Kutoka shajara yangu ya 1991: Abdulrahman Babu na Ahmed Rajab

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
FzDLMpD0Z1PbSNcpFQmSqqXMAkezmRiRitkc0yvp85mLvkvujPA4VApS-Vk1HnK_MLwXCzP959o1OyIIYvqOOfejdvljki9cWehMjA1OahK4sGxJoe3zRfTYRDWuQiNVq80eETmyxDJmQXdVW-xvbrusNwPSZE2_xNFouYveCWMh19XNjBk63IGZrlCIhVusx1YTpsiB-l0Gtcir6fLXT97KwdQMIvDKeEey5FNr6gLrYIfbCfqC6rjreoJNtzp8M3tfjFGoAl_7RD9v9_D7bEJRiyr__KMvUgo6--b6rvPCmIhhAbygcrJ445MFnKGrWZrvsg1ot33V2FAEb5S-Ur20FJ6o-iLZ6hHRwqHzXVNtGQNah3-ZtRhedoeJ2egqRevvA2yId2cHuXbTR1YKlMXijFyBz-sKFg03t134YkZ3ZCP9yNgGxS7R34uDnyjIH23FshOO9fTdqA0h0ABIkpfd9aF_14OFgA4Nu2xAaCU4-Li2hpAvOThU6wmM-ZlkV03XlJLolofhwmVN6HTBovkSnoAz04fkgFa4EIt_k1Wn-TsJ6GAsYomB3TkOrVSaspinT34plKhgA3psIKp6JkOlCDsy-B9rm3cSG5kN4_HGeX6et6YfGg=w965-h692-no

Leo alfajir nilikuwa napitia maktaba yangu nikakumbana na shajara
(diary) yangu ya 1991.

Hapo juu ni ukurasa wa tarehe 9 May. Huyo niliyemtaja kama, ‘’Ahmed,’’
ni Ahmed Rajab wakati ule alikuwa mhariri wa jarida, ''Africa Analysis,’’
na huyo, ‘’Babu,’’ ni Abdulrahman Babu, kwa ufupi wa maneno mkimbizi
wa siasa kutoka Zanzibar.

''Mlamali,'' ni Mohamed Mlamali Adam wakati ule Mhariri wa Africa Events.
Kumweleza Mlamali utahitaji kitabu kizima.

Mlamali ana kalamu sijapatapo kushuhudia lakini kubwa ni ujuzi wake wa
lugha ya Kiingereza.

Watu wengi hawamjui Mlamali.
Babu na Ahmed Rajab hawa ni watu mashuhuri hawahitaji kutambulishwa.

Tuko London.

Siku hiyo wakongwe hawa wa siasa za Afrika walinichukua kwenye mkutano
wa "Africa Alert," Brixton kitongoji cha watu weusi nje ya London.

Wapinzani Cameron walikuwa wamegombana lakini wote wamekuja Uingereza
kutafuta hifadhi kama wakimbizi wa siasa.

Babu na watu wengine maarufu waliokuwa wakiishi London na wao pia wengi
wao kama wakimbizi walikuwa wanajaribu kuwapatanisha.

Hii ndiyo ilikuwa shughuli kubwa ya Afrika Alert.

Wakati nafika Brixton miezi michache iliyopita palitokea machafuko makubwa
sana hapo.

Sikuweza kujizuia kuunganisha vurugu za Afrika na zile za pale Brixton.

Babu tulipokuwa peke yetu alinipiga maswali mengi sana kuhusu Tanzania na
kwa hakika huwezi kuchoka kuzungumza na Babu kwani ni mtu wa maskhara
sana na mwepesi wa kujishusha.

Kwa mara yangu ya kwanza nilipata fursa adhimu kumsikiliza Babu kwa karibu
na pia nikamjua Babu na Mapinduzi ya Zanzibar kupitia kinywa cha Ahmed
Rajab.

Nilimsihi sana Babu kuandika historia ya mapinduzi na nikamwambia Ahmed
Rajab aandike kitabu kuhusu maisha ya Babu.

Inasikitisha kuwa Babu hakuwahi kunyanyua kalamu kuandika historia ya
mapinduzi na Ahmed Rajab sitosema kitu kwani huenda anaandika.
 
sana na mwepezi wa kujishusha.

Huyu Babu, si ndiyo alitunukiwa uprofesa huko majuu, ambapo kwa taratibu zetu hapa Tz isingewezekana. kule wanaangalia vitu vingi ikiwa ni pamoja na yale uliyokutana nayo katika maisha yako na maamuzi uliyoyafanya. sisi tumebinywa katika ufinyu wa "formal education" tu. Hongera sana "Mosaid" kwa "jani" hilo kutoka shajara yako. natamani ungeendelea kupakua...
 
Mind

Mindi,
Nikitulia nitakuwekea vitu vingine In Shaa Allah.
 
Mlamali Adam hatunae tena inna lillah wa inna ilaihi raajiun
 
Back
Top Bottom