Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
KUTOKA PHOTO ALBUM YENYE UMRI WA MIAKA 50
Asubuhi na baridi ni kali sana.
Huenda ni haya mabadiliko ya tabia nchi.
Lakini kwa kawida Dar es Salaam haijapata kuwa na baridi kali kama hii mwezi kama huu wa August.
Nimekaa Maktaba.
Jicho likenda kwenye furushi la makabrasha, magazeti ya kale na korokoro nyingine nyingi.
Katikati ya furushi hili nikaona album ya picha imechomoza.
Nikajiuliza mna nini mle?
Nimekuta picha mbili za zamani sana zina umri wa miaka 50 na picha zote hizi nimezikata kutoka gazetini.
Picha ya kwanza inaonyesha "cabin crew"wa East African Airways (EAA) waliohitimu mafunzo yao Nairobi mwaka wa 1970.
Katika hao mmoja alikuwa "school mate,'' tumesoma sote St. Joseph's Convent umri wetu miaka 16.
Picha hii ilichapwa katika Tanganyika Standard.
Bahati mbaya sana sikuandika tarehe ingawa nakumbuka mwaka.
Picha ya pili ni ya Dome Okochi Budohi ambayo sikumbuki niliikata kutoka gazeti gani la Kenya.
Dome Okochi Budohi historia yake nimezieleza mara nyingi.
Dome Budohi Mluya kutoka Kenya kadi yake ya TANU ni no. 6.
Dome Budohi alikamatwa mwaka wa 1955 kwa tuhuma ya kuwa Mau Mau akarejeshwa Kenya na kufungwa kisiwani Lamu.
Dome alipata kuniambia kuwa baada ya uhuru wa Kenya na Tanganyika kila Nyerere alipokuwa Nairobi alijitahidi sana akutanenae lakini kwa bahati mbaya ujumbe aliokuwa akimpelekea Nyerere haukujibiwa.
Wazalendo hawa wawili waliokuwa pamoja katika uongozi wa TAA baada ya uchaguzi wa 1953 na kuwa wanachama wa mwanzo wa TANU hawakupata kukutana.
Historia ya TANU ina mengi yasiyofahamika.