Kutoka Karimjee: Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Linawapiga Msasa Wahariri Kutoka Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF)

Kutoka Karimjee: Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Linawapiga Msasa Wahariri Kutoka Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF)

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Niko hapa ukumbi wa Karimjee, nikiwaletea live, kikao kazi cha Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, NEEC, na wahariri wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, TEF. kuhusiana na mambo ya uwezeshaji wananchi kiuchumi.

Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) ni Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa na Sheria ya 16 ya 2004 kama njia ya kuharakisha mchakato wa kuwawezesha Watanzania kiuchumi. Baraza ina majukumu ya kuwezesha kubuni, kupanga, kusimamia, kufuatilia na kutathmini na pia kuratibu shughuli zote za uwezeshaji wa kiuchumi nchini. Pia inajukumu la kuhamasisha rasilimali na kusimamia fedha maalum kwa ajili ya shughuli za uwezeshaji wa kiuchumi. Uwezeshaji wa Kiuchumi ni moja ya njia ya kufikia MKUKUTA, MDG na hatimaye ndoto ya kitaifa ya mwaka 2025.

Tangu uhuru, Tanzania imejaribu kutengeneza na kupitisha sera kadhaa na mikakati ambayo inalenga kuendeleza Taifa na kuwawezesha watu wake kushiriki katika usimamizi wa uchumi wao. Sera na mikakati hiyo ni pamoja na Azimio la Arusha, Ungatuaji wa majukumu ya serikali kwa kupeleka madaraka mikoani,Biashara Huria, na Ubinafsishaji wa Makampuni ya Serikali. Ingawa sera hizi hazikufikia kikamilifu malengo yaliyokusudiwa, hata hivyo ilikuwa ni chachu ya kuleta maendeleo, amani, utulivu na umoja ambao ni mali kubwa kwa maendeleo ya kiuchumi.

Watumiaji wakuu wa huduma zetu ni makundi ya watu binafsi, vyama na vyama vya ushirika wanaohusika katika shughuli mbalimbali za kiuchumi; utafiti na taasisi za kitaaluma; na idara za serikali. NEEC inahamasisha rasilimali kutoka ndani na nje ya nchi na tunakaribisha washirika wenye nia ya kujiunga na jitihada zetu katika kufikia maono yenye heshima ya kuwawezesha Watanzania.

Dira na Dhima​

Dira​

Kuhakikisha kwamba sehemu kubwa ya Uchumi wa Nchi inamilikiwa na Watanzania wenyewe.

Dhima​

Kuongoza, kuwezesha na kuratibu shughuli za uwezeshaji kiuchumi Tanzania.

Malengo​

  • Kuongeza uzingatiaji katika kutekeleza masuala mtambuka katika shughuli za uwezeshaji wa kiuchumi.
  • Kuwezesha maendeleo ya fursa za uwezeshaji wa kiuchumi na kuziunganisha na walengwa.
  • Kuratibu mikakati ya kisekta katika ushirikishwaji wa Wananchi katika miradi ya kimkakati na uwekezaji na uwezeshaji wa kiuchumi na kufungua fursa za kiuchumi.
  • Kuongeza uelewa wa umma juu ya jukumu la NEEC katika kuratibu mipango ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi nchini Tanzania.
  • Kuimarisha uwezo wa NEEC katika kuratibu michakato ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi.

Maadili ya Msingi ya Baraza​

  • Uwajibikaji
  • Ubunifu
  • Uadilifu
  • Inayozingatia mahitaji ya watu
  • Kufanya kazi kwa umoja
  • Ushirikiano
  • Uwazi
  • Iliyojielekeza katika matokeo

