Kutoka maktaba za kijeshi

Naamini kuna mengi sana kuhusu huyu Kambona ila siri imekuwa kubwa kuhusu yeye.!
 
..Kambona ana mambo mazuri, na madhaifu, kama binadamu wengine.

..nadhani hili la ku-negotiate na kufanya juhudi za kutuliza maasi ya 1964 ni baadhi ya mazuri ambayo Kambona aliitendea nchi yake.
 
 
..mwandishi anadai maasi yaliongozwa na Kavana na Colonel.Hingi.

..siyo kweli.

..aliyeongoza maasi alikuwa ni Sajini.Francis Hingo Ilogi.

..Elisha Kavana alikamatwa na waasi na kulazimishwa kuwa Mkuu wa Majeshi. Na waasi walimpachika cheo cha Brigedia.

..moja ya madai ya waasi yalikuwa kupandishwa vyeo jeshini, na kuondolewa kwa maafisa wa Kiingereza akiwemo aliyekuwa mkuu wa majeshi.

..Uthibitisho kwamba Elisha Kavana hakuhusika na jaribio hilo ni uteuzi wake kuwa Chief of Staff wa jeshi lililoundwa na Mwalimu baada ya mapinduzi.

..Mwalimu aliunda JWTZ na kumteua Mirisho Sarakikya kuwa CDF akiwa na cheo cha Brigedia. Elisha Kavana aliteuliwa kuwa Chief of Staff akiwa na cheo cha Major.
 
Nimesoma waraka wako kuhusu maasi ya KAR 1964, ila umekosea ile sehemu ambayo unasema kuwa moja ya sababu ya uasi huo ni pale vijana wa TANU (TANU Youth League) walipounganishwa jeshi bila kuwa na taaluma za ulinzi za kutosha.
Ukweli ni kwamba kuanzia 1961 hadi maafa yanatokea, vijana wa tanu hawakushirikishwa kabisa na jeshi na ukweli sura ya jeshi letu haikubadilika sana ukiondoa wale vijana [kina kashmir] kwa wakati huo ambao wengine walikuwa mafunzoni nje na baadhi yao walikuwa wamesha rudi. Tatizo lilikuwa ni wazungu ndani ya jeshi ambao walikuwa na privilege nyingi kuliko askari wa kawaida na kipindi kile kuli kuwa na mbiu ya 'Africanisation' ambapo sehemu kubwa serikalini ilianza na mabadiliko hayo[ila jeshini yalikuwa pole pole kutokana na aina ya weledi uliokuwa ukihitajika kwenye vyeo vya juu.
Baada ya jaribio hilo ndipo pale vijana wa tanu walianza kuingizwa jeshini na masomo ya siasa jeshini pia yalianzishwa ili kuhimiza uzalendo kwenye ulinzi wa nchi.
 
..hapa kuna habari ya waliohusika na maasi ya1964 kuhukumiwa.

..mwendesha mashtaka wa serekali ya Tanganyika alikuwa Herbert Chitepo.

..Chitepo alikuwa akitokea Southern Rhodesia, sasa hivi Zimbabwe.

..Pia alikuja kuongoza chama cha ukombozi cha Zimbabwe, ZANU.

..Herbert Chitepo aliuwawa. Na nafasi yake ikachukuliwa na Robert Gabriel Mugabe.

Tanganyika Imprisons 14 For Role in Army Mutiny
 
Tafadhali naomba mnifahamishe, Kabila la Wajinga linapatikana Mkoa gani?
 
Haukuwepo na mimi sikuwepo. Bila shaka umesoma mahali kama mimi. Weka chanzo chako cha taarifa na mimi nikupe vyanzo vya taarifa.
Maandiko ya historia ya Tanzania yapo mengi, lakini hasa kwa lugha za kigeni (kiingereza na kijerumani). Waandishi wengi wanaotafsiri kiswahili wanakosea, nina ushahidi na jambo hilo. Ni vema inatafuta original document au vitabu au majarida ya wakati huo, sio kusoma makala za waandishi wa magazeti ya leo.
 
Sikuandika makala hii kutoka kwenye kichwa changu. Nimekusanya nyaraka za wakati huo, kuzichambua na kuzitafsiri zile zilizokuwa kwa lugha ya kigeni.
 
Kwahiyo jeshi liki asi,polisi wanakazi kubwa ya kupambana na waasi.
 

..hebu tuwekee hicho chanzo kinachosema mwaka 1964 alikuwa askari wa Tanganyika Rifles akiitwa Mrisho Sarakikya na siyo Mirisho Sarakikya.

..kwa nia njema kabisa nakushauri ukafanye utafiti wako ukiwa umetulia. Kuwa makini na vyanzo vyako.

..Hili ni tukio muhimu ktk historia ya nchi yetu unapaswa kulitendea haki kwa kutoa taarifa zilizo sahihi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…