Kutoka Loliondo: Tazama na sikiliza kwa umakini

Kutoka Loliondo: Tazama na sikiliza kwa umakini

sikua nafahamu hali ni mbaya kiasi hiki mpaka nilipotizama video hizi.watoto wanalala na ng'ombe na mbuzi kwa kuwa tu tunakumbatia wawekezaji?haya bana
 
Kwa kweli hili jambo linasikitisha, linahuzunisha na kukatisha tamaa kiasi cha kutosha. Ni lini mtanzania atapata haki ndani ya nchi yake? ni wapi serikali inayoitwa ya watu inapopata madaraka kiasi hiki yasiyotoka kwa watu wenyewe? tunahitaji kurudi nyuma na kujiuliza mara nyingi!

Yalitokea hivi hivi kule mara, na team ya Jaji Kisanga ili yaona haya, lakini serikali imeendelea kurudia yale yale!

Je, watu watanzania wasaidiwe vipi kupata haki yao ndani ya nchi yao? Haitoshi tu kuchangiana katika harusi, ila kwa mambo mazito na ya msingi kama haya!
 
Unapoweka pesa mbele kuliko vitu vingine - that's what you get.
 
Ni lini mtanzania atapata haki ndani ya nchi yake?
Hii nchi imeshatekwa na kikundi kidogo cha watu ambao nao, kwa bahati mbaya sana, ni mawakala wa mabwana wakubwa huko nje. Yanahotajika mapambano mengine ya kuikomboa nchi kutoka katika makucha ya ukoloni mamboleo
 
Kuna haja ya hii kitu kuipeleka Al-Jaazira, BBC, SKYNEWS, CNN, nk. Kuna siku hawa watu watatunguliwa kwenye ndege zao kama Rais wa Rwanda. Kuna haja hizi video kuja kutembezwa mwakani Tanzania nzima ili hao wanaokumbatia hawa MAFISADI waone wanakumbatia......

Ningeliweza basi ningelimtumia hadi Barack Obama, Clinton, Al Gore, Mahakama ya Human Right, jamaa wa haki za binadamu wa Helsinki.......
 
Yaani PINDA kweli Mizengwe. Yeye kila kitu hafahamu na wala hana nguvu. Ukweli unabaki mmoja tu kuwa kama PM hana nguvu nayo, basi hii kitu imetoka juu zaidi na hata niseme NJE kabisa ya Tanzania kuna mtu kashika Remote control.
 
This is so disgusting, shameful to our society and government.

Haya ni mambo ya kipumbavu tu, ndiyo nimesema kipumbavu. How comes serikali unaweza kufanya vituko vya namna hiyo kwa raia wako kisa kulinda ufisadiz wenu kwa huyo mwarabu.

It's time for all Tanzanians to stand up for the rights of all people. Tusinyanyaswe hivi, this is our country, land.
 
Kikwete alipoingia alikuwa tumaini la walio wengi.

Imani imeshuka kwako. Uzalendo umekushinda. Shabaha ya uhuru umeipoteza!

Dhumuni la kuwakataa mabepari, wanyonyaji, mabeberu na majina mengi enzi hizo tuliwaita. Nyie mmewapa majina mazuri eti wawekezaji.

Wakowapi wakina ananilea nkya, watu wa haki za binadamu mliopiga kelele wakati police wapo choma nyumba na na kuamrishwa kubaka wanawake, mimba nyingi zilitoka na wanaume kuuwawa kisirisiri, kisa muarabu beberu muwekezaji,

Raisi kikwete hata kama mkataba alisaini raisi Mwinyi omba msaada tunao wanasheria wengi wanaouwezo wa kuokoa ndugu zetu.

Hii nchi ni ya watanzania sio ya CCM, watu wenye matumbo makubwa na kushibisha kakundi ka watu.

Jamani nchii hii tunakwenda wapi?? Kwani wale viongozi wa rwanda waliotunguliwa wakafa wote mnawashinda nini? Au kwasababu mnamiliki Jeshi? Hivi jeshi la tanzania na jeshi la Libya jeshi lipi linanguvu? Hivi kikwete na Gadafi ni nani ananguvu jeshini?? Hivi kikwete na Gadafi nani rahisi kung'onlewa? Kama gadafi katoka basi Tanzania tuko mbioni.

Mungu ibariki Africa Mungu ibariki Tanzania. Naomba kuwakilisha
 
Kikwete alipoingia alikuwa tumaini la walio wengi.

Imani imeshuka kwako. Uzalendo umekushinda. Shabaha ya uhuru umeipoteza!

Dhumuni la kuwakataa mabepari, wanyonyaji, mabeberu na majina mengi enzi hizo tuliwaita. Nyie mmewapa majina mazuri eti wawekezaji.

Wakowapi wakina ananilea nkya, watu wa haki za binadamu mliopiga kelele wakati police wapo choma nyumba na na kuamrishwa kubaka wanawake, mimba nyingi zilitoka na wanaume kuuwawa kisirisiri, kisa muarabu beberu muwekezaji,

Raisi kikwete hata kama mkataba alisaini raisi Mwinyi omba msaada tunao wanasheria wengi wanaouwezo wa kuokoa ndugu zetu.

Hii nchi ni ya watanzania sio ya CCM, watu wenye matumbo makubwa na kushibisha kakundi ka watu.

Jamani nchii hii tunakwenda wapi?? Kwani wale viongozi wa rwanda waliotunguliwa wakafa wote mnawashinda nini? Au kwasababu mnamiliki Jeshi? Hivi jeshi la tanzania na jeshi la Libya jeshi lipi linanguvu? Hivi kikwete na Gadafi ni nani ananguvu jeshini?? Hivi kikwete na Gadafi nani rahisi kung'onlewa? Kama gadafi katoka basi Tanzania tuko mbioni.

