Kutoka moyoni bila unafiki, Magufuli bado yupo vichwani mwa Watanzania

Kutoka moyoni bila unafiki, Magufuli bado yupo vichwani mwa Watanzania

Mzee wa old school

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2021
Posts
873
Reaction score
1,405
Habari wana jamvi,

Kiukweli nimevumilia nimejikaza lakini nimehemewa acha niseme ukweli tu.

Mzee baba Magu Watz mpaka sasa wanaumia na nimeliona hili kila Mara katika Moshe zangu na safari za hapa na pale. Afu sasa cha kushangaza mpaka watoto, cha ajabu wakisikia mazungumzo yanayo muhusu wengine mpaka wanataka walie.

Mfano tu mzuri Leo nipo kwenye usafiri wa Masafa marefu naingia ndani nakuta mjadala watu wanaongea kwa machungu sana.. Basi tu ishatokea hakuna namna Mungu ashukuriwe kwa maisha yake hapa Duniani.

Ila kiukweli bila unafiki Mzee baba alikuwa mzalendo sana na anamachungu na taifa ingawa kuna wapingaji. Wanapinga huku mioyo inawasuta.
 
Wanafiki sana Watanzania wanaongea tu ila hakuna ushirikiano miongoni mwetu wengi ni waongeaji
Ushirikiano gani watoe. Kwa kipindi chake wengi RAIA wakawaida sana walimpa ushirikiano, sema tu kuna wapayukaji wachache mitandaoni wanaenesha watz hawakumpa ushirikiano. Lakini ki uhalisia ushirikiano ulikuwepo
 
Tofautisha watanzania baina ya hawa:

"Awamu ya sita imerithi kundi kubwa la wajinga na - the brainwashed to be catered for. Lenye mtizamo hasi katika elimu, sayansi na teknolojia."

Kama walivyo ainishwa wazi wa,i kwenye uzi huu:

Madhara ya Awamu ya Tano yanayofumbiwa Macho
Ndugu, hakuna kiongozi aliye kamilika, maana kuwa kiongozi haiondoi ubinadamu wako, ukweli ni kwamba genge LA wahuni wa chache wachumia tumbo watunga uongo ama wanatumia mapungufu take machache kuyakuza lakini kiukweli jamaa kapiga kazi kubwa ambayo haina mfano.

Pia kwenye maswala sayansi na techonologia. Hivi kwani Afrika hatuwezi kujitegemea na sayansi yetu na techologia yetu? Ni dhambi kubwa sana?

Uko brain washed ndugu, hebu kuwa mzalendo kwanza. Na ukiwa mzalendo utajali nchi yako kwa namna yeyote ile maana MTU akijaribu kuharibu mambo lazima ushughulikiwe ipasavyo. Ndivyo ilivyo.
 
Nenda ukachanje usione soo.

Yaani tukumbuke WASIOJULIKANA ?!.

Au tukumbuke kupotezana ?!

Ama kuvuruga mfumo mzima wa democracy ndiyo tumkumbuke?!

Hivi angefanya maendeleo bila kuumiza wenye mawazo tofauti angelipoteza nini? Mkumbuke wewe au nenda kabisa Chato ukahiji.
Ndugu, hivi mfano unajenga nyumba, afu ndugu yako kwa kutafuta misifa anabomoa, ili ukamilishe ujenzi wako utachukua hatua gani?
Ni kwamba, lazima umshughulikie ipasavyo ili ashindwe kuja tena kubomoa.
 
Ndugu, hivi mfano unajenga nyumba, afu ndugu yako kwa kutafuta misifa anabomoa, ili ukamilishe ujenzi wako utachukua hatua gani?
Ni kwamba, lazima umshughulikie ipasavyo ili ashindwe kuja tena kubomoa.
Ndiyo maana kukawa na sheria. Siyo uhayawani wa kujichukulia sheria mikononi!! Mshtaki wewe. Mwendesha mashitaka wewe. Jaji wewe !! One man show

Mfano alichofanyiwa Alphonse Mawazo. Eti kwa kuwa mkoa wa bwana mkubwa upinzani hautakiwi mtu anacharangwa mashoka kama nyama buchani?!

Uzuri Mungu ni fundi. Hajawahi kuitupa Tanzania
 
Back
Top Bottom