Majukumu​

  1. Kuwapatia Watanzania fursa za kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi;
  2. Kuandaa Mpango Mkakati wa sekta na kisekta na kuhamasisha matumizi ya rasilimali kwa shughuli za Uwezeshaji wa Wananchi;
  3. Kuhamasisha na kuhimiza uwekaji wa akiba, uwekezaji, na ushirikishwaji makini wa Wananchi kwenye shughuli za Kiuchumi;
  4. Kuandaa Mkakati wa kitaifa Uraghibishi wa sekta mbalimbali wa shughuli za uwezeshaji wananchi kiuchumi;
  5. Kuendeleza na kuwezesha shughuli za kibiashara zilizoanzishwa na kuendeshwa na watanzania;
  6. Kuainisha fursa za mafunzo ya kiuchumi na uwekezaji na kuratbu programu za mafunzo hayo;
  7. Kusimamia, kuongoza na kutafuta vyanzo vya fedha kwa ajili ya Mfuko wa Uwezeshaji;
  8. Kuhamasisha utafiti wa shughuli za kiuchumi na kuhimiza ushirikiano na Taasisi za utafiti;
  9. Kufanya mapitio ya sheria mbalimbali kwa lengo la kutoa mapendekezo ambayo yatalenga kuboresha mazingira ya uwezeshaji wananchi kiuchumi;
  10. Kuandaa mfumo wa kufuatilia maendeleo ya shughuli za kiuchumi na kutathimini matokeo; na mfumo wa menejimenti ya habari za uwezeshaji;
  11. Kushauri kwenye shughuli zote za uanzishaji wa vikundi, ushirika, ushirikiano na ushirikiano wa biashara wa muda mfupi;
  12. Kuanzisha mfumo wa utoaji taarifa za uwezeshaji wa wananchi kiuchumi kutoka sekta zote.
1729736146967.png

BARAZA LA TAIFA LA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI (NEEC)​

Beng’I Issa Katibu Mtendaji
Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC)
Mkutano wa Wahariri,22 Oktoba 2024

Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi
National Economic Empowerment Council (NEEC)
Baraza lilianzishwa mnamo 2004

Baraza kisheria liko chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, ambapo sheria namba 16 ilipitishwa na Bunge mwaka 2004

Ni chombo cha juu cha kutoa uongozi kwa
ajili ya Uwezeshaji wa kiuchumi

Baraza lina dhamana ya kupanga, kuratibu, kuwezesha, kufuatilia na kusimamia utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ambapo utekelezaji wake unafanywa na sekta zote.
KAZI ZA BARAZA
Kuratibu shughuli za uwezeshaji nchini
Kuonesha na kutoa fursa za ushiriki wa watanzania kiuchumi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali na Kuwaunganisha watanzania na fursa hizo
Kuandaa Mikakati, Miongozo na program za Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi.
Kuwezesha vikundi, biashara za ndani na ubia katika shughuli za kiuchumi kwa kushirikiana na wadau
Kuishauri serikali, sekta za umma, sekta binafsi kuhusu kuendeleza uwezeshaji kiuchumi Tanzania.

Sera ya Uwezeshaji, 2004​

Kifungu na 2.1 cha Sera kinaelezea hali halisi ya Ushiriki wa Wananchi katika shughuli za uchumi wa sasa ni duni​
Mfumo wa kodi, sheria, kanuni, leseni na huduma za serikali

Mitaji Miundombinu ya kiuchumi

Ubinafsishaji
Kukuza ujuzi, uzoefu, elimu, mila na desturi zenye mtazamo wa kimaendeleo
Masoko
Matumizi ya ardhi kwa uchumi
Ushirika
Uwekezaji

MFUMO WA URATIBU
Sekta za kiuchumi zote zina waratibu wa Uwezeshaji
Wizara
Mikoa
Halmashauri
Taasisi
Jumla Baraza lina Waratibu 276

MUUNDO WA URATIBU WA SERA​

Mkutano wa mwaka wa Uwezeshaji wananchi kiuchumi (WM)
Kamati ya ushauri ya uwezeshaji wananchi kiuchumi (KM OWM)
Mifuko ya Uwezeshaji
Vikundi vya kiuchumi
Ushiriki wa Watanzania Local Content
Ujasiriamali Utafiti
Uratibu - sekta ya umma

Local Content
Local Content ni thamani ya ziada inayochangiwa kwenye uchumi wa taifa kupitia ushiriki wa wananchi kutokana na uwekezaji kwenye nchi husika.
Inaweza kuwa kuongeza thamani (value addition) au kuongeza umiliki wa wananchi (ownership)

