Uchaguzi 2020 Kutoka kwa Mgombea Urais wa DP: Ahadi za chama cha Democratic Party kikishinda Uchaguzi 2020

Uchaguzi 2020 Kutoka kwa Mgombea Urais wa DP: Ahadi za chama cha Democratic Party kikishinda Uchaguzi 2020

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Kilimo:
Chama hicho kinachoshiriki Uchaguzi Mkuu kikiwakilishwa na Mgombea wa Urais Philipo Fumbo kimeahidi kuweka trekta kila kijiji ambalo litakuwa chini ya ofisi ya Afisa Mtendaji

Matrekta hayo yatakodishwa kwa wakulima kwa shilingi 30,000 kwa kila eka huku gharama zilizobaki zikilipwa na Serikali

Aidha, wameahidi kutatua matatizo ya wakulima kwa kutoa pembejeo mapema

Elimu:
Wanaahidi elimu bure nchini Tanzania. DP imesema Tanzania inadaiwa kuwa na elimu bure lakini wazazi hususani masikini bado wanataabika kulipia gharama mbalimbali.

Endapo DP itaongoza Serikali, wanaahidi elimu kuwa bure ikiwemo vifaa mbalimbali kama madaftari, sare za shule na hata usafiri.

Vilevile, DP inasisitiza kuwa watoto wa kike watakaopata ujauzito shuleni watajifungua na kisha kurudi shuleni (ikiwemo za Serikali) kwa sababu Elimu ni haki yao ya msingi.

Katiba:
DP inaahidi kuwapa Watanzania hitaji lao la mida mrefu ambalo ni Katiba Mpya. Wanataraji kufanya hili kwa kuendeleza mchakato wa Katiba Mpya ulioanzishwa na Rais Kikwete kwa kuendelea pale Tume ya Jaji Warioba ilipoishia.

Kwa ufupi, DP inakubaliana na Rasimu ya Warioba haswa suala la Serikali 3. DP haina mpango wa kuvunja Muungano.

Mila, Desturi na Tamaduni:
DP inaahidi kutochukua misaada ama mikopo kutoka kwa wahisani mabeberu wenye masharti yanayotishia mila zetu.

Wanatamba kuwa chama pekee chenye mila Tanzania.

Kuhusu kutoeleweka wazi kwa mila, desturi na maadili ya Watanzania wanaahidi kuanzisha mchakato Bungeni wa kujadili mambo hayo na kuyafanyia documentation ili kuwe na sehemu ya reference kila yanapotajwa.

Uhuru wa Kujieleza na Haki nyingine za Kiraia:

DP inaahidi kudumisha Uhuru wa Kujieleza, Uhuru wa kupashana habari na pia Uhuru wa Kuandamana ambavyo wanadai vipo kwa sasa ila havipo wazi.

Uchumi na Uwekezaji:
DP itakaribisha wawekezaji wa pande zote lakini katika uwekezaji wowote ni lazima mzawa ahusike

Kila alipo mwekezaji lazima mzawa awe na asilimia kadhaa aidha ana fedha au hana.

Serikali itawajibika kumkopesha mzawa mwenye vigezo fedha ili aweze kuwa na ushiriki katika miradi.

DP inakubaliana na sera ya Viwanda ya Serikali ya awamu ya 5 ingawa wao watahakiksha wazawa wanapewa priority kwenye mchakato mzima.

Pia watahakikisha Mkoa wa Kigoma unapata kiwanda cha kuchakata mafuta kwani hivi sasa Chikichi inalimwa Kigoma lakini kiwanda cha Korie kiko Mwanza.

Sera ya magabachori:
Sera hii iliyoshikiliwa vilivyo na muasisi wa DP, Hayati Christopher Mtikila, bado ina nafasi kubwa kwa DP kwani wanaamini Magabachori yapo ila wamekuja kivingine na sasa wanaitwa mafisadi na wanaweza kuwa hata weusi.

Wanaahidi kupambana na mafisadi kwa kuendeleza juhudi za Magufuli ambaye wanadai amechoka mbio hizo hadi kufikia kiwango cha kutamka hadharani kuwa amechoka.

Mafisadi watakaohukumiwa watafilisiwa na mali zao kutaifishwa. Wanaahidi kuwadhibiti hata wakiwa huru.

Miundombinu:
DP haifurahishwi na hatua za ujenzi wa miundombinu zilizofanywa na Serikali ya CCM mpaka sasa.

Wanaeleza kuwa flyover mbili tati sio kitu cha kujivunia miaka 60 ya uhuru. Ni aibu.

Sera inasema mtandao wa barabara za mikoani utaunganishwa kiwango cha lami lakini Katavi, Geita, Kigoma bado hazijaungabishwa.

Afya:
Vijiji vingi havina zahanati na hata mabox ya huduma ya kwanza.

Mfano: Kutoka kijiji cha Katete hadi Mwakazega ni umbali wa Kilomita 32 na ndiko huduma za afya zilipo. Je, wajawazito wataweza himili umbali au ndio tumekubali tu kama nchi wao wapate shida?

Sayansi na Teknolojia:
Vijana wengi vyuma vimekaza kwa sababu vyuo vya ufundi mfano VETA viko mijini kwenye makao makuu ya mikoa. Endapo wataingia madarakani, DP itahakikisha vinakuwepo kwenye tarafa na hata kata ili kuhakikisha vijana wanapata ujuzi wa kujiajiri.

Je, wanakubaliana na Sera ya Mikoa au Majimbo?
DP inasimama kwenye Sera ya Mikoa na si Majimbo kwani inaamini Majimbo yatagawa umoja wa Watanzania. Pia kuna makabila yenye nguvu kuliko mengine hivyo kuna uwezekano wa wengine kumezwa ndani ya majimbo.
 
Huyo Mgombea ni kama alisema yeye akiwa rais wiki kwanza tu atanunua ndege 50[emoji23][emoji23][emoji23]
 
na unajua wazi huwezi kukanyaga ikulu ndio maana unaongea ujinga
 
Back
Top Bottom