Kutoka Kigoma: Elimu ya uzazi wa mpango yaendelea kutolewa

WLF Tanzania

Member
Joined
Oct 9, 2014
Posts
38
Reaction score
22
Wadau,

Elimu ya uzazi wa mpango bado haijamfikia kila mtu, kuna jitihada za makusudi zinazofanyika na watu binafsi, mashirika pamoja na serikali ili kuendelea kueneza elimu hii.

WLF kupitia kampeni ya Thamini Uhai nayo haipo nyuma, wahamasishaji jamii kutoka Kigoma wanatuhabarisha jinsi harakati za kufikisha ujumbe kwa umma zinavyoendelea.

Mhamasishaji jamii, Upendo Reuben, ametuma picha hii ya wanafunzi wa Sekondari ya Katabuka, manispaa ya Kigoma wakisikiliza elimu ya uzazi wa mpango.


Mfanyakazi wa afya, Jockdan, anatuhabarisha kuhusu elimu ya uzazi wa mpango unaofanywa kituo cha afya Kimwanya kwa njia ya picha.


Mhamasishaji jamii kutoka Wilaya ya Kibondo, mkoani Kigoma, Benjamin, ametuma picha hii ya familia yenye watoto wengi wanaotunzwa na Bibi (wa pili kushoto). Bibi ameomba watoa huduma waongeze bidii kutoa elimu ya uzazi wa mpango.



Hayo yanatoka Kigoma, upande wako mambo yakoje? Elimu ya Uzazi wa Mpango inapenya vilivyo au inachelewa?

Karibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…