Uwekezaji wowote wa Serikali. Kwa fedha za nje au fedha za ndani.​

BIASHARA ZA NDANI – iliyosajiliwa hapa Tanzania, yenye kumilikiwa na watanzania kwa 51% na kuongozwa na watanzania kwa 51%.
BIDHAA NA HUDUMA ZA NDANI – Bidhaa na huduma zilizozalishwa hapa Tanzania
Maeneo muhimu kwa Tanzania Ajira Ushiriki wa kampuni na bidhaa za ndani Mafunzo, teknolojia na tafiti Uwekezaji wa kiuchumi kwenye jamii

Thamani ya ziada inayoletwa nchini​

NEEC 2024 9
Utekelezaji
NEEC haitekelezi Local Content moja kwa moja.

Huduma kwa kushirikiana na Taasisi zinazo simamia miradi hufanya kazi na m.f. TANESCO, TRL, Tume ya Madini, TANROAD, TAA, EWURA, PURA n.k.

Kila Taasisi ina Mratibu wa
Local Content;

Taasisi zinahakikisha mkandarasi anawasilisha mpango wa Local Content

Kutayarisha taarifa ya kitaifa ya
Local Content.

Ajira 262,96na Makampuni 3,360
UJASIRIAMALI
Kuweka mwelekeo wa ujasiriamali nchini ili watanzania wengi zaidi wafaidike na ujasiriamali
Kupima na kufuatilia mwelekeo
wa ujasirimali nchini
Kusimamia Kamati ya kitaifa ya kusimamia na kuongoza ujasiriamali nchini
Kuratibu watoa huduma za uendelezaji biashara (BDSPs) Kuandaa Mwongozo

……UJASIRIAMALI

VITUO VYA UENDELEZAJI
BIASHARA
Kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB)
Kuandaa Mwongozo
Kutoa mafunzo kwa watoa huduma za Uendelezaji biashara

Vituo vya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi

Vilianzishwa mwaka 2018
Vinatoa huduma za:
Mafunzo
Urasimishaji wa biashara
Mikopo
Kuongeza thamani ya mazao
Uanzishaji wa vikundi
Sasa hivi kuna jumla ya vituo 25

⦁ Wananchi 11,852
⦁ Mikopo bn 19.9 imetolewa

Mikoa Yenye VituoDSM, Tanga,
Katavi
Dodoma-7Singida
Geita - 2RukwaMikoa
inayomalizia
Kigoma-6PwaniNjombe
Shinyanga-3MorogoroRuvuma
⦁ Jumla ya kampuni 1,906
⦁ Ushauri kwa wananchi 8,826
⦁ mafunzo yametolewa kwa wananchi 11,893
VIKUNDI VYA KIFEDHA
Serikali imetengeneza Sera na Sheria ya huduma ndogo za fedha 2017
Kifungu 33 cha sheria;
NEEC kwa kushirikiana na BOT wanatoa elimu ya fedha,
kuchunga maslahi ya walaji,
kuunganisha vikundi na programu mbalimbali za Serikali.
NEEC ilianza kulea VICOBA mwaka 2011
Mpaka May 2024 vimesajiliwa vikundi (CMG) 49,376.

URATIBU WA MIFUKO YA UWEZESHAJI

Kutunza Daftari la Orodha ya Mifuko na programu;

Kuelimisha Umma kuhusu Mifuko/Programu za Uwezeshaji na jinsi ya kunufaika;
Kuratibu vikao vya Taasisi za Mifuko na Programu Kupokea taarifa za Mifuko na kuandaa taarifa ya nchi; Kuwaunganisha wananchi na Mifuko ya Uwezeshaji; na
Kufanya ufuatiliaji na tathmini ya huduma na matokeo ya Uwezeshaji.

….MIFUKO YA UWEZESHAJI

Na.Kundi la MifukoIdadi ya MifukoUwiano wa Kundi la Mifuko (%)
1Mifuko inayotoa mikopo
17
23
2Mifuko inayotoa Dhamana
11
15
3Mifuko inayotoa Ruzuku
35
48
4Programu za uwezeshaji
10
14
JUMLA
73
100
24 October 2024 16

MPANGO WA VIWANDA WA SANVN

Viwanda vidogo na vya kati
Mikopo ya kuanzia shilingi Milioni 8 hadi Milioni 50 kwa viwanda vidogo na shs Milioni 51 hadi Milioni 500 kwa viwanda vya kati.
Mikopo ya uwekezaji (Investments loan) na uendeshaji wa miradi (Working Capital loan)

Mpaka sasa Jumla ya viwanda 86 kwenye Mikoa 13 na Mikopo ya Shs 6.7 bilioni imetolewa.

