hafidh Kido
NIMEKUWA na utaratibu wa kufanya ziara za mara kwa mara kumtembelea mwalimu wangu Mohamed Said, lengo ni kuchota elimu ya historia na masuala mengine katika uandishi.
Mara zote nikikutana naye kwenye mazungumzo yetu huwa namdodosa maswali ya hapa na pale, nikitumia mbinu za kihabari kuchota elimu isiyoisha kwake.
Kila siku nikiondoka sikosi kuambiwa na mwalimu wangu nitafute kitabu hiki au kile cha kusoma ili kuongeza maarifa.
Wakati fulani nilipokwenda kumweleza juu ya kitabu changu kipya ‘Kanzu ya Ukubwa’ akanigusia mswada wa kitabu chake kipya cha maisha ya Jemedari wa Vita aliyesaidia kufikisha Uislamu chini ya Mlima Kilimanjaro, Mzee Rajabu Ibrahim Kirama.
Ni kitabu kidogo chenye kurasa 100 kisichochosha kusoma, kina maarifa mengi yaliyokusanywa mahala pamoja kwa umakini wa hali ya juu.
Kama ilivyo kwa mwalimu wangu Mohamed Said, maandiko yake lazima yatokane na utafiti wa kina, kila alichosema kilihusu nyaraka alizozipata kutoka kwa watoto na wajukuu wa Mzee Kirama.
Utangulizi wa kitabu umeandikwa na Profesa Issa Haji Ziddy kutoka Zanzibar, ambaye ameutendea haki utangulizi wake kwa kueleza maneno machache yenye kumaliza kila kitu kilichokusudiwa kwenye kurasa 100.
Sura ya kwanza mwandishi anatupitisha katika historia ya Wachagga, akiwaangazia sana watu wawili Mangi Ndeseruo Mamkinga aliyeongoza kabila la Wamachame Kijiji cha Nkuu kati ya mwaka 1855 hadi 1880, wa pili ni Muro Mboyo ambaye ni baba yake Kirama Mboyo ambaye baadaye ndiyo alikuja kutambulika kama Rajabu Kirama alipoupokea Uislamu kutoka Upagani.
Salim Rajabu mtoto wa kwanza wa Rajabu Kirama ndiye aliyehifadhi nyaraka ambazo mwandishi Mohamed Said alifanikiwa kuzichambua na kutuletea historia hii iliyotukuka.
Wengi tumekuwa tukishangazwa na namna Uislamu ulivyochipua katika Mkoa wa Kilimanjaro, tukisema ukiona Mchagga au Mpare ni Muislamu basi anakuwa Muislamu kweli kweli.
Nadhani hii inatokana na magumu waliyopitia babu zao kina Rajabu Kirama, waliteswa, walifungwa na kudhalilishwa na watawala wa kimila wakisaidiwa na wageni, Wajerumani na Waingereza.
Kazi kubwa ya Muro Mboyo ilikuwa ni kumlinda Mangi Ndesaruo Mamkinga, alikuwa ndiye Jemedari wa Jeshi la kabila la Wamachame.
Utaona alikuwa mtu muhimu katika historia ya Wachagga.
Baadaye ilikuja kutokea fitina kubwa ya kitawala, ambapo Muro Mboyo alitakiwa kumuua Mangi Ngamini.
Fitna ilianzia wakati Mangi Ndeseruo akiwa mgonjwa, akataka wazee wa kimila wamrithishe kiti cha umangi mtoto wake mdogo Shangali ambaye kwa wakati huo alikuwa mtoto wa miaka mitatu.
Hata hivyo, Ngamini akachukua madaraka kwa kufuata taratibu zote za kimila, lakini baadaye kilizuka kikundi kumtaka auawe.
Aliyekuwa na taarifa za kuuawawa kwa Mangi Ngamini ni Mangi Sina wa Kibosho, ambaye inaelezwa katika nyaraka hizi alilelewa na Mangi Ndesaruo tangu utotoni kisha akapewa eneo la kutawala Kibosho.
Habari za sababu za kulelewa nyumba ya Mangi Ndesaruo zipo pia kwenye kitabu hiki chenye historia kubwa ya Wachagga.
Aidha, kwa kuwa Muro Mboyo kazi yake ilikuwa kumlinda Mangi, akaona si busara kumuua atakuwa hajatimiza wajibu wake, akaamua kutoroka naye hadi Old Moshi kwa Mangi Rindi Mandara.
Hata hivyo, inaelezwa safari yao hii haikufanikiwa bali palitokea vita kubwa ya kiukoo iliyoleta uhasama wa hali ya juu, ambapo inaelezwa Mangi Ngamini aliuawawa katika vita hii. Ndipo Muro Mboyo akakimbilia uhamishoni Old Moshi.
Habari ni ndefu, kubwa na ya kusisimua; kwa mfano mwaka 1945 Sheikh Hassan bin Ameir alifanya ziara Machame, miongoni mwa matunda ya ziara hiyo ni kupelekwa walimu wanne kwenda kusomesha dini Kilimanjaro.
Waalimu hao ni Sheikh Saleh Mwamba, Shariff Alawi, Sheikh Mahmud Mshinda na Sheikh Abdallah Minhaji.
Ambapo wawili walikwenda Upareni ambao wanatajwa Sheikh Salehe Mwamba alieda Usangi na Shariff Alawi alienda Ugweno, huku Sheikh Mahmud Mshinda alienda Moshi na Sheikh Abdallah Minhaj alipelekwa Machame.
Nakushauri msomaji wangu ukitafute kitabu hiki murua, kina historia kubwa si tu katika dini ya Uislamu na Ukristo namna ulivyowasili Kilimanjaro, lakini pia kinaeleza kwa mapana yake historia ya kabila la Wachagga.
Mwisho