Shujaa Mwendazake
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 4,016
- 6,759
Jana nilimshuhudia Bernard Morrison akivua bukta yake baada ya ushindi na kubakiwa na gguo ya ndani.
Hilo suala la kusherehekea ubingwa kwa staili hiyo si la ajabu machoni mwangu hivyo hata kimjadala halikunistua sana. Kwa haiba ya mchezaji mwenyewe pia halikuwa la ajabu , wengi tunamjua BM23 mambo yake na vituko vyake,"mzee wa kukera".
Leo katika fukunyuafukunyua zangu baada ya hilo suala kuanza kuleta minong`ono nikakutana na kitu kimoja ambacho TFF walishafanya.
Mjadala ulikuwa ni suala alilofanya BM23 nlipo vipi kisheria hapa nchini.
Nilipoenda mbali zaidi nikakutana na adhabu aliyopewa Mwinyi Zahera baada ya kuvaa kaptula uwanjani huko nyuma.
Sasa nimebaki najiuliza itakuwaje kwa mkali BM23 kwa sababu Mwinyi Zahera alikuwa anapenda kuvaa pensi akiwa kocha wa Yanga,kanuni ikatumika,lengo kulinda maadili. Tusubiri tuone nini kitafuata.
Sitaki kuamini kuwa TFF wtakuwa na "Double Standards" , na kama wakimuacha najua watakuja na ufafanuzi mzuri.
t.co
Kazi na iendeleee.

Dewji: Siungi mkono Morrison kuvua bukta
Mfadhili wa zamani wa Simba Azzim Dewji amesema hakufurahishwa na kitendo kilichofanywa na winga wa timu hiyo Bernard Morrison alipoamua kuvua kaptula yake. Morrison mara baada ya Simba kuibuka...
Kazi na iendeleee.