Mpango Unaoendeshwa SIDO, BENKI YA AZANIA, NEEC, VETA na NSSF
Ulianza 2020

IMARISHA UCHUMI NA MAMA SAMIA (IMASA)

Ni Programu ya Uwezeshaji kwa Mikoa yote 26 ya Tanzania Bara na 5 Zanziba kwa kushirikiana na ZEEA
Walengwa ni Wanawake, Vijana, Wazee na watu wenye ulemavu.
Program hii itatekelezwa kwa miaka 5 kuanzia Mwaka huu.

LENGO LA PROGRAM

Kuibua Vipaumbele vya kiuchumi kwa kila Mkoa;

Vipaumbela viwe vile vitakavyoleta matokeo makubwa kwa watu wengi;
Wananchi ambao tayari wana shughuli waboreshe shughuli zao za kiuchumi;
Kuziba Mapengo kati ya program zote za Uwezeshaji ambazo zimeanzishwa na Serikali;

Awamu za utekelezaji

AWAMU YA KWANZAUandaaji wa kanzi data ya walengwa/wanufaika wa programu (Utambuzi wa shughuli za kiuchumi za wadau na mahitaji maalum ya uwezeshaji)
AWAMU YA PILIUandaaji wa Program maalum za Uwezeshaji Kiuchumi kwa Wanawake, Vijana na watu wenye mahitaji maalum kulingana na mahitaji yaliyoonekana katika uchakataji wa takwimu na kuanza utekelezaji wake.

Muundo wa Utekelezaji wa
Programu

OFISI ZA WAKUU WA MIKOA
OR-TAMISEMI
Kuhusisha Programu ya IMASA na programu zote za uwezesahji zinazoendelea hivi sasa

WANAWAKE, VIJANA, WAZEE NA WENYE ULEMAVU
– (m.f. Mikopo 10%, Mifuko yote ya uwezeshaji, 30% Manunuzi ya Umma, BBT, Nishati safi, Ruzuku ya mbolea, vituo vya uwezeshaji wananchi kiuchumi, n.k.)

Kuhakikisha programu hii inajielekeza kwenye maeneo yatakayofikia watu wengi zaidi.

WADAU

…….IMARISHA UCHUMI NA MAMA SAMIA

Mikoa 24 Imefikiwa
Watu 92,533 Wameshajisajili (21/10/2024) Wanawake zaidi ya 65%
Vipaumbele: Kuongeza thamani ya mazao, Fursa katika viwanda, Maghala, Masoko ya Nje ya Nchi, Maeneo ya kufanyia biashara (Masoko, Super markets), n.k.

na upatikanaji wa taarifa.
Wananchi wengi wanahitaji ujuzi wa teknolojia

Manunuzi ya Umma Kwa Makundi Maalum

Serikali inatekeleza Sera ya manunuzi ya umma kwa makundi maalum.
Mpango maalum unatengenezwa kwa ajili ya kujenga uwezo wa makundi haya.

MAJUKWAA YA UWEZESHAJI WANAWAKE KIUCHUMI

NEEC inashirikiana na Wizara ya Jinsia kutekeleza dhana ya majukwaa.
NEEC inaratibu shughuli za uwezeshaji katika Majukwaa kulingana na Sera ya Taifa ya Uwezeshaji
Jumla ya Majukwaa 35,304 yameanzishwa (Jan. 2024)
Majukwaa yameanzisha; Makampuni (Shinyanga na Pwani); SACCOSS (Dodoma na Mwanza); Kisekta (DSM na Songwe); Usindikaji, n.k.

Paskali.
 
