Kutoka kalamu ya Mohamed Ghassani: Ureno, Zanzibar na Oman

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
1548301339490.png

Ali Mahfoudh na Samora Machel baada ya ukombozi wa Msumbiji

1548301511010.png

Ali Mahfoudh, Samora Machel na Julius Nyerere wakati wa mapambano ya
kuiomboa Msumbiji, Mahfoudh anampa Nyerere taarifa za vita.

Tarehe ya leo, 23 Januari, ni siku ya kumbukumbu kubwa kwenye pwani za Bahari ya Hindi, hasa Oman na Afrika Mashariki. Siku kama hii mwaka 1650, Waomani wakiongozwa na Imam Sultan Bin Saif Al Ya'arubi walifanikiwa kuwashinda wakoloni wa Kireno na kuwafukuza kwenye ardhi na bandari zao. Wareno walikuwa wameitawala Oman kwa miaka 143, tangu mwaka 1507. Wakati huo Dola ya Ureno ilikuwa sawa na ilivyo leo Marekani kwa nguvu zake.

Umuhimu wa tukio hili ni kwamba ni baada ya hapo, ndipo iliwezekana pia kufunguka sehemu nyengine za Bahari ya Hindi kutoka utawala katili wa Wareno, ambao walikuwa wakiwachinja wenyeji na kuichoma moto miji yao. Mafanikio ya Oman yalisaidia pakubwa kumuondoa Mreno kutoka visiwa vya Unguja, Pemba, Mombasa na wakawarejesha nyuma hadi Msumbiji ya sasa. Kwa hakika, mpaka wa leo baina ya Tanzania ya sasa na Msumbiji ulichorwa na Waomani hawa walioshirikiana na wenyeji kumshinda Mreno.

Kuna mtu anaweza kuuliza kwa nini nimeiweka picha hii na wakati habari ni nyengine kabisa? Hapana. Historia ina tabia ya kuwa na vikuku vinavyoshikana kuunda mnyororo mmoja. Pichani ni marehemu wawili - kulia ni Rais Samora Machel wa Msumbiji na kushoto ni Kanali Ali Mahfoudh, mwanajeshi shupavu wa Zanzibar. Kiasili, Kanali Ali ni kutoka ukoo wa Al Maani unaochipukia Sohar, kaskazini mwa Oman. Utawala wa Kireno katika ardhi za Oman ulianzia Seeb hadi Sohar (Al Batina). Hadi leo, kama ilivyo kwa Pemba, Al Batina nako kuna mchezo wa ng'ombe ambao ulitokana na athari ya karne na nusu ya utawala wa Kireno.

Sasa vikuku vya historia vinaunganika wapi? Kanali Ali Mahfoudh, mzaliwa wa Zanzibar na mwenye pia damu ya Msumbiji, alikuja kuwa jemedari wa vita vya ukombozi wa Msumbiji dhidi ya Wareno kwa mualiko na ushirikiano wa ndugu yake Samora Machel wa Msumbiji karne kadhaa baada ya wazee wake (Waomani kutoka Zanzibar) kuongoza vita dhidi ya Mreno kwa mualiko na ushirikiano wa ndugu zao wa Pwani ya Afrika Mashariki.

Hishima aliyopewa Kanali Ali nchini Msumbiji ililingana na hishima waliyopewa wazee wake karne kadhaa nyuma. Kuna wakati masultani wa Msumbiji walikuwa hawamruhusu mtu kuingia katika ngome zao isipokuwa Waomani kutoka Zanzibar na wakubwa zao walikuwa wakivaa vilemba vyekundu ambavyo walipewa na masultani wa Zanzibar.

Watu wa Bahari ya Hindi, hasa baina ya mashariki mwa Afrika na Oman wana mafungamano ya karne kadhaa na kila unapochimba kuvikata vikuku hivi vya kihistoria ndivyo unavyokuta vimeungana zaidi.
 
View attachment 1003248
Ali Mahfoudh na Samora Machel baada ya ukombozi wa Msumbiji

View attachment 1003249

Hakika Yale mavamizi na mapinduaji ya 1964,Mungu atajua cha kuyafanya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom