[FONT=Verdana, Arial]
Author[/FONT] [FONT=Verdana, Arial]
Topic: Tuimarishe Lugha Yetu ya Kiswahili[/FONT] [FONT=Verdana, Arial]
Kishoka[/FONT]
[FONT=Verdana, Arial]
Member[/FONT]
[FONT=Verdana, Arial]
[FONT=Verdana, Arial]posted 10-10-1999 20:13
[/FONT]Webmaster na Waungwana,
Napenda kutoa hoja.
Kiswahili, lugha yetu kuu wana wa Tanzania na watu wa Afrika Mashariki ni lugha ambayo imetufanya tuonewe wivu na watu wengi duniani hasa Barani Afrika.
Ukichukulia kwa msingi kuwa tuna zaidi ya makabila 130(ethnic gruops) na wote tumeunganishwa na kuwa wamoja kwa kutumia lugha hiii marudufu. Amani, utulivu na mshikamano wa watanzania umetokana na lugha hii ambayo katika miaka 100 ijayo kuna hatari kuwa inaweza kuwa Lugha kuu Afrika, na kwa Jamii za watanzania lugha za asili zinaweza kusahaul;ika.
Kwa sasa hivi takwimu zinasema kuna wazungumzaji kiswahili zaidi ya milioni 60 duniani, na kiswahili kimekuwa ni lugha ya mawasiliano tu.
Changamoto ninayotoa kwenu enyi wana bodi ni kwamba ni Lini tutakapokiimarisha kiswahili na kukifanya kiwe lugha kuu katika matumizi yetu ya kila siku kuanzia nyumbani, mashuleni, makazini hata katika ngwe na viwanja vya kimataifa?
Nia yangu ya kusema hivyo ni kuwa katika jamii zote nilizowahii kuishi nazo(kimataifa) kila jamii inajigamba kwa kuwa na lugha kuu inayotumika katika nchi yao na hawaoni soni(aibu) kutumia lugha yao. Kwa bahati mbaya sana na labda huu ni ugonjwa mbaya, watanzania tunashindwa kujivunia lugha yetu na tunakimbilia kutukuza lugha za wageni.
Nitatoa mfano mmoja ambao ni mkubwa. Imekuwa ni kawaida yetu kumcheka mtanzania ambaye haongei kiingereza vizuri au haongei kiingereza kabisa na na tumefikia hatua ya kuwaita hao ndugu zetu washamba, wakuja au hawajasoma na kuwacheka. Kuongea na kutumia kiingereza kumetufanya kujenga matabaka ya walioendelea(wasomi) na wasioendelea. Na hii inatupeleka pabaya kwa sababu ya kudharau lugha na utamaduni wetu na kukimbilia lugha za kigeni.
Natumaini wengi wetu tumewahi kutembelea sehemu mbalimbali duniani na tumeona jinsi inavyotubidi kujifunza lugha zao na mara nyingine ni vigumu kupata mtu anayezungumza kiingereza.
Wenzetu wote ukiondoa waafrika, wanatumia lugha zao kwa ajili ya mawasiliano yao ya kila siku na lugha zao zinatumika katika kufundishia masomo katika ngazi zote kuanzia shule za msingi mpaka vyuo vikuu.
Ukiangalia kwa makini nchi hizi zimepiga hatua kimaendeleo katika nyanja zote za biashara, kiuchumi, sayansi na teknolojia kwa sababu moja kuu. Elimu inayotolewa katika nchi hizi ni katika lugha wanayoilelewa na waliyokuwa nayo. Mfano China, Japan, Russia, Norway, Brazil nk.
Kiingereza, Kifaransa au lugha yeyote ile ya kigeni zimefundishwa kama lugha za ziada na hazijatumika katika kufundishia masomo mengine. Masomo mengine yetu iwe ni hesabu, fizikia, historia, uchumi,udaktari nk, yamefundishwa kwa lugha zao za asili.
Kwa kufanya hivyo idadi ya watu walioenda shule na kufaulu katika nyanja mbalimbali imeongezeka kwa ajili ya kutumia lugha wanayoifahamu vizuri katika kujielimisha.
Hii imesaidia sana katika maendeleo ya taifa lolote lile hata kama taifa hilo ni bado masikini, lakini kunatoa nafasi kubwa ya kupiga hatua kimaendeleo. wengi wetu bado hatukielewi vizuri kiingereza na hata waalimu wengi katika shule za msing na sekondari bado hawajaweza kumudu kiingereza vizuri.
Je waungwana manonaje basi tukikifanya kiaswahili kitumike katika kufundishia masomo yote ukiachia kiingereza chenyewe?
Je ule mpango wa serikali ulioanza miaka ya themanini ya kubadilisha mfumo wetu wa elimu na kufanya Kiswahili kiwe lugha kuu ya kufundishia(kutoa elimu) umefikia wapi? Napenda kutoa hoja [/FONT]