Choddi
Member
- Jul 27, 2018
- 94
- 188
PEP GUARDIOLA NA MZIMU WA YAYA TOURE,UEFA CHAMPIONS LEAGUE
------------------------------------------------------------------------------
Hadithi inanza mwaka 2008 wakati Pep Guardiola
alipoteuliwa kuwa kocha mkuu wa timu ya Barcelona.Wakati huo Yaya Toure akiwa ni mmoja wa wachezaji tegemezi katika kikosi cha Barcelona panga pangua lazima Yaya Toure aanze.Msimu wa 2008/2009 Barcelona wakashinda mataji sita na kuweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kushinda mataji yote ndani ya msimu mmoja.Toure akiwa kikosi cha kwanza.
Ghafla msimu wa 2009/2010 mambo yakaanza kubadilika,Toure akaanza kukaa benchi ni baada ya Pep kuanza kuwapa nafasi vijana wadogo kutoka La Masia kina Sergio Busquets.Maisha ya Yaya Toure yakawa magumu ilipofika mwezi July 2010 Toure akaamua kuhamia Manchester City kwa ada ya £24m.Wakala wa Toure bwana Dimitri Seluks akamtupia lawama Guardiola kuwa ni mbaguzi amefanyia uhuni na ubaguzi mteja wake.
Maisha ya Yaya Toure pale Manchester City yakawa mazuri mpira ukakubali,Toure akawa star wa team akiwa pamoja na kina Sergio Aguero,Dzenko,Vincent Kampony,Balloteli na David silva wakaunda timu tishio ikiwemo kubeba mara tatu ubingwa wa Ligi kuu Wuingereza na kombe la FA mwaka 2011.Yaya Toure akawa mfalme pale Etihad.Toure akawa kama dhahabu pale Uingereza.
Mungu si Athumani kama wahenga walivyo sema Milima haikutani ila binadamu ukutana.Mwaka 2018 Guardiola akateuliwa kuwa kocha mkuu pale Manchester City.Dunia nzima ikaanza kubashiri nini kinaweza kutokea ukizingatia historia ya Yaya na Guardiola.Maisha ya Yaya Toure yakaanza kuwa magumubaada ya Pep kuanza kazi dakika za kucheza zikaanza kupungua,Toure akaachwa kwenye kikosi cha Manchester City kilicho shiriki michuano ya UEFA msimu wa 2018/2019.Dunia ikaanza kuhoji ila Pep akajibu ili Yaya acheze ni lazima wakala wake bwana Seluks aombe radhi kwa zile kauli zake dhidi ya Guardiola.Seluks akagoma mwisho mwaka 2020 ikamlazimu Toure kuhamia Olympiaco.
Wakala wa Yaya Toure akatoa lawama na shutuma kwa Guardiola juu ya mteja wake,akajiapiza na kwambia Guardiola kupitia yombo vya Habari.
"NA UHAKIKA FRICA NA ASILI YAKE KAMWE HAITOKUJA KUKURUHUSU USHINDE KOMBE LA UEFA.HII ITAKUWA KAMA LAANA YA WAAFRICA DHIDI YAKO.WAKATI UTAJIBU MBELENI"
Tangu mwaka 2018 Manchester City wamecheza Nusu fainali tatu UEFA CHAMPIONS mara zote walitolewa.Mwaka 2020 walifika nusu fainali wanatolewa na mabishoo wa Paris PSG.Tena mwaka 2021 wakafanikiwa kufika fainali napo wakafungwa na Chelsea moja bila.
Usiku wa jana mei 4 2022 wamefungwa na kutolewa na Real Madrid katika Hatua ya Nusu fainali pale Santiago Benabeu.
Popote alipo bwana Seluks Dimitri ni wazi yupo anakunywa mvinyo wa Paris huku akiwa na tabasamu bashabasha.Maneno yake bado yanaishi na uenda yakaendelea kuishi.Ni wakati wa Pep Guardiola kuchagua kuiishi historia kiume huku amesimama au aombe radhi ili aione tena pepo ya ubingwa wa ligi ya mabingwa ulaya (UEFA CHAMPIONS).Nadhani wakati utatujibia hiki kitendawili zaidi.
Mwananchi
Nehu jr