Attachments

Nini tofauti yake na TIC?
TIC ni kituo cha uwekezaji Tanzania, kutangaza vivutio na fursa za uwekezaji ili kuvutia wawekezaji kuja kuwekeza Tanzania, yaani investiment, to invest in Tanzania. Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, ni kuwawezesha wananchi kiuchumini, hapa ni empowerment, to empower Tanzanians.
P
 
Wanabodi,
Niko hapa ukumbi wa Karimjee, nikiwaletea live, kikao kazi cha Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, NEEC, na wahariri wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, TEF. kuhusiana na mambo ya uwezeshaji wananchi kiuchumi.

Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) ni Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa na Sheria ya 16 ya 2004 kama njia ya kuharakisha mchakato wa kuwawezesha Watanzania kiuchumi. Baraza ina majukumu ya kuwezesha kubuni, kupanga, kusimamia, kufuatilia na kutathmini na pia kuratibu shughuli zote za uwezeshaji wa kiuchumi nchini. Pia inajukumu la kuhamasisha rasilimali na kusimamia fedha maalum kwa ajili ya shughuli za uwezeshaji wa kiuchumi. Uwezeshaji wa Kiuchumi ni moja ya njia ya kufikia MKUKUTA, MDG na hatimaye ndoto ya kitaifa ya mwaka 2025.

Tangu uhuru, Tanzania imejaribu kutengeneza na kupitisha sera kadhaa na mikakati ambayo inalenga kuendeleza Taifa na kuwawezesha watu wake kushiriki katika usimamizi wa uchumi wao. Sera na mikakati hiyo ni pamoja na Azimio la Arusha, Ungatuaji wa majukumu ya serikali kwa kupeleka madaraka mikoani,Biashara Huria, na Ubinafsishaji wa Makampuni ya Serikali. Ingawa sera hizi hazikufikia kikamilifu malengo yaliyokusudiwa, hata hivyo ilikuwa ni chachu ya kuleta maendeleo, amani, utulivu na umoja ambao ni mali kubwa kwa maendeleo ya kiuchumi.

Watumiaji wakuu wa huduma zetu ni makundi ya watu binafsi, vyama na vyama vya ushirika wanaohusika katika shughuli mbalimbali za kiuchumi; utafiti na taasisi za kitaaluma; na idara za serikali.
NEEC inahamasisha rasilimali kutoka ndani na nje ya nchi na tunakaribisha washirika wenye nia ya kujiunga na jitihada zetu katika kufikia maono yenye heshima ya kuwawezesha Watanzania.

Dira na Dhima​

Dira​

Kuhakikisha kwamba sehemu kubwa ya Uchumi wa Nchi inamilikiwa na Watanzania wenyewe.

Dhima​

Kuongoza, kuwezesha na kuratibu shughuli za uwezeshaji kiuchumi Tanzania.

Malengo​

  • Kuongeza uzingatiaji katika kutekeleza masuala mtambuka katika shughuli za uwezeshaji wa kiuchumi.
  • Kuwezesha maendeleo ya fursa za uwezeshaji wa kiuchumi na kuziunganisha na walengwa.
  • Kuratibu mikakati ya kisekta katika ushirikishwaji wa Wananchi katika miradi ya kimkakati na uwekezaji na uwezeshaji wa kiuchumi na kufungua fursa za kiuchumi.
  • Kuongeza uelewa wa umma juu ya jukumu la NEEC katika kuratibu mipango ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi nchini Tanzania.
  • Kuimarisha uwezo wa NEEC katika kuratibu michakato ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi.

Maadili ya Msingi ya Baraza​

  • Uwajibikaji
  • Ubunifu
  • Uadilifu
  • Inayozingatia mahitaji ya watu
  • Kufanya kazi kwa umoja
  • Ushirikiano
  • Uwazi
  • Iliyojielekeza katika matokeo