Mungu ibariki Africa Mungu ibariki Tanzania. Naomba kuwakilisha

Maneno yako, yamenifanya nitokwe na machozi....kilichobaki ni kuchapana tu! Kweli tena.
 
Kukaa kimya kwa vyombo husika kunatia shaka tukio zima. Ni bora hili jambo likawekwa wazi na hatua za haraka zichukuliwe. Wananchi hao hawatasahau madhila waliofanyiwa ambayo ni kinyume na haki za binadamu.
 
Kwa kumbukumbu zangu, mgogoro wa Loliondo ni wa siku nyingi.

Pori tengefu hili liliuzwa enzi za utawala wa mzee Ruksa. Kama mnakumbuka vizuri, kulikuwa na mgogoro fulani wakati wa kuwahamisha wakaazi wa eneo hilo miaka ya mwanzo ya '90, enzi hizo Mrema akiwa waziri wa mambo ya ndani.

Mrema aliwajibu kejeli sana hao wakazi wa Loliondo, walipokuwa wakilalamikia kuhamishwa katika ardhi ya mababu zao kwa nguvu bila utu! Laana hii itatafuna vizazi vyao! Uonevu huo umenisikitisha sana
 
Ukitaka kufahamu maana ya ubepari na western civilization (christian or rather supported by christians) ndio hiyo

Kunyan'anya mali za watu..
 
Ukitaka kufahamu maana ya ubepari na western civilization (christian or rather supported by christians) ndio hiyo

Kunyan'anya mali za watu..
Lakini cha ajabu aliyewapa hao Waarabu eneo hilo la ardhi ni Sheikh Ali Hassan Mwinyi, ambaye ni Muislamu. Na wanaofanya udhalimu huo ni hao Waarabu rafiki zake Mwinyi.
 
Natafuta zile picha za Waarabu wa Loliondo. Hapa nimepata video zinazoongelea hali ya huko.
 
hivi mbunge wa eneo hilo ni nani? iko haja ya wabunge wote wa Arusha na Manyara kushirikiana na kuona mali zao hazi chukuliwe kwa kigezo cha serekali kuwa na haki zaidi kuliko hao raia walio iweka hiyo serikali madarakani.
 
Nakumbuka wakati wa Mwl kwa sababu ya kuelewa haki za wa masai aliweka waziri wa utalii Solomon Ole Saibul, sijui yuko wapi yule baba au umri ndio ulisha mtupa mkono.

Iko haja ya kuweka waziri mwingine wa utalii toka huko, na deputy ndio atoke Singida/Shy/Serengeti? Wenye kupata dhahama ya hawa wawekezaji.
 
Eee MUNGU,kumbuka yanayotupata sisi,angalia, uone fedheha yetu: urithi wetu umechukuliwa na wageni; nyumba zetu zimekuwa mali za wasimcha MUNGU:tumekuwa yatima,tumefiwa na baba na mama zetu wamegeuka wajane, maombolezo 5:1....

Hivi kwanini watawala mnatuchanganya!? mmetutoa kwenye gas , mkatupeleka kwenye kwenya mabucha ya nyama na sasa mnataka kutunyan'ganya aridhi hivi ni lini mtachoka tukunyanyasa?

Mnasikia raha gani kula dhahabu ya damu?

Hivi hizi hela ambazo mnabadilishana na wageni kwa kuwa tayari watu wamwage damu yao na wauwawe ni kwa faida ya nani?
uwekezaji wenu umemsaidia nani zaidi ya watoto wenu ,vimada wenu, marafiki zenu na makuadi zenu? Hivi mnataka twende wapi?

Kila tunapojaribu nyinyi mnatudhurumu. Hivi kweli mnauza nchi yetu na kuwatesa wengine kwa ajiri ya rushwa?
ubinafsi utatufikisha wapi?

Tumewachagua viongozi watutetee lakini wamegeuka wanafiki kwa kugeuza ukweli kwa kuwa uwongo. Kweli tunauza nchi kwa pichi la mchele utatufaa nini kwa watu millioni 44 ikiwa pishi lenyewe wala wachache?

Tuoneeni huruma, tumekubali mlichotudhurumu basi tuachieni maisha yetu tuendeshe maisha yetu kwani tunateseka mno!
lakini, naamini MUNGU yupo na atashuka na nguvu zake atawaadhibu kwa kadri ya stahili yao.

Mimi najiuliza kunasababu gani ya kukusanya fedha ambazo hazina thamani ya kazi uliyostahili kulipwa ambayo huwezi kuitumia kwafuraha wewe na kizazi chako?

Tuwape kiasi gani muweze kuyalinda maisha yetu kwani tumejitoa sana lakini bado hamridhiki!

Kwa kujitoa kwetu imesababisha tukose elimu, hospitali, chakula na kwa kweli hata watoto wetu hawajui tena wimbo wa mahitaji muhimu ya mwanadamu tuliokuwa tukuelewa sote.....semeni tuwape nini watawala wetu mridhike ili mtuachie nchi yetu angalau watoto wa wajukuu zetu siku moja waweze kufika na kutembea loliondo wakiwa kama nchini kwao.

Kama mtan'gan'gania tuambieni kipi kitafuata ili tujue kwakukipmbilia kama kupo japo nafikiri madini mliochukua ndiyo makaburi yatakayo tumika kutuzikia ili mpate level mjenge hotel za kitalii kwa kuwa udongo hautatosha.

Inatia hasira mno mwili wangu hauonyeshi machozi lakini nafsi yangu inalia mno!

MUNGU Sikia kilio cha watu wako wantugawa kila siku ili watudhurumu.
 
Back
Top Bottom