Majukumu​

  1. Kuwapatia Watanzania fursa za kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi;
  2. Kuandaa Mpango Mkakati wa sekta na kisekta na kuhamasisha matumizi ya rasilimali kwa shughuli za Uwezeshaji wa Wananchi;
  3. Kuhamasisha na kuhimiza uwekaji wa akiba, uwekezaji, na ushirikishwaji makini wa Wananchi kwenye shughuli za Kiuchumi;
  4. Kuandaa Mkakati wa kitaifa Uraghibishi wa sekta mbalimbali wa shughuli za uwezeshaji wananchi kiuchumi;
  5. Kuendeleza na kuwezesha shughuli za kibiashara zilizoanzishwa na kuendeshwa na watanzania;
  6. Kuainisha fursa za mafunzo ya kiuchumi na uwekezaji na kuratbu programu za mafunzo hayo;
  7. Kusimamia, kuongoza na kutafuta vyanzo vya fedha kwa ajili ya Mfuko wa Uwezeshaji;
  8. Kuhamasisha utafiti wa shughuli za kiuchumi na kuhimiza ushirikiano na Taasisi za utafiti;
  9. Kufanya mapitio ya sheria mbalimbali kwa lengo la kutoa mapendekezo ambayo yatalenga kuboresha mazingira ya uwezeshaji wananchi kiuchumi;
  10. Kuandaa mfumo wa kufuatilia maendeleo ya shughuli za kiuchumi na kutathimini matokeo; na mfumo wa menejimenti ya habari za uwezeshaji;
  11. Kushauri kwenye shughuli zote za uanzishaji wa vikundi, ushirika, ushirikiano na ushirikiano wa biashara wa muda mfupi;
  12. Kuanzisha mfumo wa utoaji taarifa za uwezeshaji wa wananchi kiuchumi kutoka sekta zote.
Karibuni.

Paskali.
Hao NEEC wanadharau sana mimi niliwatembelea walipokuja Morogoro mhusika mkuu hakutaka kunisikiliza mawazo yangu aliyenisikiliza alikili yule ambaye hakutaka kukusikiliza angelipata kitu kutoka kwako

They Lack something which I have the unlocking codes,

Ni organization, ambayo haina watu wengi, na niligundua hilo nilipo watembelea kwenye banda lao Morogoro, wana mipango mizuri ambayo hawawezi kuifanikisha, they do not have the tools, (hawana nyenzo), may be that is a kind way of explaining them
 
Hao NEEC wanadharau sana mimi niliwatembelea walipokuja Morogoro mhusika mkuu hakutaka kunisikiliza mawazo yangu aliyenisikiliza alikili yule ambaye hakutaka kukusikiliza angelipata kitu kutoka kwako
Tuko nae hapa, na atakusoma, ila sio vibaya ukakisema hicho ambacho hakukusikiliza ili akisikie na tukusikie.
P
 
Tuko nae hapa, na atakusoma, ila sio vibaya ukakisema hicho ambacho hakukusikiliza ili akisikie na tukusikie.
P
Asilimia 80 ya mafanikio kwenye biashara yanategemea mjasiriamali na asilimia 20 ni mjasiriamali na yanayomzunguka, (the entrepreneur and his her environments).

Mimi nimegundua kwamba asilimia 20 ina nguvu hata kuua biashara, kuna mambo makuu ma nne yaliyojificha 1. Maamuzi ya kisiasa ambayo yanaweza kusababisha biashara zikue ama kufa. 2 National economy and social development strategies of an existing government, (Serikali iliyoko madarakani ilivyo jipanga kuinua kipato cha mtu mmoja mmoja, 3. Social demographic variables, (aina ya watu, elimu zao wanao zunguka biashara), 4. Technology not necessarily new, (kuwa tayari kupokea mabadiliko ya teknolojia), neno la kisasa linaitwa sasisha

Lakini haya bado hayawezi kufanikiwa kwenye jamii ya kanyaga twende ambayo haitambui mawazo chanya na hasi

Jamii ambayo haiwezi kubuni namna ya kukabiliana na changamoto zilizopo na zitakazo kuja.

The society which is not able to create methods that will overcome uncertainty or use tested methods

Hapa siwezi kusema yote nina andiko langu linalo husu uncertainty ,(changamoto), changamoto husababishwa na 1. Disasters,( majanga)
2.information-media
3. Binadamu

Kwakifupi changamoto nyingi tulizonazo zinasababishwa na binadamu, binadamu anaweza kujisababishia changamoto kwa uzembe uvivu ujinga na ushamba, pia binadamu ana weza wasababishia wengine changamoto kwa makusudi ama kwa kutokujua
 
Back
Top Bottom